Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Kilain hafai kabisa kusimamia kondoo wa bwana, hastahili kuwa kiongozi wa kanisa.

Tazama wewe unaweza kumuweka chui au Dubu katika zizi moja na wanakondoo wako?

Kilain ni chui, hafai kuwa zizin maana atakula na kuwamaliza wanakondoo wote badala ya kuwachunga.
 
naona safari ya matumaini ya bw mamvi sasa imenyooka kutoka monduli hadi magogoni. anachekeleaje!
Genius yule. Embu ingia Facebook account yake uone aliandika nini tarehe 13 mwezi huu, ndio utajua huu mchongo kachonga nani. Lowassa hawezekaniki!
 
...... Hapa ndio utaona Busara za Mk.were, ingawa akili za darasani nusu kijiko, ila busara za pwani zinamsaidia kupisha upepeo.

Kijamaa kimekaa kimya utafikiri kilikuwa hakijui kilichokuwa kinaendelea, na inawezekana kilishiriki. lakini utaanzia wapi sasa kumuunganisha?

Hapa wenye midomo mirefu, midomo imewahukumu, kuanzia Muhongo, maswi, Werema hadi Pinda.

Ni wakati muafaka Chenge akajiuzulu kule kwenye KATIBA pia.

Eneo alilosoma Mh. Deo F. kwenye ripoti ya PAC juu ya nukuu ya Mwl. Nyerere (R.I.P):

PAC said:
Mwanzo wa kunukuu.

"…kubadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Ndugu Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wangu kwa muda mrefu. Hakuwa amefanya kosa lolote; lakini nilitaka kumbadili na kuteua Waziri Mkuu mwingine. Nilimwita, nikamwambia hivyo. Tukakaa pamoja mimi na yeye, tukashauriana na kukubaliana nani anafaa kushika nafasi yake. Nikamteua Hayati Edward Moringe Sokoine. Najua kuwa watu wa aina ya Rashidi Kawawa ni adimu sana Duniani, hawazaliwi kila siku; hata hivyo
ni jambo la kushangaza kidogo kwamba viongozi wetu wa Mageuzi, hata bado hatujafa, wanaona kuwa ni kosa kuwakumbusha kuwa vyeo walivyonavyo ni dhamana.

Wanadhani kuwa Uwaziri ni Usultani; ukishakuwa Sultani utakufa sultani! Nadhani wanakosea. Nchi hii imewahi kung'oa Masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia Masultani wa kuchaguliwa, tutapanda mbegu ya Masultani wa kuzaliwa. Narudia; kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa Nchi isitikisike. Lakini
huwezi kumtimua Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi yenyewe
. Ni vizuri jambo hili likatamkwa waziwazi na likaeleweka sawasawa. Maana watu wengine wananong'ona nong'ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa nchi ni mkasa na balaa kwa Nchi yeyote ile."

Mwisho wa kunukuu.

Hiyo nukuu haijawekwa kwa makosa ina maana yake....kwani PAC walishidwa kuishia kwenye sentensi ya '.......kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa Nchi isitikisike.'

Maneno hayo ya mwisho kwenye nukuu , mimi naona ni
warning ya kiutu uzima kwa 'mkulu kulu'. PAC wanajua kabisa kuwa watanzania waleo hawaogopi tena nchi kutikisika.
 
Itv watarudia habari ikiisha tutaangalia sasa ingawa jioni walikata umeme
 
Ni kweli Mkombozi Bank ni ya kanisa na moja ya dhambi katika kanisa ni wizi na udanganyifu. Ifahamike kwamba bank hii inaendeshwa sawa na bank zingine chini ya usimamizi na miongozo kutoka central bank.
Kama kuna statutory/regulatory requirements ambazo Mkombozi Bank haiku comply wakati wote wa kufunguliwa kwa accounts na kufanya hizo transactions in question, naomba ziwekwe hapa tujadili. Vinginevyo hatutatukuwa tukiwatendea haki tukiwahukumu kuwa ni wakosa wakati hakuna kosa lililobayana ambalo wao kama bank wamelifanya.

Kuhusu askofu Kilaini na mwenziye, ni kwwli fedha walipokea. Mwenye ushahidi kwamba ffedha hizo walizipokea kwa niaba ya kanisa ama kanisa liliwatuma kuwa na huo ubia, aweke hapa. Kinyume na hapo ifahamike kwamba Kilaini ni viongozi wa kanisa lakini wao si kanisa. Ndiyo maana sheria imebainisha ni wakati gani mtumishi atahesabiwa kafanya kosa la kikazi linalomhusisha mwajili anayemwakilisha, ni wakati gani anakuwa ame commit personal offence, hata kama ni mtumishi.

NINAOMBA TUZITENDEE HAKI DHAMIRA ZETU KWA KUCHAMBUA HOJA KATIKA MISINGI YA UKWELI SAHIHI BADALA YA EMOTIONS NA MISUKUMO YA UTASHI WETU.

Tuko pamoja.


Mwenzetu tupo pamoja kweli au ndio mapenzi yamezidi. Yaani unasema mpaka sasa hakuna kosa lililobayana walilolifanya?
Ama kweli akipenda chongo huona kengeza
 
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
¡°... Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya IPTL ...¡±
Kamishna Mkuu wa TRA
¡°... TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo, kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa kwenda kule.
 
baada ya zitto na deo kusoma taarifa ya kamati ya pac waziri mkuu mizengo pinda hana kosa wala hajatajwa popote kuwa kaiba au katengeneza mazingira ya kuiba bado pinda anabakia na heshima yake ya uadilifu

waliyo iba pesa ya umma wawajibike wote pia ambao kamati ya zitto haijawataja iwataja maana kuna walichota bilioni 73 kwa mifuko na mabegi ambao hawa kutajwa ni vizuri wangetajwa na wao

Bado mnaendelea kutetea inefficiency iliyothibitishwa beyond doubt?
 
Hivi nani anasimamia shughuli za serikali?


Si yule mbunge wa ccm kule Katavi. Mtoto wa mkulima na waziri mkuu mwizi na fisadi mkubwa.

Jamaa anayeliaga bungeni badala ya kujenga hoja

Zee lina amlisha polisi kupiga hovyo raia tena wanapodai haki zao

Sasa nasema angó'lewe tu huyu mizengo kayanza Pita Pinda, maana hatuma maana nyingine sasa tumechoka na

ufisadi wake ila kumng'oa tu namimi nasema ang'olewe.
 
Dalali kivipi?, unaweza kuwa Dalali bila kupata chako?, Muhongo kapata ngapi ya udalali?, hebu onyesha makosa ya Muhongo yako wapi?

yeye kaingia Wizarani kakuta kuna kesi isiyoisha na Mkono kila siku anakula pesa za Tanesco hakuna kinachofikia muafaka,

kama waziri akawakutaniaha Wadai na Wadaiwa wamalize tofauti zao, yeye kakaa pembeni, sasa ulitaka Muhongo kama Waziri afanye nini, azidi kumgawia Mkono pesa ya uwakili wakati issue inaweza kuisha kwa Mdai na Mdaiwa kukutana?

Wizi wa ESCROW UPO NA KWELI PESA YA WANANCHI IMEIBIWA, NA KUNA WATU WANAPASHWA KUWAJIBISHWA, LAKINI NI MKITENDO CHA AIBU KWA MTU KAMA Zitto, kutafuta mwanya wa kumuingiza Muhongo Kwenye hiyo report Muhongo anafit vipi vipi kama sio kwa interest za Zitto na Genge lake? yaani bila Muhongo huo wizi usingefanyika?
Muhongo kama waziri angesimamia hizo pesa zisitolewe kutoka kwenye account,aondoke tu akafundishe folds na faults
 
.....Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 106 na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu. Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

My Take: Hapa tumeshajua NGEDERE ni nani na MWIZI ni nani! Kwishnei. Tujifunze kuacha HOJA itawale na siyo NGUVU na MABAVU. Mie napendekeza kwa mamlaka ya uteuzi huyu MWIZI AVULIWE UJAJI!
 
ITV watarudia report baada ya taarifa ya habari, kutokana na kukatwa kwa umeme eneo kubwa la nchi
 
aibu mahakama kuu kuweka katazo kuzuia kashfa
ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya
mabilioni kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow.

Mahakama zinatumika vibaya hizi. Acha wafe na aibu zao.
SPIKA kawatupilia mbali ujingaujinga wao.
 
Back
Top Bottom