Full Time: Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024

Full Time: Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024

Yaani huu Upumbavu unaboa Kabisa
Yaani nchi imekuwa Ya watu wa Hovyo sana kila jambo wao ni Fursa
Na Tukifungwa Walivyo wapuuzi kimyaa

Na fursa yenyewe Ya umimi.
Inaligawa Taifa
 
Its match day!!

Ni Tanzania Vs Guinea katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia Saa 10:00 Jioni.

Ni mchezo wa kufuzu AFCON ya mwaka 2025 pale Morocco ambapo kundi H Taifa Stars inahitaji ushindi wa namna yoyote ili ifuzu wakati Guinea wao wakihitaji ushindi au droo ili waweze kufuzu.

Saa 10:00 jioni kupitia Azam Sports 1HD, DStv pia kupitia Chaneli 225.

Mliopo Dar muende kwa wingi uwanjani, Kiingilio Bure.

Live updates zitakujia hapa..

Mpira umeanza ikiwa dakika 3

Dakika, 5 Taifa Stars wametengeneza nafasi nzuri sana hapa

Dakika, 10 Taifa stars wamendelea kutengeneza mashambulizi mengi bado kupata goli tu!

Dakika, 11 Saimon Msuva anakosa goli la wazi kabisa!

Dakika, 16 Stars wanafanya shambulizi kali sana ila Mussa Camara anadaka mpira huo!

Dakika, 20 Bado milango yote ni migumu kwa timu zote mbili.

Dakika, 35 si Stars wa Guinea ambaye amepata goli hadi sasa.

Dakika, 40 Guinea wanakosa kutumia nafasi ya wazi kufunga goli.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika Taifa Stars 0 - 0 Guinea
Ni afadhali timu ya Tanganyika wafunge goli jioni wataweza kulilinda kuliko kufunga mchana.....itakuwa ngumu kulinda goli hilo.

Mungu ibariki Tanganyika, Mungu wabariki wachezaji wa Tanganyika. Amina..
 
Yaani huu Upumbavu unaboa Kabisa
Yaani nchi imekuwa Ya watu wa Hovyo sana kila jambo wao ni Fursa
Na Tukifungwa Walivyo wapuuzi kimyaa

Na fursa yenyewe Ya umimi.
Inaligawa Taifa
Kunywa sumu ili uondokane na hiyo kero.
 
Kwakipi Alicho kifanya
Kama Tukishinda Mnamsifia na kwann Tukifungwa Mnakuwa kimya kumpa Lawama huyo Mungu wenu
Samia ndio kaleta Afcon

Samia ndio amekuwa anawpa ndege kusafiri Taifa stars

Samia ndio amekuwa anawatia moto sio tuu Taifa stars Bali Timu zote zinazoshieiki mashindano Kimataifa.

Samia amekuwa akiwapa pesa walifanya vizuri

Wewe umefanya kipi Hadi tukudigie badala ya Samia?
 
Back
Top Bottom