FULL TIME: Yanga SC 1-0 Simba SC | Semi-Final | Community Shield | Benjamin Mkapa Stadium | 08/08/2024

FULL TIME: Yanga SC 1-0 Simba SC | Semi-Final | Community Shield | Benjamin Mkapa Stadium | 08/08/2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1723061788399.png

Ngao ya Jamii: Alhamis hii ni nusu fainali ya wababe. Saa 1:00 usiku ni Kariakoo Derby Yanga SC dhidi ya Simba SC ngoma itapigwa dimba la Benjamin Mkapa.

Dakika 2, Mpira umeanza kwa kasi sana.

Dakika 4, Yanga wamekosa nafasi ya wazi baada ya Prince Dube kupiga mpira ukagonga nguzo ya goli.

Dakika 6, Steve Mkwala anakosa nafasi ya wazi kuweka mpira kimiani.

Dakika 11, Yanga wanatengeneza nafasi nzuri ila wameshindwa kuitumia vyema.

Dakika 17, Timu zote zinacheza kwa tahadhari sana kila mmoja anafanya mashambulizi ya kushutukiza.

Dakika 22, Simba wameendelea kumiliki mpira

Dakika 24, Simba wamepata faulo ila wanashindwa kuitumia vyema.

Dakika 26, Max Mpia anakosa nafasi nzuri kabisa.

Dakika 30, Simba wamekuwa wa moto sana wakiendelea kupima watu umri.

Dakika 32, Yanga wanapata faulo tuone kama watafanikiwa kuweka mpira wavuni.

Dakika 33, Yanga wanakosa faulo waliyoipiga.

Dakika 36, Yanga wamekuwa watulivu sana wanaendelea kutengeneza nafasi.

Dakika 37, Aucho anapata kadi ya njano baada ya kumfanyia mazambi Steve Mutala.

Dakika 41, Aziz ki anakosa nafasi ya wazi baada ya kupiga shuti zito na mpira ukapenda kutoka nje.

Dakika 43, Max Mpia anakosa nafasi nzuri baada ya kupewa pasi nzuri na Aziz Ki

Dakika 44, gooooooool Max anawapa goli hapa Yanga gooooooool

DAkika 45, Yanga 1-Simba0

Dakika 45 za Kipindi cha Kwanza zimetamatika Yanga SC 1- Simba SC 0

Kipindi cha pili kimeanza na Yanga wanafanya mabadiliko ya anaingia Mzize anatoka Prince Dube.

Simba Pia wanafanya mabadiliko anatoka Mzamiru anaingia Oka Jefa.

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi sana kwa timu zote mbili.

Dakika 44, Simba wamepata kona 3 dotto zote wamekosa kuzitumia vyema.

Dakika 59, Bado shughuli nzito Yanga wanaendelea kuongeza goli la pili nao Simba wanapambana kurudisha.

Dakika 66, Mudathiri anachukua nafasi ya Duke Abuya.

Dakika 70, Mukala anatoka anaingia Kibu Densi na anaingia Ngoma kuchukua nafasi ya Fernandes

Dakika 77, Kalubu anapata kadi ya chajo baada ya kumfanyia faulo Aziz Ki

Dakika 81, Chama anachukua nafasi ya Aziz KI

Dakika 84, Pacome anapata kadi ya njano

Dakika 87, Pacome anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Musonda. Lakini pia Max Mpia natoka nafasi yake inachukuliwa na Bakari Nondo.

Dakika 4 zimeongezwa kumaliza mchezo huu.

Dakika 90 zinatamatika Yanga 1- Simba 0

Screenshot_20240808_164035_Instagram.jpg
Screenshot_20240808_164025_Instagram.jpg

 
Back
Top Bottom