Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Kabla hujazaliwa hujawa sehemu yoyote iweje ukifa uende sehemu?

Hizo propaganda za after life ni kujifariji tu ukifa na Hadith Yako inaishia hapo kama ilivyo kwa viumbe wengine!
 
Kabla hujazaliwa hujawa sehemu yoyote iweje ukifa uende sehemu?

Hizo propaganda za after life ni kujifariji tu ukifa na Hadith Yako inaishia hapo kama ilivyo kwa viumbe wengine!
Sawa mkuu,subiri utajionea mwenyewe....yaani binadamu ulivyo na thamani hivyo umeletwa Duniani utawale kila kitu halafu eti ukifa iwe basi?...
 
Mimi nadhani kila mtu ashike lile analo amini kulingana na mapokeo na makuzi ya mtu husika, kama kwenye dini, kwenye sayansi, au utamaduni .

Mimi naamini hapa duniani sio kwetu bali kuna mahali ndipo uwenyeji wetu ulipo, na hapa duniani tunapita na marejeo ni kwa yule aliwezesha kuwa hapa, na sifa zote njema apewe yeye(MUNGU)
 
Sawa mkuu,subiri utajionea mwenyewe....yaani binadamu ulivyo na thamani hivyo umeletwa Duniani utawale kila kitu halafu eti ukifa iwe basi?...
Aliekudanganya kwamba binadamu ana thamani ni nani?
Kipi kinakufanya ujione special kuliko viumbe Wengine?
Au kuvaa nguo na kua na utashi ndio unaona ndio una thamani sana Kuliko viumbe hao,
Bila shaka Bado hujaijua kanuni ya Maisha wewe Kila kiumbe kinasurvive Kwa destiny yake hata sisi hiyo ndio destiny yetu nje ya Hapo ni hekaya za kujifariji!
 
Hakuna mtu anayekufa, miili yetu ndio inakufa miili yetu ina 'expire' lakini sisi hatu 'expire' kwasababu sisi ni nuru tunatoka katika mwili na ukitoka katika mwili unaendelea ku exist hivyo mwili ukifa ww unaendelea kuwepo kama ulivyokuwa kabla hujavaa mwili.

Watu hawafi, wakati wa msiba ni wakati maalum sisi kujifunza kwa miili yetu kwamba mwili wako ni wa mauti ni wa finite na mtu yeyote aliyeondoka katika mwili ana touch na roho anakosa touch na mwili, anaweza kukupapasa na wewe usihisi inategemea wewe una ukaribu na nini, ukiwa karibu sana na mwili hautam-feel lakini ukiwa karibu na roho utam-feel na utamuona.


KAMA HUJIELEWI, HUWEZI KUNIELEWA
 
Nadhani hakuna malaika Israel Bali ni kati ya Gabriel na Raphael
Israel ni jina la makosa....Israel ni jina na nabii Yaqoub ibn Ishaq ( Jacob mtoto wa Isaka) ...Jina la malaika anaehusika na kazi ya kutoa roho viumbe anaitwa MALAKUL MAUT kwa jina jepesi anaitwa ( Malaika wa kifo / Angel of death) .
 
Quran 56:47-50

And they used to say, "When we die and become dust and bones, are we indeed to be resurrected?

And our forefathers [as well]?"

Say, [O Muhammad], "Indeed, the former and the later peoples

Are to be gathered together for the appointment of a known Day
 
Kwa mujibu wa kitabu kitukufu cha Quran ...inaeleza kuwa huko zamani wstu walikuwa wakihoji kama mtoa mada anavyohoji kumuuliza Mtume wa Mungu....kuwa je tutakapokufa na miili yetu kusagika na kubaki mifupa, je tutafufuliwa upya? Na vp kuhusu na mababa na mababu zetu nao waliokwisha kufa nao watafufuliwa...jibu walilopewa ni simple tu kuwa wooooote tutafufuliwa.Kama Mungu aliweza kumuumba mwanaadamu out of nothing mpk akamleta ulimwenguni, je ni vipi ashindwe kumfufua na kumrejesha ktk umbile lake la kwanza?
 
Ni sawa na mtu atengeneze sanamu la udongo kisha aamue alibomoe liwe mchanga...je unadhani atashindwa tena kuurudisha udongo na kuwa sanamu?
 
Mnaotaka kujua masuala ya maisha ya mwanadamu yalikuwaje kabla ya kuja duniani, baada ya kuja duniani, wakati wa kufa na maisha baada ya kifo basi nawashauri msome kitabu cha Quran. Hata kama sio muislam jiwekee utaratibu wa kusoma vitabu ...kila kitu katika ulimwengu huu kimewekwa kwenye kitabu. .ila ni kuwa watu hatuna muda au hatutaki kusoma vitabu.
 
Inawezekana we tulishakuzika lakini we hujui na unaendelea KUPYATILA ( kuandika kwa kutumia smartphone). Hakika hili ni fumbo!
 
Kwanza iweleweke kuwa mwanadamu ili awe kamili katika ulimwengu huu ni lazima awe na muunganiko wa vitu vitatu.

Cha kwanza ni Mwili

Cha pili ni Nafsi

Cha tatu ni Roho.

ROHO ni kiumbe kitakatifu, infact ndio kiini cha uhai kwa viumbe,Roho inatoka kwa Mungu. So kifo ni kitendo cha mwili na nafsi kutengana na Roho. Roho ndio huuwezesha mwili kufanya kazi, kunyanyuka,kutembea ,kukaa,kutenda na kila kitu....hili uwezekana tu pindi roho iwapo ikitoka mwili unakuwa hauna nguvu ya kutenda kila kiungo kinakuwa hakifanyi kazi.

NAFSI ni wewe, Mimi na Yule.....hii ndio nafsi , ndio wewe mwanaadamu ,Hii ina nafasi ya kufanya maamuzi either yawe mazuri au mabaya ikishirikiana na akili pamoja na mwili. Infact nafsi ndio controller imepewa uwezo wa kutawala kila kifaa cha utendaji katika mwili wa mwanaadamu kwa muda maalumu...as long as Roho bado haijaondolewa kutoka katika mwili. Roho ikiwepo tu katika mwili....ni sawa na Umeme unapokuwepo katika computer...yaani hapa computer inakuwa ON...ila computer hii haiwezi kufanya kazi bila ya kuwa na program...sasa hiyo program ndio Nafsi....inaamua sasa computer ifanye kitu gani. Nafsi italipwa kutokana na mema au mabaya iliyoyafanya katika kuuongoza huu mwili hapa ulimwenguni.

Mwili ni jumba la nje lililoifunika NAFSI.Hili jumba lipo ni mifupa iliyovikwa nyama kikapatikana kiwiliwili then ndani yake ikawekwa NAFSI na ROHO kumuunda mwanadamu aliyekamilika kabisa
 
Ifahamike kuwa kabla ya kukabidhiwa hii miili duniani....tulikwishaumbwa sote kabla..Yaani mwanadamu yupo katika mfumo wa nafsi ila nafsi hizi huletwa duniani kwa awamu ....ili nafsi moja ije duniani ni lazima kuwa kuja muunganiko wa nafsi mbili, nafsi ya Me na Ke...zikikutana hizi zinatengeneza nafasi ya nafsi nyingine kuja duniani.

Nafsi ikija duniani inapewa mwili na roho ili iwe na nguvu ya kiutendaji kutenda mema au maovu katika muda mahususi
 
Katika safari ya Nafsi kuna vituo...kituo cha kwanza ni kwa Mungu....then kituo cha pili ni hapa ulimwenguni kwanza kwenye tumbo la mama na kisha baada ya kuzaliwa,kituo cha Tatu ni Kaburini, kituo cha nne ni Siku ya ufufuo na kituo cha mwisho ambacho ni cha tano ni maisha ya milele PEPONI au MOTONI. Huko tena hakuna kufa ni either upate RAHA ZA MILELE au upate TABU NA SHIDA ZA MILELE.
 
3. Akifa basi amekufa kama ilivyo kwa viumbe wengine, kwamba hakuna kinachoendelea?
Aliyekuambia Mbwa, paka, fisi, vyura wakifa hakuna kinachoendelea ni nani?

Wanyama wana hisia, wanacommunicate, wana vita n.k

Binadamu tunaumia, tunacommumocate, tuna vita n.k

Utofauti wetu ni nn? Au sababu ya akili ya kujenga nyumba na roketi na ndege?

Usiniambie wanyama hawana nafsi, how do we know that?
 
Baada ya Roho kutenganishwa, hupelekwa juu kuhifadhiwa sehemu takatifu...na nafsi inabaki chini na mwili, hapa nafsi inauwezo wa kusikia kila kitu kinachoendelea ulimwenguni ila haina uwezo wa kutenda kuutumikisha mwili tena. So inakwenda kuhifadhiwa katika kituo kinachofuata ambacho ni kaburini!

Huko mwili unaachana na nafsi, mwili unarudi katika asili yake ya udongo na Nafsi inabaki vilevile katika uhalisia, ikiendelea kuhojiwa kwa yale iliyokuwa ikiyatenda hapa ulimwenguni huku ikisubiri muda wa ulimwengu uishe ili siku ya mwisho ifufuliwe kuelekea katika vituo vinavyofuata.

So Maisha ya Nafsi huwa hayana mwisho toka ilipoumbwa huwa inabadilishiwa tu mazingira ila nafsi ya mwanadamu huwa ni ya milele inabadilishiwa tu hali ya kuvikwa mwili au kuvuliwa mwili.
 
Kama hujui unakoenda lazima uogope,lakini km anajua huwezi kuogopa!
Heaven is real
Hell is real!
Chaguo ni lako, kumbuka uwe na dini ama huna njia ni moja tu nayo ni Yesu!
Yesu alisema "mimi ndie njia ya kweli na ya uzima mtu haji kwa baba bila ya mimi"...
 
Maisha ya duniani tunayoishi ni mafupi mno kulinganisha na maisha tuliyoyaishi baada ya nafsi zetu kuumbwa huko juu mbinguni na baada ya kufa kuishi huko chini ardhini na baadae katika ulimwengu wa milele ambao huo hauna mwisho
 
Back
Top Bottom