Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Kilain hafai kabisa kusimamia kondoo wa bwana, hastahili kuwa kiongozi wa kanisa.

Tazama wewe unaweza kumuweka chui au Dubu katika zizi moja na wanakondoo wako?

Kilain ni chui, hafai kuwa zizin maana atakula na kuwamaliza wanakondoo wote badala ya kuwachunga.
 
naona safari ya matumaini ya bw mamvi sasa imenyooka kutoka monduli hadi magogoni. anachekeleaje!
Genius yule. Embu ingia Facebook account yake uone aliandika nini tarehe 13 mwezi huu, ndio utajua huu mchongo kachonga nani. Lowassa hawezekaniki!
 

Eneo alilosoma Mh. Deo F. kwenye ripoti ya PAC juu ya nukuu ya Mwl. Nyerere (R.I.P):


Hiyo nukuu haijawekwa kwa makosa ina maana yake....kwani PAC walishidwa kuishia kwenye sentensi ya '.......kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa Nchi isitikisike.'

Maneno hayo ya mwisho kwenye nukuu , mimi naona ni
warning ya kiutu uzima kwa 'mkulu kulu'. PAC wanajua kabisa kuwa watanzania waleo hawaogopi tena nchi kutikisika.
 
Itv watarudia habari ikiisha tutaangalia sasa ingawa jioni walikata umeme
 


Mwenzetu tupo pamoja kweli au ndio mapenzi yamezidi. Yaani unasema mpaka sasa hakuna kosa lililobayana walilolifanya?
Ama kweli akipenda chongo huona kengeza
 
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
¡°... Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya IPTL ...¡±
Kamishna Mkuu wa TRA
¡°... TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo, kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa kwenda kule.
 

Bado mnaendelea kutetea inefficiency iliyothibitishwa beyond doubt?
 
Hivi nani anasimamia shughuli za serikali?


Si yule mbunge wa ccm kule Katavi. Mtoto wa mkulima na waziri mkuu mwizi na fisadi mkubwa.

Jamaa anayeliaga bungeni badala ya kujenga hoja

Zee lina amlisha polisi kupiga hovyo raia tena wanapodai haki zao

Sasa nasema angó'lewe tu huyu mizengo kayanza Pita Pinda, maana hatuma maana nyingine sasa tumechoka na

ufisadi wake ila kumng'oa tu namimi nasema ang'olewe.
 
Muhongo kama waziri angesimamia hizo pesa zisitolewe kutoka kwenye account,aondoke tu akafundishe folds na faults
 
.....Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 106 na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu. Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

My Take: Hapa tumeshajua NGEDERE ni nani na MWIZI ni nani! Kwishnei. Tujifunze kuacha HOJA itawale na siyo NGUVU na MABAVU. Mie napendekeza kwa mamlaka ya uteuzi huyu MWIZI AVULIWE UJAJI!
 
ITV watarudia report baada ya taarifa ya habari, kutokana na kukatwa kwa umeme eneo kubwa la nchi
 
aibu mahakama kuu kuweka katazo kuzuia kashfa
ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya
mabilioni kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow.

Mahakama zinatumika vibaya hizi. Acha wafe na aibu zao.
SPIKA kawatupilia mbali ujingaujinga wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…