Full Time: Simba SC 3 - 0 Al Merrikh

Ni kweli japo si rahisi vita kuifunga simba kwa zaidi ya goli moja! Halafu inaelekea El Merreikh watu wameidharau Sana! Lakini ukweli ni kuwa hawa Wasudan watapata point moja nyingine, aidha toka kwa vita au toka kwa Al Ahly. Kwa hiyo simba ishafuzu!!
 
Hatuwezi tukakosa sare kwa Mkapa, wale watapigwa fitina kama zote
Ila ni kweli,Simba sasa sio ya kushindwa kula nyama laini laini kama hizi.
Kama aliliwa kwao anashindwaje kuvua chupi akiwa geto la Simba?
 
Ahsante kwa kutoa somo hapa.
Kumbe bado kazi ipo kwa hizi timu 3,Simba,Al Ahly na Vita.
Kwakweli kwenye soka mambo yanabadilika ngoja tusubiri kwanza,mambk bado.
 
Mimisri hawezi kuongoza. Ataharibiwa na Wasudan! Halafu hana ubavu wa kufunga simba!
 
Head to head inaangaliwa baada ya kulingana point na kulingana goal difference. Yaani ili Vita itabidi simba ufungwe jumla ya mabao yasiyopungua 8 katika mechi mbili zilizobaki na simba asifunge hata goli moja kwenye mechi zilizobaki.
Hapana wanaangalia H2H kwanza kabla ya goal difference endapo mtalingana point. Endapo watakuwa sawa sawa kwenye H2H ndio wanaenda kwenye goal difference
 
Halafu cha ajabu watu wameshakanusha kuwa Al Ahly ataifunga Simba! Si rahisi kivile! Hiyo mechi Ahyl atacheza kwa pressure kali mno!! Matokeo yake atafunguka Sana na hapo ndipo atakapolizwa ka mtoto mdogo! Uwezekano mkubwa wa hiyo mechi ni sare!!
Pamoja na kuwa Ahyl atakuwa nyumbani lakini bado naona ataiheshimu Sana simba kuliko mnavyodhani!! Anachogombania ni nafasi ya pili tu!
 
Goal difference wataangalia endapo H2H watalingana. Mfano Simba akipoteza kwa As Vita magoli mawili kwa moja hapo matokeo yatambeba As Vita kwasababu kwenye H2H Simba ameruhusu magoli mengi ya ugenini. Hivyo itaifanya mechi ya mwisho dhidi ya Al Al Ahly, Simba akatafute sare kwa udi na uvumba ama ushindi. Huku As Vita ata akishinda goli moja tu dhidi ya Al Merreikh, anakuwa kafuzu endapo Simba atafungwa Misri.
 
Mimisri hawezi kuongoza. Ataharibiwa na Wasudan! Halafu hana ubavu wa kufunga simba!
Mechi ngumu kwa Al Ahly ilikuwa ya jana kule Congo.

Hao Wasudani hawawezi kumzuia Mwarabu.. hata Simba tunaenda kula kipigo Misri.
 
Al Ahly hawatocheza kwa pressure kali mno endapo mechi inayofuata dhidi ya Al Merreikh watashinda. Maana wakishinda hiyo mechi watakuwa na point 10. Hivyo picha kamili ya kundi hili litapatikana kwenye mechi inayofuata ya Simba vs As Vita na Al Merreikh vs Al Ahly. As Vita akitoa sare au kufungwa atakuwa wameaga mashindano. Huku Al Ahly akimfunga Al Merreikh, mechi ya mwisho ya Al Ahly vs Simba itakuwa ni vita ya kumkwepa Mamelodi (kuongoza kundi)
 
... mechi yetu hii ya nyumbani zidi ya As vita tunatakiwa tushinde na sio sare ili tuwe na pointi 13
Tunahitaji sare tu, sio lazima kushinda. Zingatieni kanuni za mashindano haya, tusiishi kwa kukariri. Kanuni za mashindano haya ya CAF Champions League 2020/2021 zinasema timu zikilingana point, kinachofuata kuangaliwa ni points baina ya timu zilizolingana, yaani Head to Head, na zikilingana tena ndio zinafuata criteria nyingine. Simba na Vita zikilingana point 11, Simba inasonga bila kuangalia magoli ya Vita, hatakama watafikisha 15, maana tutakuwa na points 4 dhidi ya kwao 1 kwa kuangalia timu hizi mbili tu
 
Mechi ambayo Simba hawezi kupoteza kirahisi niya VITA CLUB...
lakini ya Misri toa akilini mwako kama tutapata point kule.
 
Umeandika pumba. Uongo
 
Leo mchana nilikuwa nafanya kikao nikaambiwa mpaka kufika mapumziko ni mbili bila,
Niliumia na kukasirishwa sana nikawaza leo lazima wewe jamaa uniletee mbwembwe,
Wangeruhusu kuingia uwanja wa taifa ningevaa kanzu nishabikie waarabu aisee...
Hahahahah mkuu THIS IS SIMBA

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…