Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

dah, hatari sana hii. rudisha tu baba askofu nenda katubu pia ila usirudie tena kosa.
Kama JR alisema anakupa sadaka basi siku nyingine aje atoe kanisani moja kwa moja.
 
Hakuna mtu aliyepokea huo mgao ambaye hakujua kama zile pesa ni chafu.
Askofu unawekewa milioni 80 tena kwenye akaunti yako binafsi alafu usijue hizo pesa umepewa kwa sababu zipi?

Ninachokiona kuhusu maaskofu, inaonekana kulikuwa na 'upinzani' katika kutumia Mkombozi bank kupitishia hizo pesa, mgao waliopewa akina kilaini ni ili wafanikishe kulegeza 'upinzani' huo.
 
duu awa maharamia wahukumiwe ipasavyo iwefundishoo maana imekua ndo mchezo hadi kanisa daa uu ufuskaaaa
 
mm nashindwa kuwaelewa kabisa .....inamaana hizi pesa ni zao binafsi...nzigilwa yy kama yy ...na kilaini yy kama yy.au.....shame kwakweli tuhuma hizi
 
Wanigambila stupid mno,infact actually mazima kwakweli ututake radhi wahaya kwa kupaita Bukoba porini.
Vinginevyo ntamuagiza mtoto wangu Kokuberwa aliyegraduate masters ya sheria nchini Urusi akuburuze mahakamani.

Hahahaa haaaa
 
Mimi si mwanasiasa, lakini nilikupenda sana Zito. Hivi karibuni nilianza kupata mashaka na mwenendo wako wa kisiasa. Leo umenisuuza nafsi!! Ahsante Zitto.

usipende kusikiliza maneno ya watu ndugu lakin ss nadhan ni mda wa kumtambua nani ni mzalendo wa kweli wale waliokua wanamuita msaliti wako wapi
 
Hatari sana.

Ndiyo maana kwa wenzetu Wazungu wasiopenda unafiki, Makanisa yanabadilishwa na kuwa Restaurants.

Sioni logic ya kutaja makanisa hii ni esue ya individual parson. Stop nonsense.
 
Hakuna evidence kama hawa waliopewa walijua ni za escrow

NI akili ya binadamu yupi huyo anapokea pesa ambayo hajaifanyia kazi, bila kujua imetokea wapi? na madhumuni haswa ya kupewa pesa, bila kujua future implications ya pesa ya bure.

Duniani akuna kitu cha bure with xception kutoka kwa mzazi. Wote waliopewa mgao wa pesa wakamatwe na kufilisiwa thn wakajitetee mahakamani.
 
Hivi hii haiwezi kuwa sadaka ya ondoleo la dhambi kweli? Maana kwa dili hili toba ya ruge haikuwa ndogo.
 
Stanbic zimeonekana Accounts transfer without names kitu ambacho ni kosa. BOT na Takukuru wameagizwa washughulikie hilo PAC haina mandate ya kufanya huo uchunguzi.
 
Jamani Chenge aondoke sasa! Dah!
Halafu si ana katoto ka kike huyu kalikua kanamfwata mahakamni kipindi kile aue wale hawara zake kwenye bajaji?

We have heard too much of this guy. It is high time now he rested so that we have the opporrunity to hear about other people. After all he is not the only pebble on the beach.
 
walisema Mbowe eti naye yumo sasa yapo wapi? Cc: msalani, simiyu yetu, faizal fox, lizabon.
Mkuu hii kitu haijaisha. Wamo wengi. Kuna zile transaction za mamilioni ya dola na mabilioni ya shilingi ambazo hazina majina. Hizo ndizo zinafanyiwa kazi ya kiuchunguzi na PCCB. Report ya PCCB bado, tuendelee kusubiri
 
Bi Mkubwa uchunguzi umefanywa na Taasisi siyo ZZK, utamuonea bure mzee wa hammer yeye anawakilisha uchunguzi

Isitoshe huo ushahidi wa baruwa, nyaraka na vimemo hawana jeuri ya kuvikwepa

Mbaya zaidi kila kitu nifeki ndiyo maana walitaka kutumia mahakama kuficha maovu yasisomwe yakajulikana.

Wakati mwingine kubari kushindwa.

Naongelea uwasilishaji, si huo uchunguzi. Na pia tumesikia upande mmoja mpaka tungoje upande wa pili wanasemaje.

Mpaka sasa sijaona kilichowasilishwa ambacho hakijibiki.
 
Hii ripoti nimeisoma mstari kwa mstari kwa pages zote 115 as ilikuwa interesting ambayo baadaye imenipa hasira. Viongozi waliopewa dhamana bado wanakuja mbele ya bunge na umma kuongopa juu ya hili suala. Kumbe nyuma ya pazia wana deals zao. Hawa viongozi wote wanatakiwa kuadhibiwa vikali hata kama ni kunyongwa.

Prof. Muhongo ni ndugu yangu but kwa hili....OGWO NI MUJIGO GWAO, NUFWE OMWENE (huo ni mzigo wako, kufa mwenyewe).
Mh. Werema, uheshimiwa haukufai hata chembe, tena wewe ndo unatakiwa adhabu ya kifo ianzie. Serikali inakosa mapato, madawa hospitalini hamna kwa sababu ya uzembe wako. You need to be prosecuted.

Mzee wa "Nimo kimya kimya" hapa hana ujanja, yeye pia alidanganya umma kwa makusudi as alikuwa anajua A to Z kuhusu process zote. Hivyo anapswa kuwajibika na kushtakiwa pia.

JK, ningekushauri uondoke tu mapema maana nchi imekushinda several times. Pamoja na kwamba hujatajwa kwenye ripoti, lakini ulikuwa unajua each and everything. Na wewe umeshindwa kuilinda katiba ya JMT. You also need to go.
 
Well,
Natafakari hatua za stahiki kuchukua dhidi ya Stanbic Bank binafsi. Nitataka maelezo ya kina kwa nini nisifunge akaunti na kuachana na benki yao Jumatatu tarehe 01/12/2014.

Tuipinge rushwa/ufisadi/dhuluma na CCM popote hata pale penye masalahi yetu binafsi huo ndio uzalendo wa kweli wajameni.
 
Huu mfumo unatia shaka kweli. Kuratibu, kugawiwa, kunufaika. Mfumo "......" At work.
Ona hii...

MILIONI 319 ZAPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA KATOLIKI LA MAKONGO JUU JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (katikati), akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Makongo Juu iliyofanyika kanisani hapo Juni 29-2014 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira, Mrs Rugemalira, Paroko wa Parokia ya Makongo Juu, Joseph Masenge, Mwakilishi wa Mkombozi Commecial Benki, Edina Lupembe na Respius Didace.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Wa pili kulia), akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Makongo Juu iliyofanyika kanisani hapo Juni 29-2014 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira, Mrs Rugemalira ambao ni wakazi wa Makongo, Paroko wa Parokia ya Makongo Juu na Joseph Masenge

Wadau mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hiyo.

Wadau mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hiyo.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Paroko wa Parokia ya Makongo, Joseph Masenge wakiwa katika picha ya pamoja na watoto walioahidi kila mmoja kuchangia sh.100,000 za ujenzi wa kanisa hilo.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo akiwaongoza wageni waalikwa wakati wa kuchukua chakula.
 
Back
Top Bottom