... kwamba wewe ni mtaalamu wa tafsiri kuliko waliotafsiri Biblia? Kwamba nina mengi ya kujifunza kwamba sio Roho Mtakatifu bali Roho Takatifu? Ha ha ha! Be serious Mkuu.
Hakika nimeamini Shetani ni baba wa uongo na upotoshaji. Biblia nzima Roho Mtakatifu anawakilishwa kwa kiwakilishi nafsi kiambata "a" badala ya "i" sijui unatuletea stori za wapi Chief?
Kwa ufahamu wako unafikiri waliotafsiri Biblia walikuwa sahihi kwa asilimia 100%?
Mimi ni MKRISTO tena ni MKRISTO kweli kweli (sijisifu la hasha), lakini nimeutafuta UKWELI na nimejua kuna makosa mengi tu ya "tafsiri" ndani ya Biblia.
Fanya utafiti wako mdogo utaona hilo. Hata hao wanaojiita "theologians" wanalifahamu hilo kwa hakika.
ROHO TAKATIFU au ROHO MTAKATIFU siyo nafsi ya tatu ya MUNGU BABA, bali ni uwezo wa MUNGU BABA au nyenzo ya MUNGU BABA anayowapatia "wateule wake" ili waweze kutenda kazi alizowakusudia kuzitenda. Tena, uwezo huo au nyenzo hiyo ya MUNGU BABA ndiyo inayowafanya wateule hao kufanyika "watoto wa MUNGU". Hakuna mwanadamu atakayeingia kwenye UFALME WA MUNGU bila ya kuwa na ROHO TAKATIFU ndani yake.
ROHO TAKATIFU ndiyo ROHO YA MUNGU na pia ndiyo ROHO YA KRISTO.
Ikiwa MUNGU BABA ni "ROHO", iweje basi awe na nafsi nyingine ya tatu ambayo ni ROHO MTAKATIFU???
BWANA YESU KRISTO alisema hivi :
"mimi na BABA yangu tu wamoja" (YOHANA 10:30).
Kama Roho Mtakatifu angekuwa nafsi ya tatu ya MUNGU basi YESU KRISTO angesema, mimi, roho mtakatifu, na BABA yangu tu wamoja.
Tena YESU KRISTO akasema;
Yohana 14:10
"Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi".
Hapa napo tunaona BWANA YESU KRISTO hamtaji ROHO TAKATIFU, bali anaonesha dhahiri kuwa kuna wawili tu, yaani MUNGU BABA na MUNGU MWANA.
Pia soma YOHANA 1:1-14.