Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Mungu awabariki PAC!! spika Makinda pia katutendea haki leo, pongezi zimuendee. Kinachobaki sasa ni Pinda na team yake kuachia ngazi kabla jogoo hajawika
 
bado! kuwafukuza kazi na kurudisha pesa kwa mtazamo wangu bado si suluhisho la ufisadi! nchi imeliwa imekwisha sasa!tunahitaji kifungo ndo wataacha!
Hahahah lakini kina ZZK wametimiza kazi yao kwa weledi na ufasaha mkubwa.
 
Subiri, yote yanajibika na haondoki mtu.

Huyu ajuza nae vipi? Kwa sasa unakoelekea naona ujira wa buku 7 utakosa maana naona unaleta mambo ya CCM maslahi hapa wakati wenye chama washaamua watu na uchafu wao wawajibike.

Yajibike yasijibike sio hoja - hapa serikali na taasisi zake zimechafuka beyond repair, haisafishiki. Njia pekee iliyo wazi ni wao wote kujiuzulu nafasi za kisiasa na kwa wale watendaji kufukuzwa kazi, then wooote hao washitakiwe na kufilisiwa
 
Hata jana ulisema report haisomwi na leo ikasomwa.
Watumwa mnaofanya maamuzi kwa kuongozwa na tumbo huwa hamuamini mpaka muone mmeshikwa mikono kwenye sahani na kuambiwa kuwa leo ndo mwisho wenu wa kula.


Ha ha ha ha hii comment imenigusa na kunichekesha kwa namna ya pekee
 
Na huku unakujaga!
Jiangalie utapoteza ID huku.
Mi ni Profesa, natumia usafiri Huu kwa muda.
UsAfiri mwingine upo
mtaroni kupitia jukwaa hili hili.

Mimi huku ni kwa sababu maalum kama leo...sipawezi kabisa
 
Asingeweza kusimamia yeye Hizo pesa kwani Tayari zilishakuwa chini ya usimamizi wa BOT, kwenye mchakato wa kutoa hizo pesa ulihusika Mwanasheria mkuu, Hazina, TRA, Ikulu, TISS of-course na wizara yake, na kwenye Wizara yake muhongo sio mtendaji, mtendaji ni Katibu na ndiye aliyekuwa kwenye hayo mawasiliano

Kiukweli sijaona Mantiki ya Jina la Muhongo kuwemo kwenye hiyo report,

Kutokana na report ya PAC Muhongo ndiye aliyemleta Singasinga na kumkukutanisha na huyo bwana wa VIP.
 
Samahani wadau mimi sijaona Pinda, Muhongo, Maswi, Werema, Ndulu, na Mbowe wanavyhusika. Sijaona hii report ikibainisha hela zinazopaswa kurudi.
report umeisoma au umepitisha tu macho?

Mheshimiwa Spika, Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya
juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama
masharti ya Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu cha
90(2) yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya
‘approval’’ ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni
mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za
malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.
Mheshimiwa
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati
na Madini amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge lako
tukufu na Taifa kwa ujumla kuhusiana na Fedha za Akaunti ya
Tegeta ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha
za umma.

Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki
Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa
kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe
Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Waziri Mkuu
kuhusiana na suala hili, Kamati iliipitia kwa umakini Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyoainisha
Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu na kubaini kuwa, kwa mujibu wa
Ibara ya 52 (1)
na kwanini una lazimisha mbowe atajwe? mna nini nyinyi wachumia tumbo wa CCM?
 
Taifa kwanza lifanye kazi yake,halafu kanisa litasimama katika zamu yake#bring back our mkwanjazii
 
Mim nalia na viongozi wa dini "toa ndugu toa ndugu ulichonacho mungu anakuona mpaka moyoni mwako" ,sasa kweli amewaona ,vipi mlitoa fungu la kumi? Kwa hizo fedha za madafu mlizogawana kwenye viloba ,nchi hii itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno makubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

Mkuu umewaza mbali sana. Kilaini na Nzigirwa hawakutoa zaka wallah. Aisee hii inavutia sana...

Halafu, hivi hawa wachunga kondoo walilipa kodi kwa zawadi walizopewa? Ya kaisari na apewe...
 
Hakuna Waziri Mkuu Yeyote Chini Ya Kikwete atabaki salama.

Honestly Pinda Is Inocent.

Mkilazimishia ataondoka .. Huyo ajae .. ATAKUWA SALAMA?

Kauri zake ndo zimemponza. Viongozi wetu wanafanya kazi zao bora liende tu. Hawako makini. Unapokuwa umepewa ofisi kubwa hivyo inabidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa.
Ripoti haijamtaja kuhusika kwa wizi huu moja kwa moja ila to be honest wizi wa namna hii unapotokea na mawaziri kugawana hela kwa kiwango hiki bila waziri mkuu na rais kujua ina maana hawastahili kuongoza nchi. Hawafai kabisa.
Tuwe wakweli ndugu zanguni.
Hawa viongozi wakubwa wa nchi hii WAMEHUSIKA KWA KIWANGO KIKUBWA. Nchi hii tunajua deal zinavyopigwa.
Hata rais alistahili kuwajibika tu ktk hili, ataendelea kuwepo ktk kiti chake kwa kuwa hakuna namna ya kumwajibisha. Ila ataongoza nchi hii kwa aibu kubwa.
Mnyika aliwahi kusema rais ni dhaifu na hili linathibitika kwa matukio kama haya. Serikali yake inaanguka kwa mara ya pili.Huu ni UDHAIFU na AIBU kubwa kwake na kwa familia yake lakini na kwa Watanzania kwa ujumla.
Mwl Nyerere akifufuka leo atatuadhibu Watanzania kwa kutokumsikiliza pale alipomkataa JK kuwa hawezi majukumu makubwa ya kitaifa.
Na tunataka kufanya kosa jingine kubwa maana watu wanaanza kumpigia chapuo Lowasa awe rais ajaye. Hili litakuwa kosa jingine la kitaifa.
WATANZANIA TUWE WASIKIVU.
 
Kuna mambo sijayaelewa vizuri na taarifa hii ya Zitto..kwamba AG kaipotosha benki Kuu kuhusu kodi ya VAT...tangu lini kazi hiyo ya assessment ya VAT ikafanywa na AG? Kwani Wizara ya fedha au TRA hawakuwepo kutoa ufafanuzi. Kamati ya Zitto ina uelewa upi wa Sheria kubaini kuwa hukumu ilipotoshwa? Nataka kuelewa tu!!

Kama hujaelewa repoti hapa utaelewa nini?

Subirini tu tuwafagie wote ndio utalewa hujui ni kiasi gani mioyo yetu ina huzuni.
 
Jamani aibu saaaaana tena dhambi hebu angalieni kwa hao walaji wa fedha za escrow wenzetu waislamu hawapo ila sisi wakristo ndio tumetia aibu jamani

Kweli mi huwaga nawashangaa waislam wana maisha duni sana, kumbe sisi ni mijizi ndo mana tuna afford kuishi maisha bora kuliko wenzetu!
Huku Mbezi na Mikocheni wagalatia tumepastawisha kumbe ni hela za wizi! Huu ni uonevu! Na aibu mno!
Ona Tiba ana shule nzuri eti ya Yatima huku anaifund na wizi wa fedha ya umma!
Kwa nini wakristo Rugemalila na cos wasingepeleka fedha hizo shule za Kata za Mbagala na Buguruni?
Ukimkuta na rozari kuubwa utadhani mnyororo wa kufungia Mbwa. Kumbe jizi tu!
 
KIKWETE awajibike!!!!!!!! To cut a long story short.

He's the spine of the most corrupt presidency in our history. Even so much as his family and friends are the hub of untold crimes of crimes, money laundering, drugs & human trafficking, vote rigging, piracy..... and the likes.

I don't know HOW but I know WHY he should go.
 
Hahahahahaaaaa upo? Nakukumbuka sana ulivyokua Unakataaa na kuutetea huu wizi. Kazi unayo, maana suala sio kujibika suala ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu.

Nimependa ubunifu wako...wa attachment....ila title ya Movie inabidi iboreshwe zaidi, mfano "The Bunge Claw"
 
Back
Top Bottom