Fundisho la Utatu haliingii akilini kabisa, mnaoamini mmetoa wapi mbona Biblia iko wazi kabisa?

Fundisho la Utatu haliingii akilini kabisa, mnaoamini mmetoa wapi mbona Biblia iko wazi kabisa?

Najibu swali la kwanza
Yohana 17 : 3

Jibu ni philiipe 2:5 - 11

ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Kwa andiko hilo lina tuzibitishia yule alikuwa Mungu ndani ya mwili wa wanadamu

Hiyo ni kawaida ya Mungu anaweza kujibadirisha chochote na anacho kipenda
Kwa hiyo kwa yesu alikuja mwenyewe akaona kuliko kujiita Mungu ni bora niwe kama mwanadamu mwenzao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na unaposema nini maana ya yohana 17..3 nenda soma mpaka msitari wa 5 anaposema sasa unitukuze mimi pamoja nawe kwa utukufu ule niliokuwa nao kabla ya ulimwengu kuwako,,, lbda kama hujui maana ya ulimwengu ni dunia sayar zote mbalamwez zote vacuum zote living and non living things before any living and non living thing the 3 coexsting powers were there🙄🙄🤒
Lakini yote yakiegemea katika KUSADIKI, hapa ndipo Kiranga anapotolea changamoto. Na huwa tunataka kulazimisha kuthibitisha kwa namna ambayo ni nje ya KUAMINI na KUSADIKI😆.
 
Ni ukweli unaoumiza kukiri kuwa dini hizi za asili ya Abraham zinashindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu, suala la maisha kabla na baada ya kufariki, isipokuwa tunaegemea katika IMANI, KUSADIKI na UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO.
Binafsi nimesikiliza kwa kiasi cha kutosha viongozi wa dini hizi, na wengineo kama monks, na latest kabisa ambae nimekuwa nikimsikiliza ni SADHGURU.
Pia nimejaribu kuskiliza mara kadhaa wanaokataa suala la MUNGU. Issue kubwa na ya uhakika ni kuwa HAWAJUI.
Na nimetokea kuliheshimu neno SIJUI likiwa katika UAMINIFU WAKE.
Jesus: "Baba wasamehe kwa kuwa HAWAJUI walitendalo".
Sadhguru on God: "the honest answer is I DONT KNOW (if he exists) but there is a source of creation,you can call God"
Most of meditation practice: You can become God when you are initiated and know the truth(enlightment).
 
Kwa framework ya logic.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye kaumba ulimwengu huu, hayupo.

Hayupo kwa sababu maelezo ya kuwepo kwake yanajipinga yenyewe, yana logical inconsistency na contradiction.

Ndiyo maana haiwezekani kuthibitisha yupo, huwezi kuthibitisha kitu ambacho hakipo kuwa kipo kwa logical consistency.

Ndiyo maana wanaosema yupo, wanaishia kuongelea upande wa imani tu. Imani unaweza kuamini cochote, hata cha uongo.

Kwenye kuthibitisha hawawezi.
 
Lakini yote yakiegemea katika KUSADIKI, hapa ndipo Kiranga anapotolea changamoto. Na huwa tunataka kulazimisha kuthibitisha kwa namna ambayo ni nje ya KUAMINI na KUSADIKI😆.
hatyongelei sayans mzee tunaongelea imani ( imani ni kuwa na uhakika wa mambi yatarajiwayo na ni bayana ya mambi yasioonekana)
 
JEHOVAH ni MUNGU Baba na sio Yesu (MUNGU Mwana).
MUNGU alimwambia Musa amwite JEHOVAH . Na Musa hakuwahi kuiona sura ya MUNGU , kwa hiyo huyo ndiye MUNGU Baba - haonekani
Mungu Alimwambia Musa amwite Niko ambae Niko
 
Shenzi type . We sio Mkristo
Upo ki-ubishani na sio kutaka kulewa usipo paelewa
Mi naina kama wewe ndio shenzi maana jamaa amekujibu vzr ,dhehebu linahusianaje hapo
 
Hoja yako ilikuwa kwamba, ukikijadili tu kitu, hilo linathibitisha kuwa kipo kweli.

Kwa sababu, kama hakipo kweli, usingeweza kukijadili.

Hivyo, kumjadili Mungu tu kunathibitisha kwamba yupo kweli.

Nimekuonesha kwamba tunaweza kumjadili James Bond 007, jasusi wa Kiingereza, ambaye ni character wa hadithi na sinema, hayupo nje ya hadithi na sinema.

Hivyo, hoja yako kwamba kitu ukiweza kukijadili tu huo ni uthibitisho kwamba kipo kiukweli, nje ya ulimwengu wa fikra na hadithi tu, imeonekana kuwa ni potofu na haina mashiko.

Jaribu hoja nyingine.

Ukisema Mungu yupo kihistoria na si kihaithi, toa uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Unaelewa kwamba historia inatenganishwa na hadithi tupu kwa uthibitisho right?

Thibitisha Mungu yupo, acha longolongo.
Elewa kwamba James bond hawezi kutoka nje ya hadithi na sinema zake. Tunapomjadili ni lazima akae ndani kwanza. Akiwa nje, hata hadithi na sinema zake havitakuwapo.

Tafadhali tusitiane ujinga.

Mara kadhaa nimesema kuwa kuna mambo mengine hayana mfumo wa kuthibitisha uwepo wake ingawa yapo. Uwepo wake ndiyo uthibitisho wake pekee. Nilitoa na mifano lakini unajitoa ufahamu na kujifanya huelewi.

Natoa mfano tena:
Kuna msemo usemao; "kila lenye mwanzo, halikosi mwisho". Uhai wako upo mwilini mwako, una mwanzo na mwisho wake. Je unaweza thibitisha mwanzo na mwisho wa uhai wako? Je, usipothibitisha ina maana wewe sio hai na huishi? Tafakari kwa makini.

Mungu yupo, usijitoe ufahamu.
 
Uumbaji ni uumbaji huo huo unaoufahamu na unathibitisha kwamba haukujiumba mwenyewe
Mimi kutojiumba mwenyewe si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Kama vile wewe kutojizaa mwenyewe si uthibitisho kwamba baba yako ni Donald Trump.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Elewa kwamba James bond hawezi kutoka nje ya hadithi na sinema zake. Tunapomjadili ni lazima akae ndani kwanza. Akiwa nje, hata hadithi na sinema zake havitakuwapo.

Tafadhali tusitiane ujinga.

Mara kadhaa nimesema kuwa kuna mambo mengine hayana mfumo wa kuthibitisha uwepo wake ingawa yapo. Uwepo wake ndiyo uthibitisho wake pekee. Nilitoa na mifano lakini unajitoa ufahamu na kujifanya huelewi.

Natoa mfano tena:
Kuna msemo usemao; "kila lenye mwanzo, halikosi mwisho". Uhai wako upo mwilini mwako, una mwanzo na mwisho wake. Je unaweza thibitisha mwanzo na mwisho wa uhai wako? Je, usipothibitisha ina maana wewe sio hai na huishi? Tafakari kwa makini.

Mungu yupo, usijitoe ufahamu.
Hebu achana na habari za Mungu kwa dakika chache, tujadili mantiki ya hoja tu.

Umekubali kwamba, kitu kuweza kujadiliwa si uthibitisho kwamba kipo katika uhalisia nje ya ulimwengu wa fikra na hadithi tu?

Kwa sababu tumeona tunaweza kumjadili James Bond 007, character wa hadithi na sinema tu, ambaye kiuhalisia hayupo?

Nataka tumalize na kukubaliana kuhusu hii hoja potofu kwamba kitu ukiweza kukijadili ni lazima kiwepo, kisingekuwepo usingeweza kukijadili.

Tujue kwamba hata characters wa hadithi, waliobuniwa kifikra tu na ambao hawapo nje ya hadithi tunaweza kuwajadili.
 
hatyongelei sayans mzee tunaongelea imani ( imani ni kuwa na uhakika wa mambi yatarajiwayo na ni bayana ya mambi yasioonekana)
Imani unaweza na unaruhusiwa kuamini hata uongo.

Kwa hivyo haina uzito wa kitu kinachoweza kutenganisha ukweli na uongo.

Swali ni je, katika facts, katika mantiku, unachoamini ni kweli? Au ni ujinga tu umejazwa?
 
Hebu achana na habari za Mungu kwa dakika chache, tujadili mantiki ya hoja tu.

Umekubali kwamba, kitu kuweza kujadiliwa si uthibitisho kwamba kipo katika uhalisia nje ya ulimwengu wa fikra na hadithi tu?

Kwa sababu tumeona tunaweza kumjadili James Bond 007, character wa hadithi na sinema tu, ambaye kiuhalisia hayupo?

Nataka tumalize na kukubaliana kuhusu hii hoja potofu kwamba kitu ukiweza kukijadili ni lazima kiwepo, kisingekuwepo usingeweza kukijadili.

Tujue kwamba hata characters wa hadithi, waliobuniwa kifikra tu na ambao hawapo nje ya hadithi tunaweza kuwajadili.
James Bond akijadiliwa kwa dhana ya hadithi, yupo, huyu hapo. Uwezi kujadlii jambo ambalo halipo katika dhana husika. James Bond huyo huyo akijadiliwa ktk dhana ya historia, hayupo kabisa. Elewa, hadithi na historia ni vitu viwili tofauti kabisa.

Sisi hapa tunamjadili Mungu ktk dhana ya historia. Ni kwa sababu vitabu vilivyoandika juu ya uwepo wa Mungu ni vya historia, sio vya hadithi.

Jambo la kihistoria lina uhalisia wake, na hatuwezi kukubaliana kizembe kwamba Mungu hayupo.

Mungu yupo, tuache kiburi dhidi yake.
 
Kwa hivyo umekubali tunaweza kujadili kitu ambacho kipo katika hadithi tu?
 
Hakuna mtu mwenye majibu sahihi ya kukuaminisha , biblia pia haina majibu sahihi , cha msingi we mwabudu Mungu , kama we ni mkristo umeelekezwa ukiomba Kwa Mungu omba kupitia jina la Yesu , ukiona Una uhitaji wa Mungu kukusaidia jua huo ni ushawishi wa roho mtakatifu , fuata maelekezo , lakini kuanza kubishana sjui utatu mtakatifu , mara Yesu ni Mungu wala sio Mungu , utaishia kuwa confused...hakuna mwenye majibu sahihi labda Mungu mwenyewe ambaye Hana hata mpango wa kukuaminisha , yeye anasubiri Tu ufate maelekezo basi
Majibu sahihi yapo. Biblia ina majibu sahihi. Ukitafuta kwa bidii utayapata.

MUNGU hana nafsi tatu bali MUNGU kama MUNGU ni ROHO na ROHO hizo ziko SABA.

Kuna MUNGU BABA ambaye ni ROHO kwa asili (hana mwili wala umbo) na kuna MUNGU MWANA (KRISTO) ambaye naye hapo mwanzo alikuwa ROHO (NENO) lakini baadaye, alifanyika mwili na kuzaliwa kama mwanadamu na kuwa na UMBO la kibinadamu.

ROHO TAKATIFU siyo nafsi ya MUNGU bali ni nguvu au uweza wa MUNGU anaowapa wale wote wanaomtii kwa kuzishika Amri zake na imani ya KRISTO.

Yeyote anayejazwa au kupewa nguvu hii au uweza huu (ROHO TAKATIFU) humbadilisha mtu huyo no kumfanya kuwa mwana wa MUNGU.

Roho Takatifu ni kama umeme ndani ya bulb. Bila nguvu ya umeme bulb haiwezi kuwaka. Roho Takatifu humfanya mtu kuwa kama MUNGU yaani mtu mwenye Roho Takatifu ataishi milele, hata kama akifa, atafufuliwa na kuishi tena milele na milele.

YESU KRISTO naye alikuwa na ROHO TAKATIFU , uweza wa KIMUNGU wa kutenda kama MUNGU na kuishi kama MUNGU.

Hivyo basi ROHO TAKATIFU siyo nafsi ya tatu ya MUNGU. Hayo yote niliyokuandikia hapo juu yanapatikana ndani ya BIBLIA. Someni nanyi mtafahamu.
 
Sipendi na sina uvumilivu wa kujadili jambo ambalo halina uhalisia.
Hata huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote unayesema yupo hana uhalisia.

Ndiyo maana ukiambiwa uthibitishe yupo huwezi.

Unaishia kutapatapa na hoja mufilisi tu. Hoja ambazo tukiziweka katika darubini kali zinaonekana kukosa mashiko.

Habari ya kuwapo huyo Mungu haina tofauti na habari yavm kuwapo James Bond 007.

Wote wawili, Mungu na James Bond 007, ni characters katika hadithi za kutungwa na watu.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Zamani mkuu wa kanisa Katoliki akisema kitu hata kama ni uwongo inabidi ukubali. Hivyo tukubali tu huo utatu kwa kuwa unaungwa mkono na kanisa. Ila mwenye akili ahoji, ila yasikupate yaliyompata Nicolaus corpenicas alipopindua meza na kusema Dunia ndiyo inayolizunguka jua.
 
Hata huyo Mungu mjuzi wa yite, mwenye uwezo wote na upendo wote unayesema yupo hana uhalisia.

Ndiyo maana ukiambiwa uthibitishe yupo huwezi.

Habari ya kuwapo huyo Mungu haina tofauti na habari yavm kuwapo James Bond 007.

Wote wawili, Mungu na James Bond 007, ni characters katika hadithi za kutungwa na watu.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
Je nitakuwa sahihi nikisema wewe haupo duniani na sio hai kwa kuwa hajathitisha chanzo cha uhai wako?
 
Back
Top Bottom