Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Jamani aibu saaaaana tena dhambi hebu angalieni kwa hao walaji wa fedha za escrow wenzetu waislamu hawapo ila sisi wakristo ndio tumetia aibu jamani

Nyerere aliwahi kusema, " Ni kweli baraza langu la Mawaziri lina Wakatoliki wengi, huyu mmoja ameendelea kidogo, ana wanawake wawili", akimaanisha kuwa, ukatoliki sio jina, uislam sio jina. Mara unapokwenda kinyume na taratibu za imani yako,unakuwa umetoka ktk msitari, kurudi mpaka utubu.

Sasa hii mijizi yenye majina ya Ulaya haiwakilishi imani ya Kikristo, tukiangalia majina yetu dhidi ya vitendo vyetu, hakuna hata mmoja anayepaswa kuwamo ktk dini au imani aliyomo. Hata hivyo hao wenye majina ya Uarabuni nawapa hongera kwa kutokuwamo ktk hii orodha chafu.
 
alikua anajua kila kitu kinachoendelea akakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote, alizembea kazi yake kam waziri mkuu alishindwa kusimamia serikali ipasvyo ktiba inavyompasaa. hakuiba ila alisidia katika wizi, he must go
 
Mkombozi bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal; no question about it. Stanbic bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal, no question about it. Ila walijua na pengine wameshagawa fedha kwa mtindo huo mara nyingi, kuwa hakuna sheria yoyote itakayofanya kazi. Tatizo la nchi yetu si kutunga sheria nyingi zaidi na kuongeza vyombo vya utekelezajia. Tatizo letu ni kuwa taasisi ambazo zinatakiwa kuzitumia sheria hawazitumii na hivyo inaonekana kama vile hazitoshi. Tatizo liko kwenye enforcement ya sheria. Waziri mkuu kila siku ilikuwa ni kudanganya kuwa hiyo ni hela ya binafsi akijua wazi kuwa si kweli. Na aende tuuuuu!! Useless.

sure kipima pembe.no enforcement.watu wanaiba hadharani na wahusika wa kuwabana wanakula goodtime zao.who care.
waziri mkuu na apigwe tuu
 
Kwani ile ripoti ya Richmond Lowassa alitajwa wapi kuwa kahusika? Asikimbie kivuli chake, aende kurina asali Tu. Ajiuzuru tu, tumechoka.
 
Mimi kama mwanakanisa naomba tu wawajibishe hawa maaskofu wawili maana ni aibu kwa kanisa na uzuri baba askofu pengo ulishasema jamaa tukaae mbali na hawa mafisadi. Sasa tunaona sasa na uliwah kusema wasikaribishwe ndani ya makanisa. Wakatoliki tuzidi kuwaombea mungu awasamehe na wahamishwe tz
 
Report ya PAC inasema wazi kuwa Waziri Mkuu Pinda alikuwa anajulishwa kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kuhamisha fedha za Escrow. Pia hela zilizohamishwa kutoka mkombozi zingine majina ya waliolipwa yamefichwa
 
du yani mtu mmoja anapewa 1.6bilioni . wakati selikari inadaiwa na bohari la madawa. wa Tanzania wanakufa kwa kukosa madawa huku wengine wanachota fedha kama maji kwenye kisima
 
Movie haijaisha mpaka tusikie upande wa pili, hoja za Zitto zimekaa kishabiki shabiki, mapendekezo pia yamekaa kishabiki, mpaka neno dalali alilotumia Mhongo kwa Mengi limerudiwa kuelekezwa kwa Mhongo.

Yote yanajibika tena kiufasaha kabisa.
Huna lolote wewe....
Una roho ngumu , subiri kama kuna atakayesalia katika hao wezi.
Wezi wakubwa nyie.
 
Back
Top Bottom