Mmeme
JF-Expert Member
- Nov 25, 2017
- 700
- 298
Tayari nimekujibu post # 209. Kitu asilia hakina chanzo, na wewe unajua hivyo.Unaelewa nikikuuliza kuwa chanzo ni kitu cha lazima au si kitu cha lazima, ukijibu kwamba chanzo ni kitu cha lazima kwa vingine vyote, ukimuondoa Mungu, ambaye hana mwanzo, ulichojibu hapo kimsingi ni kusema kwamba chanzo si kitu cha lazima?
Yani ni kama nimekuuliza, wilaya ya Ilala inapatikana katika nchi ya Tanzania au haipatikani katika nchi ya Tanzania?
Halafu unanijibu kwamba, ukiutoa mkoa wa Dar es salaam, ulio nchini Tanzania, ambao una wilaya ya Ilala, wilaya ya Ilala haipatikani Tanzania.
Kwa nini unataka kuuondoa mkoa wa Dar es salaam wakati swali langu halijauliza uuondoe mkoa wa Dar es salaam?
Kwa nini unasema "licha ya Mungu" wakati swali langu halikuuliza "licha ya Mungu"?
Huo mfano wako ni wa kiporojo zaidi kuliko uhalisi. Hauna afya ya mjadala wetu. Rudi kwenye hoja ya uwepo wa Mungu au la.
Hoja yangu ilijengwa katika msingi wa "Licha ya Mungu" kwa kuwa natambua uwepo wa Mungu. Nisingefanya hivyo, ningekuwa nimeikubali kizembe hoja dhaifu. Hata hivyo, kwa nini unakerwa na hiyo sentensi?