Full Time: Pyramids FC 2 - 1 Mamelodi Sundowns FC | CAFCL Final | 2nd Leg | 30 June Stadium | 01-06-2025 (Ag 3 -2) Pyramids Mabingwa

Full Time: Pyramids FC 2 - 1 Mamelodi Sundowns FC | CAFCL Final | 2nd Leg | 30 June Stadium | 01-06-2025 (Ag 3 -2) Pyramids Mabingwa

Attachments

  • FB_IMG_1748196804254.jpg
    FB_IMG_1748196804254.jpg
    46.4 KB · Views: 17
Hayo malengo ni kwa mujibu wa nani mbona kama mashabiki wa yanga ndio mnawasemea simba, malengo ya simba yalikuwa ni kuvuka robo fainali either cafcl au cafcc ili hilo jina la mwakarobo life na walishasema kuwa msimu huu wanajenga timu bado hawana timu ya kubeba kombe lolote la caf, huko kwingine walipofika ndio wakatamani wabebe kombe kama ambavyo timu yoyote ingetamani ila si kwamba ndio yalikuwa malengo yao toka mwanzo, yanga msimu huu ndio mlikuwa na malengo ya kucheza fainali cafcl na mkadai kwamba msimu huu hakuna timu ya kuwasumbua africa labda mcheze na malaika haya je mmetimiza hayo malengo yenu, ninyi siku zote malengo yenu ni kuwafunga simba na kufikia rekodi za simba hili hata msemaji wenu aliwahi kudhihirisha kwa kusema walikuwa wanaumia kuona wamezidiwa kwenye caf ranking na simba hivyo msimu huu wanaenda kufyeka hicho kichaka matokeo yake mlipoishia makundi ghafla fyekeo likawa butu
Mental health illness is actually existing, hili povu si ungeagiza makontena ya nguo hata buku ya badarini ufulie kwa mashine Watu wanukie sop sop?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mental health illness is actually existing, hili povu si ungeagiza makontena ya nguo hata buku ya badarini ufulie kwa mashine Watu wanukie sop sop?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Ukiniquote uhakikishe unajIbu hoja zangu usiniletee taarab
 
Mimi mwanzo nilitamani mamelodi washinde sababu nilidhani pyramids wakishinda, watatushusha simba kwenye caf ranking ila baada ya kujua kwamba hata pyramids wakishinda, hawawezi kutushusha kwenye hiyo nafasi yetu basi sina wasiwasi yeyote ashinde tu
kuwa nafasi ya tano huwa mnalipwa shi ngapi wenzetu?
 
Sasa berkane aliyekuwa na makombe mawili ya cafcc na hili la tatu unataka kumfananisha na yule usm alger ambaye hakuwahi kuchukua cafcc na ndio akalichukulia kwenu kwa mara ya kwanza, huko cafcl simba hata wawe wabovu kiasi gani hawajaishia hatua ya makundi mfano msimu uliopita tulishuhudia simba mbovu ambayo karibu kila shabiki aliikatia tamaa, lakini waliishia robo fainali sawa na yanga tu waliokuwa wanatupigia kelele kuwa wana kikosi bora na msimu huu ulipoanza pia mlidai mna kikosi bora na kipana, na mtafika fainali huko cafcl maana hakuna timu ya kuwafunga labda mcheze na malaika cha ajabu pamoja na kupangwa kwenye kundi jepesi lililojaa vibonde ambalo hata ninyi wenyewe mlifurahia kupangwa, lakini bado mmeishia makundi ilihali simba waliosema wanajenga timu huku wakianza msimu na wachezaji wapya zaidi ya nusu ila wamefika fainali ambayo ninyi mlifika mkiwa na kikosi bora na striker akiwa mayele
kwamba ulikufa kiume kufungwa na berkane?
 
Sasa mbona hujajibu hoja zangu matokeo yake unanilisha maneno, yanga ana kipi cha kumzidi simba mbona unajitoa ufahamu au na ninyi mnalo hilo kombe, nimekuambia hapa tunalinganisha simba na yanga wewe unaniletea habari za pyramids hivi umeelewa hata mada
Sioni kitu ambacho Simba kamzidi Yanga hakuna hakuna labdah uchawi tu
 
Motsepe kampa Kanu business card inaonekana anataka Kumtumia kuijenga zaidi Mamelody
Mayele alikuwa tz mamelody walikuwa na nafasi ya kumchukua ila wakakomaa na shalulile
Azizi kaenda wydad wao bado wanakomaa na viungo nyatunyatu acha Pyramid achukue
 
Motsepe kampa Kanu business card inaonekana anataka Kumtumia kuijenga zaidi Mamelody
Mayele alikuwa tz mamelody walikuwa na nafasi ya kumchukua ila wakakomaa na shalulile
Azizi kaenda wydad wao bado wanakomaa na viungo nyatunyatu acha Pyramid achukue

Kanu ndie bosi wa enyimba.

Timu yake ya nyumbani kwao anayoiongoza yeye imefeli, anaanzaje kuijenga mamelodi
 
Kanu ndie bosi wa enyimba.

Timu yake ya nyumbani kwao anayoiongoza yeye imefeli, anaanzaje kuijenga mamelodi
Unaweza kupata ushauri mzuri hata kwa Alie fail maana ana experience
Kumbuka Kanu kacheza arsenal na ulaya kwa ujumla ana uzoefu wa masuala ya mpira
 
Sasa kama mnajua timu haihukumiwi kwa historical records pekee kwanini yanga mkiona simba wamewazidi mahali mnakimbilia kuleta habari za makombe mengi ya ligi kuliko simba, haya tuzungumzie current form kwa msimu huu yanga mmewazidi nini simba tukija kwenye ligi ya ndani mnaongoza kwa tofauti ya point moja, ambapo hadi sasa bado hamna uhakika wa kuchukua ubingwa na kwa asilimia kubwa mechi ya derby ndio itaamua nani awe bingwa, tukija kimataifa simba wako kwenye nafasi ya tano kwenye caf ranking ilihali yanga wako nafasi ya kumi na moja simba wamefika fainali cafcc na wamepoteza mbele ya berkane, ambaye msimu huu ni bingwa wa ligi ya morocco ambayo ni ligi ya pili kwa ubora africa na pia berkane ni mzoefu wa hiyo michuano na ana makombe mawili ya cafcc, ila yanga ameshindwa kuvuka kundi rahisi mbele ya mc alger na al hilal ambao siyo wazoefu wa hiyo michuano na ndio maana wote wameishia robo fainali, sasa hebu niambie huo ubora wa yanga kwa simba uko wapi hasa kiujumla au ninyi mnaangalia majina ya wachezaji na mbwembwe zao uwanjani

Mkuu kwanza elewa katika mpira mafanikio ya kwanza ni kupata taji na ndio lengo la kila shabiki kufurahia kuona timu yake inakusanya taji kwavile mafanikio ya kipesa hayawezi kugaiwa kwa kila shabiki.

Mpaka sasa Yanga anagombea mataji mawili kati ya mataji matatu aliyoshiriki ( CAFCL, ligi kuu na CRDB FA) wakati Simba ikiwa inagombea taji moja tu kati ya mataji matatu aliyokuwa anashiriki. Siwezi kusema kugombea taji ni lazima uchukue lakini tayari Simba kabakisha shindano moja tu ambalo akilikosa anakuwa kamaliza msimu patupu kwa mara nyingine tena.

Kwenye mashindano ya klabu bingwa uzoefu haufanyi kazi bali ni ubora, mbinu sahihi dhidi ya mpinzani ndio hufanya kazi. Simba ilitolewa hatua ya robo fainali na timu ya Kaizer Chief ambayo hawakuwa na mwendelezo wa kushiriki mashindano ya CAF kwa muda mrefu sana tofauti na Simba ambao mara kwa mara wameshiriki mashindano ya CAF. Alkadharika Belouizdad pamoja na uzoefu wao wa kucheza robo fainali mara kwa mara ila wanashindwa kufuzu robo fainali kwa kutolewa na Yanga katika makundi hivyo achana na mambo ya uzoefu bali deal na current form kama navyokusisitiza mara kwa mara, mpira ni current form sio mambo ya uzoefu.

Umeongelea upande wa mashindano ya kimataifa twende in terms of numbers:

Mara ya kwanza Simba kuanza kufanya vizuri mashindano ya CAF ilikuwa ni msimu wa mwaka 2018/2019 ambapo ndio walianza kuwa na muendelezo wa kuingia mara kwa mara katika mashindano ya CAF.
Kutoka msimu wa 2018/ 2019 hadi msimu huu wa 2024/2025 Simba wamevuna point 48 katika misimu 7 ambapo ndani ya misimu 7 misimu 5 imefanyika performance ranking hivyo anapata wastani wa poont 9.6 kwa kila msimu

wakati Yanga wameanza kuingia katika kufanya vizuri CAF msimu wa 2022/2023 na kufanya muendelezo kwa misimu mitatu mfululizo na kupata point 34 zilizopatikana kwa performance ya misimu mitatu hivyo Yanga anakuwa na wastani wa point 11.333 kwa msimu. Kwa maana nyingine ni kwamba Yanga imepitwa na Simba lakini wanakuja kwa kasi katika kupata point za CAF na kuwa na wastani mzuri kama wataendelea kuwa na muendelezo.
 
Marumo alikua ameshuka daraja
Mashindano ya CAF na ligi ni mashindano mawili tofauti mkuu, ligi ni marathon hivyo lazima uvimbe haswa.

Kwenye CAF:
Hatua ya kwanza ni mechi 2
Hatua ya pili mechi 2
Makundi mechi 6
Robo fainali mechi 2
Nusu fainali mechi 2

Kutoka hatua ya kwanza hadi kuingia fainali kuna michezo 14 katika michezo 14 michizo 8 ni ya mfumo wa mtoano ina maana kwenye mashindano ya CAF ni ujanja wa mbinu sahihi ya kuzichanga karata ipasavyo tofauti na ligi kuu ambapo mechi hazipungui 30 ni mbio ndefu haswa yenye milima na mabonde mpaka kuweza kustahimili na ndio maana sio ajabu kumuona Constantine kipindi anacheza mechi ya kwanza dhidi ya Simba alikuwa anaongoza ligi ya Algeria lakini leo hii kamaliza nafasi ya 9 wakati kwenye CAFCC kacheza hadi nusu fainali.
 
Back
Top Bottom