Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

asirud asijeendeleza uhongo wake

Kwa wale wasiofahamu, Muhongo ameshastaafu. Umri wake ulishafika kitambo, labda aombe mkataba. Na kwa jinsi alivyokuwa arrogant na kwa aibu kama hii hawezi kurudi Mlimani, labda wanaweza kumpa kazi UDOM
 
Haya kwa wale ambao hawaiona wala kusikia riport hiyo kwa sababu ya kukatika kwa umeme ITV watairudia mara baada ya taarifa ya habari
 
Hivi kuna tofauti gani kati ya mwizi,jizi,jambazi na fisadi!msaada tafadhali
 
Duuu hawa 'watumishi' wa Mungu hawatosheki na sadaka, matoleo na fungu la moja kwa kumi hadi washadidie fedha haramu!!!

Hata mie nimeshangaa sana kwa kweli. Lakini hawa viongozi wa dini wamekuwa wakijihusha hata na madawa ya kulevya na wamekuwa wakisemekana muda mrefu sana. Dini zingine bwana!!!! Sasa waumini wao wanawaambia nini???
 
kwa mfumo wa nchi hii usitegemee mkombozi bank kama watafanywa kitu
 
Anayajua na vyovyote vile alibariki lakini yeye ni a homestead pumpkin kuling'oa yataka tahadhari ya hali ya juu vinginevyo we will suffer the consequence

Hili shuzi ni la PUNDA usimuingize mkulu
 
Muhongo kama waziri angesimamia hizo pesa zisitolewe kutoka kwenye account,aondoke tu akafundishe folds na faults

Asingeweza kusimamia yeye Hizo pesa kwani Tayari zilishakuwa chini ya usimamizi wa BOT, kwenye mchakato wa kutoa hizo pesa ulihusika Mwanasheria mkuu, Hazina, TRA, Ikulu, TISS of-course na wizara yake, na kwenye Wizara yake muhongo sio mtendaji, mtendaji ni Katibu na ndiye aliyekuwa kwenye hayo mawasiliano

Kiukweli sijaona Mantiki ya Jina la Muhongo kuwemo kwenye hiyo report,
 
Subiri, yote yanajibika na haondoki mtu.

Hata jana ulisema report haisomwi na leo ikasomwa.
Watumwa mnaofanya maamuzi kwa kuongozwa na tumbo huwa hamuamini mpaka muone mmeshikwa mikono kwenye sahani na kuambiwa kuwa leo ndo mwisho wenu wa kula.
 
Ndugu zangu
hao waliotajwa ni sehemu ndogo sana ya uozo uliopo nchini.

Kwa mfano, hivi serikali inawezaje kulipa kampuni isiyojulikana?

Kwa taratibu za nchi nyingine, kama una kampuni inayokwenda kuwekeza, ni lazima kwanza ubalozi wa nchi hiyo uthibitishe kampuni husika kuwepo na kusajiliwa kutoka nchi husika.
Na kwamba kampuni hiyo inafanya kazi zake bila kuwa na doa.

Huwezi kwenda kusajili kampuni Uingereza bila vyombo vya usalama kujiridhisha kwanza.

Hii maana yake ni nini!
1. Kwamba kuna tatizo katika idara ya usalama nchini. Ima hawajui wanafanya nini au nao ni sehemu ya rushwa
2. BRELA ifungwe. Ni taasisi hiyo iliyosajili Richmond hewa, na wakati huu imehusika bila kujiridhisha
3. Mfumo wa watendaji wetu ni hovyo. Hivi unawezaje kuidhinisha malipo kwa kampuni usiojua ipo au haipo

Haya yote yapo chini ya mwamvuli wa Rushwa. Kwamba, kama katibu mkuu wa wizara au waziri au waziri mkuu wanaweza kutetea uhalifu, mkurugenzi wa idara anaweza kusajili kampuni hata ya kigaidi ilimradi tu amepewa kitu.

Ukiangalia kwa undani, mfumo mzima umekufa. Tunaishi kwa solar energy maana uzembe huu ulijulikana si kwa waziri mkuu ni zaidi ya hapo. Hivi waziri mkuu, mkuu wake wa kazi ni nani. Na je boss alijua, na alifanya nini kwa suala hili.
 
Kuna mambo sijayaelewa vizuri na taarifa hii ya Zitto..kwamba AG kaipotosha benki Kuu kuhusu kodi ya VAT...tangu lini kazi hiyo ya assessment ya VAT ikafanywa na AG? Kwani Wizara ya fedha au TRA hawakuwepo kutoa ufafanuzi. Kamati ya Zitto ina uelewa upi wa Sheria kubaini kuwa hukumu ilipotoshwa? Nataka kuelewa tu!!
 
Kazi sio kusoma report kazi ni kuchukua hatua stahiki,ila hapa tulipofikia sio pabaya sana...
 
Kweli tumekosea Mungu atasamehe taasisi zetu za dini zinapindisha maadili wanayofundisha Hili la Mkombozi ni funzo wengine tujisafishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…