Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
kocha kaona atoke na so far bado sekunde na hatujafungwa na tupo pungufu. Balua anashambulia kama tupo 12 uwanjani.Naunga mkono, mavambo hakupaswa kutoka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kocha kaona atoke na so far bado sekunde na hatujafungwa na tupo pungufu. Balua anashambulia kama tupo 12 uwanjani.Naunga mkono, mavambo hakupaswa kutoka.
Kula NYAMA NYAMAZA. 🤣Pia unaunga mkono kwamba Ngoma baada ya kupewa red card, alitakiwa afanyiwe substitution
Unataka kuja kupiga na wewe!!Matuta bado?
Epuka matapeli. Giants wapo club bingwa sio shirikishoWana timu nzuri ila wamekutana na giant wa Tanzania
Big Up.
Mchezo wa Ngao ya Jamii kutafuta mshindi wa tatu mchezo unachezwa uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Coastal Union dhidi ya Simba SC.
Dakika 2, Mpira umeanza kwa kasi kubwa sana.
Dakika 5, Simba wanaumiliki mpira sana na kufanya mashambulizi kwenye lango la Coastal.
Dakika 8, Mutala anakosa goli akiwa katika nafasi nzuri sana .
Dakika ya 11, gooooool ,Kalabaka anawapa uongozi Simba SC
Dakika 15, Simba bado wapo kwenye kilele cha kumiliiki mpira.
Dakika 17, Masoud Kalabaka anapiga shuti kali sana ila mpira unapenda kutoka nje.
Dakika 22, Simba wanaendelea na mashambulizi makali sana kwenye lango la Coastal
Dakika 24, wanafanya shambulizi kali kupitia Lucas Kikoti ila wanashindwa kuitumia nafasi hiyo ili kuzawazisha goli.
Dakika 27, Steven Kukwala anakosa nafasi ya wazi kabisa hapa oh.
Dakika 31, Hadi sasa Simba wameendelea kufanya vyema mbele ya Coastal
Dakika 32, John Makwata anaruka kichwa safi sana lakini mlinda mlango wa Simba anawaweka Simba salama baada ya kudaka mpira huo.
Dakika 38, Mukwala anakosa nafasi ya wazi tena yeye na kipa.
Dakika 40, Mukwala anakosa tena nafasi hii sasa ni balaa kutoka kwake.
Zimeongezwa dakika 3 ili kutamatika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimetamatika na Simba anatoka akiwa kifua mbele Coastal Union 0- 1 Simba SC.
Kipindi cha pili kimeanza tusubiri dakika 90 zitakuwaje je ni Simba SC au ni Coast Union ataibuka mshindi wa 3.
Dakika 46, Coastal wanafanya mabadiliko Gwalala anaingia anatoka Baraki.
Dakika 49, Chazi Haua anafanya shambulizi kali sana ila golikipa wa Coastal anawaokoa wenzie
Dakika 54, Coastal wamepata faulo freekik hiyo inapigwa na Kikoti lakini mpira umegonga mwamba.
Dakika 55 Simba wanafanya mabadiliko Mashaka anaingia anatoka Mukwale lakini Ngoma anaingia Mavambo anatoka.
Dakika 63, Coastal Union wanafanya mabadiliko Lucas Kikoti anakwenda nje Cosmas anachukua nafasi yake.
Simba wanafanya mabadiliko Shabalala anatoka nafasi yake inachukuliwa na Numa.
Dakika 68, Kelvin Kijili anakosa nafasi nzuri sana hapa ya kuwapatia timu yake Simba SC goli la pili
Dakika 78, Coastal wanakosa nafasi ya wazi kabisa ya kusawazisha
Dakika 79, Ngoma anapata kadi ya njano.
Dakika 80, Simba wanafanya mabadiliko, Joshua Mutale anatoka nafasi yake inachukuliwa na Kibu Denis.
Dakika 83, Ngoma anapata kadi nyekundu baada ya kumfanyia faulo mchezaji wa Coastal Union.
Dakika 85, Mashaka anapata kadi ya njano baada ya kufanya faulo kwa mchezaji wa Coastal Union
Dakika 86, Banza anapata kadi ya njano baada ya kumchezea faulo Kijili.
Dakika 89, Gwalala anapata kadi ya njano
Dakika 4 zimeongezwa kumalizika kwa dakika 90 za mchezo wa leo.
Makosa ya leo yatatugharimu sana kwenye ligi. Tumejiweka kwenye mazingira ya timu ndogo kutuona wa kawaida na hivyo kutoingia na woga wanapocheza na Simba. Kocha kazingua na wachezaji wamezingua pia.Huu mpira balua angeachia moja kwa kibu ingekuwa bora zaidi, si mbaya kajitahidi kapiga on target, ila angepasia ndio ingependeza zaidi.
Acheni visingizio mchezaji mbovu tu.Marefa wengi wa bongo ni Yanga..huyu dogo kayoko mwenye kukodoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango ni Yanga lialia
Hakuna cha kazi nzuri hapo. Ukweli tuuseme. Wamefanya makosa mengi kabisa ikiwemo kupoozesha mpira wakati wa kushambulia. Wanahitaji kubadilika.FT. Kazi nzuri vijana wa Simba
Kumekucha, kumekuuuchaaaaaaMakosa ya leo yatatugharimu sana kwenye ligi. Tumejiweka kwenye mazingira ya timu ndogo kutuona wa kawaida na hivyo kutoingia na woga wanapocheza na Simba. Kocha kazingua na wachezaji wamezingua pia.
Furaha pekee kwa Simba leo ilipaswa kuwa mchezo mzuri wenye ushindi mnono.Hii kushika nafasi ya tatu haina mvuto kwa kweli!!
Hii timu angepewa Mgunda ingekua bora sana sijajua kwanini Mo na team yake hawajawaamini ila kwangu Mimi Mgunda kwa mchezaji yoyote lazima atakua mzuri tu kwakua anakupa uhuru wakuonyesha kipaji chakoSimba timu tunayo😂
Tumshukuru Sasi kwa kutuondolea aibu
li-komwe leo amekuwa lisemaji la costiIla Ally Kamwe kanifurahisha