Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Ushauri wa bure...
Inahitaji central defender mwenye kasi...
Hamza ni mzuri but slow.....
Che MALONE anahitaji patner anaweza kufanya correction anapotekeza...
 
Leo ndio leo kwenye kipute hiki cha Kombe la Shirikisho Africa kati ya wenyeji Simba ya Tanzania na wageni Sfaxien ya Tunisia.

Hii ni Match Day 3 kwa timu hizi na mechi zilizopita wote walichezea kichapo ugenini (2-1 na 3-2). Leo kila mmoja anatafuta ushindi kufufua matumaini ya hatua ya makundi.

Mechi hii itapigwa saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nini kitatokea katika Dimba la Benjamin Mkapa leo? Kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa mchezo huu kupitia JamiiForums.

Azam na DStv pia watarusha mechi hii.
View attachment 3177038

---------------------------------------------
Updates : 1500 Hours Vikosi vya leo
View attachment 3177287View attachment 3177288
________________________________________________

1' Mpira umeanza kwa Simba kuanzisha mpira hapa... wanashambulia lango la Sfaxien lakini Zimbwe anapiga pasi kuuubwa inaenda nje

2' Goooaaaal Sfaxien wanapata goal hapa kupitia Hazem Hassen

06' Simba wanashambulia hapa Kibu Denis anaangushwa... Freekick inapigwa na Jean Ahoua.. Kibu anafungaaaaa goal 1-1

09' Simba wametulia wanafanya shambulizi la Kushtukiza lakini Sfaxien wanaokoa shambulizi hilo

14' Simba wanamiliki mpira kwa Kiasi kikubwa kwa chenga za hapa na pale wanajaribu kuingia lakini mpira unatolewa nje

19' Musa Conte anamdondosha Awesu Awesu na Simba anapata freekick, Jean Ahoua anapiga ndefu ila kipa wa Sfaxien, Dahmen anaidaka

24' Kapombe anapress kuelekea Sfaxien anampasia Ateba lakini control yake inakuwa sio nzuri anadhibitiwa na mabeki wa Sfaxien matokeo bado ni 1-1


29' Kapombe anachezewa faulo hapa inakuwa ni freekick nje kidogo ya 18.. Kibu anapiga inagonga ukuta, Zimbwe anaiwahi lakini anapiga inatoka nje
Wawakilishi wa Taifa
 
Dakika ya 32

SSC 1
CSS 1

Ateba anakosa goal la wazi kabisa baada ya mlinzi kujichanganya hapa...daaah
 
Laiti FOWADI simba ingekuwa inaingia kwenye box kwa kasi + pressure+ numbers ....wangefunga nyingi
 
Back
Top Bottom