Full Time: Pyramids FC 2 - 1 Mamelodi Sundowns FC | CAFCL Final | 2nd Leg | 30 June Stadium | 01-06-2025 (Ag 3 -2) Pyramids Mabingwa

Si tulikua tunazungumzia "current form"
 
Sasa kwa kuzingatia hiyo hoja yako ya current form yanga wamewazidi nini simba maana ni kama umeandika kitu sawa na kile kile nilichoandika mimi ila ukanicrush, kama ni makombe ya caf wote hawana kama ni medali za caf wote wanazo kama ni makombe ya ndani yote wote wameshabeba sasa kilichobaki ambacho yanga wanaweza kusema wamewazidi simba ni nini, maana simba wao wamewazidi yanga kwenye hizo caf ranking ambazo huwezi kuzibeza sababu kwa asilimia kubwa ndio zinaamua kwenye hatua ya makundi timu ipangwe pot namba ngapi na ipangwe na timu gani either na vibonde au timu ngumu hivyo naamini wote tunajua umuhimu wa hilo
 
Unajua mashabiki wa yanga mnashangaza sana yani wakati ninyi mnasema simba msimu huu kafika fainali cafcc kwa kucheza na timu dhaifu hamkufikiria yote haya, ila wengine wakisema hata yanga msimu ule walicheza na timu dhaifu kwa kutumia vigezo vile vile mlivyovitumia ninyi kuzipima timu zilizocheza na simba ndio mnakumbuka haya, sasa kwa kutumia hoja yako hiyo hiyo tuambie udhaifu wa timu zilizocheza na simba msimu huu na ubora wa timu zilizocheza na yanga msimu ule ikiwa yote haya mnayajua
 
Sasa kwa kuzingatia hiyo hoja yako ya current form yanga wamewazidi nini simba maana ni kama umeandika kitu sawa na kile kile nilichoandika mimi ila ukanicrush
Siwezi kusema kuwa Yanga kamzidi nini mpaka msimu uishe, msimu ukiisha ndio unapiga hesabu kuwa msimu huu timu imekusanya mataji mangapi kati ya mangapi. Mpaka sasa Yanga inawania mataji mawili ambalo ni ligi kuu na FA endapo Yanga itabeba makombe haya yote mawili basi tutaaema kuwa Yanga kamzidi Simba katika mataji. Endapo watagawana basi watakuwa na idadi sawa ya mataji kwa msimu huu. Na endapo Yanga atakosa Yote basi tutaaema Simba kamzidi Yanga katika mataji msimu huu.

Au wewe current form unaipigia ya misimu mingapi nyuma? Tuanzie hapo kwanza
 
Deal na mimi na wala usichukue maneno ya mashabiki wengine wa Yanga ukaja kunilisha maneno ambayo sijayatamka. Watu wanaona timu ni dhaifu ni wale wanaokalili majina makubwa ya timu ndizo bora pasipo kuangalia mabadiliko ya ubora wa timu ama wengine wanachanganya matokeo ya mashindano mawili tofauti yaani wanalinganisha timu X ikiwa katika ligi kuu ipoje pasipo kuzingatia ni vipimo viwili tofauti na inayohitaji approach mbili tofauti. Sijatoa hoja ya kusema timu alizokutana na Simba kuwa ni dhaifu mfate aliyetoa hoja hiyo ndio mkaelekezane nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…