Fundisho la Utatu haliingii akilini kabisa, mnaoamini mmetoa wapi mbona Biblia iko wazi kabisa?

Rudi kwenye hoja yetu tafadhali. "Mungu yupo na hana chanzo".
 
Kwa hivyo umekubali vitabu vitakatifu havina hoja?
Rudi kwenye hoja, usijitoe ufahamu tafadhali.

Utakatifu wa vitabu ni uzi mwingine, ukipenda anzisha tujadili.

Mungu yupo na hana chanzo.
 
Biblia inamwita Roho Mtakatifu wewe unaita Roho Takatifu! Unatumia Biblia ya wapi? Dah; Shetani is so powerful.
Una mengi sana ya kujifunza ili uelewe kuwa kilichowachanganya wengi ni Lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya na tafsiri kutoka Lugha hiyo kwenda lugha zingine.

Lugha iliyotumiwa kuandika original manuscript za Agano Jipya ni Kiyunani (Kigiriki). Lugha ya Kigiriki inatumia gender pronouns na nouns hata kwenye vitu. Ndiyo maana waliotafsiri waliandika Roho Mtakatifu badala ya Roho Takatifu.
 
... kwamba wewe ni mtaalamu wa tafsiri kuliko waliotafsiri Biblia? Kwamba nina mengi ya kujifunza kwamba sio Roho Mtakatifu bali Roho Takatifu? Ha ha ha! Be serious Mkuu.

Hakika nimeamini Shetani ni baba wa uongo na upotoshaji. Biblia nzima Roho Mtakatifu anawakilishwa kwa kiwakilishi nafsi kiambata "a" badala ya "i" sijui unatuletea stori za wapi Chief?
 
Rudi kwenye hoja, usijitoe ufahamu tafadhali.

Utakatifu wa vitabu ni uzi mwingine, ukipenda anzisha tujadili.

Mungu yupo na hana chanzo.
Kama utakatifu wa vitabu ni hoja ya uzi mwingine, kwa nini umeileta hoja hiyo katika uzi huu?

Mimi sijaileta hoja hiyo hapa, wewe umeileta.

Hoja umeleta wewe mwenyewe, unaona nakubana, unaikana kuwa si ya uzi huu sasa?

Unakana na kusema vitabu vitakatifu havina hoja?

Siondoki hapo mpaka nipate jibu.
 
Kwa ufahamu wako unafikiri waliotafsiri Biblia walikuwa sahihi kwa asilimia 100%?
Mimi ni MKRISTO tena ni MKRISTO kweli kweli (sijisifu la hasha), lakini nimeutafuta UKWELI na nimejua kuna makosa mengi tu ya "tafsiri" ndani ya Biblia.
Fanya utafiti wako mdogo utaona hilo. Hata hao wanaojiita "theologians" wanalifahamu hilo kwa hakika.

ROHO TAKATIFU au ROHO MTAKATIFU siyo nafsi ya tatu ya MUNGU BABA, bali ni uwezo wa MUNGU BABA au nyenzo ya MUNGU BABA anayowapatia "wateule wake" ili waweze kutenda kazi alizowakusudia kuzitenda. Tena, uwezo huo au nyenzo hiyo ya MUNGU BABA ndiyo inayowafanya wateule hao kufanyika "watoto wa MUNGU". Hakuna mwanadamu atakayeingia kwenye UFALME WA MUNGU bila ya kuwa na ROHO TAKATIFU ndani yake.

ROHO TAKATIFU ndiyo ROHO YA MUNGU na pia ndiyo ROHO YA KRISTO.

Ikiwa MUNGU BABA ni "ROHO", iweje basi awe na nafsi nyingine ya tatu ambayo ni ROHO MTAKATIFU???

BWANA YESU KRISTO alisema hivi :
"mimi na BABA yangu tu wamoja" (YOHANA 10:30).
Kama Roho Mtakatifu angekuwa nafsi ya tatu ya MUNGU basi YESU KRISTO angesema, mimi, roho mtakatifu, na BABA yangu tu wamoja.

Tena YESU KRISTO akasema;

Yohana 14:10​

"Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi".

Hapa napo tunaona BWANA YESU KRISTO hamtaji ROHO TAKATIFU, bali anaonesha dhahiri kuwa kuna wawili tu, yaani MUNGU BABA na MUNGU MWANA.

Pia soma YOHANA 1:1-14.
 
YOHANA 1

Neno akawa mwili

1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.

6 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. 8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. 9Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
 
Umebanwa mpaka Unatafuta pa kutorokea.
Utakatifu wa vitabu haukuwa mkondo wa mjadala wetu kuhusu uwepo wa Mungu. Ni sawa na wewe ulipoleta hadithi za James Bond 007, lakini hatukubadili mkondo wa hoja yetu ya uwepo wa Mungu au la. Umejitoa ufahamu kabisa kwa kujaribu kunitia gizani katika mwanga. Sio rahisi katika hili.

Hata hivyo kama unataka tujadili hoja juu ya vitabu vitakatifu, niko tayari. Karibu.

Mungu yupo na hana chanzo.
 
Kuna swali la James Bond 007 umeniuliza nikashindwa kujibu?

Hoja ya vitabu vitakatifu umeileta mwenyewe, jibu maswali yanayoihusu.

Hoja ya vitabu kuwa vitakatifu umeikataa? Huamini katika vitabu vitakatifu tena?
 
... asante kwa ufafanuzi japo umezingatia zaidi itikadi za kimadhehebu kuliko Biblia yenyewe kuhusu Roho Mtakatifu vs Roho Takatifu. Kama imefahamika kwamba waliotafsiri Biblia wamekosea kuhusiana na hilo, kwanini marekebisho yasifanywe ili iendane na tafsiri sahihi; at least dhehebu lenu mtoke na toleo sahihi?

1. Yohana 14:16-17; "Nami nitamwomba Baba naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele ndiye roho wa kweli ...."; ==> Nami (mimi/Yesu), Baba, msaidizi mwingine. Wanatajwa wangapi hapo? (Yesu, Baba, na Roho Mtakatifu).

3. Matendo ya Mitume 5:3, 4 "Petro akasema, Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya dhamani ya kiwanja kilipokuwa kwako hakikuwa mali yako na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, dhamani yake haikuwa katika uwezo wako? ili kuwaje hata ukaweka neno hilo mwonyoni mwako? hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.";

Kama kumwambia uongo Roho Mtakatifu ni kumwambia uongo Mungu utasemaje Roho Mtakatifu sio Mungu?
 
Kuna swali la James Bond 007 umeniuliza nikashindwa kujibu?

Hoja ya vitabu vitakatifu umeileta mwenyewe, jibu maswali yanayoihusu.

Hoja ya vitabu kuwa vitakatifu umeikataa? Huamini katika vitabu vitakatifu tena?
Sikuuliza swali kwani ningekuwa nimekengeuka mkondo wa hoja yetu. Siulizi maswali kizembe.

Vitabu vitakatifu haikuwa hoja, ila unalazimisha iwe hoja. Niko tayari kujibu hoja zako kama utauliza tena ukiona bodo zinatija kijamii.

Sivikatai vitabu vitakatifu kwani hivyo ndiyo msingi wa imani yetu.
 
Vitabu gani hivyo, vitaje tuviangalie tuone kama msingi wa imani yako ni sahihi au si sahihi.
 
Vitabu gani hivyo, vitaje tuviangalie tuone kama msingi wa imani yako ni sahihi au si sahihi.
Biblia Takatifu na Kuran Takatifu ndiyo vitabu ninavyovifahamu kwa majina. Kati ya hivyo, nafahamu mengi ktk Biblia Takatifu.
 
Biblia Takatifu na Kuran Takatifu ndiyo vitabu ninavyovifahamu kwa majina. Kati ya hivyo, nafahamu mengi ktk Biblia Takatifu.
Biblia na Quran vyote vimejaa contradictions.

Hivyo si vitakatifu.

Unaelewa hilo?
 
Huo unyenyekevu unamfanyia nani?
 
Umeandika vitu vinavyosomeka!
 
Mwanzo 1:26-28 BHN
Kisha Mungu akasema, “TUMFANYE mtu kwa mfano wake......" Mimi sio mtu wa kusali sana ila najaribu kuwaza, Mungu alikua na nani alivyokua akihusisha uwingi ktk uumbaji wake na hata mambo mengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…