Full Time: Simba SC 3 - 0 Al Merrikh

As vita akifikisha points 10 na yeye atakuwa amemfunga simba. Sasa itategemea amemfunga simba magoli mangapi.
 
Sawa mkuu.
Kwa mfano Vita akishinda mechi zake zilizobakia na Simba afungwe zote,apo watalingana point kati ya Simba na Vita,je nani atapita apo?
Anapita Vita kwa sababu anamagoli mengi zaidi ya simba wakilingana pointi 10 na ninaona uko mbele simba akijitahidi kati ya mechi zake hizo mbili ashinde moja na kufungwa moja atapita ila naona mwendo huu wa simba huko mbele anamaliza nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikishikwa na wamisri. Hebu tusubiri tuone bado mechi hizi ni bado ni mapema wote watatu wana nafasi ya kufuzu yaani simba, Al ahly, na As Vita tusubiri tuone yajao yanafuraisha kama tukiwa makini na mechi yetu hii ya nyumbani zidi ya As vita tunatakiwa tushinde na sio sare ili tuwe na pointi 13 ili twende laundi ya pili, kila la heri Simba Mungu awe pamoja nawe.
 
Hatua ya makundi hakuna goli la ugenini, magoli ya ugenini yanakuwa kwenye mechi za mtoano
 
Kimahesabu Simba ni kama ameshapita robo. Hebu tumuangalie vita. Mechi ya kwanza kafungwa 1-0 na Simba.Halafu VITA akamfunga Merrekh 4-1. Hapo vita anaondoka na goal difference ya 2, Mechi ya Al Ahly na VITA ilikuwa 2-2, VITA anabaki 2 ile ile.Leo kakubali kichapo cha 3-0, Ana deni la -1. Simba anayo magoli +5 mkononi. Kwenye mpira lolote linaweza kutokea lkn nafasi ya VITA ni ndogo sana.....! Pia tukumbuke pengo la S.S.C ni kuwa wa kwanza kwenye kundi...! H2H VITA na Simba Congo Vita kapigwa home..
 
Magoli mengi ya vita umeyatoa wapi? Simba ana gd +5 vita ana -1. Uwezekano wa Vita kumzidi simba magoli ni kwenye mechi zilizobaki.
 
Tatizo ni huyo kibonde el merreikh anaweza akapigwa 6 kule congo. Tukifungwa 1-0 na vita halafu al ahly akatufunga 2-0 tunabaki na gd +2 ambazo vita anaweza kufunga zaidi dhidi ya el merreikh. Simba kufuzu ni draw au win dhidi ya vita na si kutegemea gd.
 
Hapa pamenifikirisha, Sasa AS VITA alipigwa kwao na Simba....ndo kusema AS VITA akifurukuta saaana ataishia point 10 ambazo Simba Sasa anazo. H2H VITA alipigwa na Simba tena nyumbani...! Kwa hiyo Kwa Simba njia Nyeupee....
Yaani njia peke ya As Vita kupata matumaini ya kufuzu ni kumfunga Simba kwa zaidi ya goli moja hata ikiwa ushindi kwa tofauti ya goli moja (2 kwa moja, au goli tatu kwa mbili, n.k)
 
Vitu vya sheria havitaki maono na mtizamo Bali vinataka fact/sheria/Kanuni zinasemaje.Wanaanza kuangalia kwanza Head 2 Head, matokeo yenu nyinyi wawili mechi zote 2, ikitokea mko sawa, mfano Simba kashinda Congo 1, na Vita kashinda Dar 1 bila hapo wanakuja kigezo number 2 ambacho ndio Goal Difference, ikitokea GD bado mpo sawa vinakuja vigezo vingine mpaka number saba, nachelea kuviandika kwa kuchanganya nilisoma katika gazeti, kigezo cha mwisho number nane inachezeshwa droo kati yenu atakayeshinda ndio anaendelea
 
As Vita Akishinda dhidi ya Simba goli mbili kwa moja. Inatosha kumfanya afuzu hata akishinda kagoli kamoja tu dhidi ya Al Merreikh, endapo Simba watashindwa kupata point Misri
 
Hizi hesabu zako zote zitakufa pale Vita akimfunga El Mereik, na akamfunga Simba goli zinaizidi Simba kwa 2, kisha Simba akafungwa na Al Ahly.

Yaani Vita akilingana Points na Simba wataangali H2H ambapo tuseme Vita akulishinda 2-0 atakua na aggregate ya H2H ya 2-1 so atapita yeye.
 
Hapa pamenifikirisha, Sasa AS VITA alipigwa kwao na Simba....ndo kusema AS VITA akifurukuta saaana ataishia point 10 ambazo Simba Sasa anazo. H2H VITA alipigwa na Simba tena nyumbani...! Kwa hiyo Kwa Simba njia Nyeupee....
Unajichanganya,

Unaposema As Vita akifurukuta sana ataishia points 10 basi lazima atakua amemfunga na Simba, sasa vipi tena useme H2H uifikirie ile moja tu ya Kinshasa aliyoshinda Simba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…