Mkuu kwanza elewa katika mpira mafanikio ya kwanza ni kupata taji na ndio lengo la kila shabiki kufurahia kuona timu yake inakusanya taji kwavile mafanikio ya kipesa hayawezi kugaiwa kwa kila shabiki.
Mpaka sasa Yanga anagombea mataji mawili kati ya mataji matatu aliyoshiriki ( CAFCL, ligi kuu na CRDB FA) wakati Simba ikiwa inagombea taji moja tu kati ya mataji matatu aliyokuwa anashiriki. Siwezi kusema kugombea taji ni lazima uchukue lakini tayari Simba kabakisha shindano moja tu ambalo akilikosa anakuwa kamaliza msimu patupu kwa mara nyingine tena.
Kwenye mashindano ya klabu bingwa uzoefu haufanyi kazi bali ni ubora, mbinu sahihi dhidi ya mpinzani ndio hufanya kazi. Simba ilitolewa hatua ya robo fainali na timu ya Kaizer Chief ambayo hawakuwa na mwendelezo wa kushiriki mashindano ya CAF kwa muda mrefu sana tofauti na Simba ambao mara kwa mara wameshiriki mashindano ya CAF. Alkadharika Belouizdad pamoja na uzoefu wao wa kucheza robo fainali mara kwa mara ila wanashindwa kufuzu robo fainali kwa kutolewa na Yanga katika makundi hivyo achana na mambo ya uzoefu bali deal na current form kama navyokusisitiza mara kwa mara, mpira ni current form sio mambo ya uzoefu.
Umeongelea upande wa mashindano ya kimataifa twende in terms of numbers:
Mara ya kwanza Simba kuanza kufanya vizuri mashindano ya CAF ilikuwa ni msimu wa mwaka 2018/2019 ambapo ndio walianza kuwa na muendelezo wa kuingia mara kwa mara katika mashindano ya CAF.
Kutoka msimu wa 2018/ 2019 hadi msimu huu wa 2024/2025 Simba wamevuna point 48 katika misimu 7 ambapo ndani ya misimu 7 misimu 5 imefanyika performance ranking hivyo anapata wastani wa poont 9.6 kwa kila msimu
wakati Yanga wameanza kuingia katika kufanya vizuri CAF msimu wa 2022/2023 na kufanya muendelezo kwa misimu mitatu mfululizo na kupata point 34 zilizopatikana kwa performance ya misimu mitatu hivyo Yanga anakuwa na wastani wa point 11.333 kwa msimu. Kwa maana nyingine ni kwamba Yanga imepitwa na Simba lakini wanakuja kwa kasi katika kupata point za CAF na kuwa na wastani mzuri kama wataendelea kuwa na muendelezo.