Kwanza iweleweke kuwa mwanadamu ili awe kamili katika ulimwengu huu ni lazima awe na muunganiko wa vitu vitatu.
Cha kwanza ni Mwili
Cha pili ni Nafsi
Cha tatu ni Roho.
ROHO ni kiumbe kitakatifu, infact ndio kiini cha uhai kwa viumbe,Roho inatoka kwa Mungu. So kifo ni kitendo cha mwili na nafsi kutengana na Roho. Roho ndio huuwezesha mwili kufanya kazi, kunyanyuka,kutembea ,kukaa,kutenda na kila kitu....hili uwezekana tu pindi roho iwapo ikitoka mwili unakuwa hauna nguvu ya kutenda kila kiungo kinakuwa hakifanyi kazi.
NAFSI ni wewe, Mimi na Yule.....hii ndio nafsi , ndio wewe mwanaadamu ,Hii ina nafasi ya kufanya maamuzi either yawe mazuri au mabaya ikishirikiana na akili pamoja na mwili. Infact nafsi ndio controller imepewa uwezo wa kutawala kila kifaa cha utendaji katika mwili wa mwanaadamu kwa muda maalumu...as long as Roho bado haijaondolewa kutoka katika mwili. Roho ikiwepo tu katika mwili....ni sawa na Umeme unapokuwepo katika computer...yaani hapa computer inakuwa ON...ila computer hii haiwezi kufanya kazi bila ya kuwa na program...sasa hiyo program ndio Nafsi....inaamua sasa computer ifanye kitu gani. Nafsi italipwa kutokana na mema au mabaya iliyoyafanya katika kuuongoza huu mwili hapa ulimwenguni.
Mwili ni jumba la nje lililoifunika NAFSI.Hili jumba lipo ni mifupa iliyovikwa nyama kikapatikana kiwiliwili then ndani yake ikawekwa NAFSI na ROHO kumuunda mwanadamu aliyekamilika kabisa