Uchaguzi 2020 Furaha Dominic Jacob mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Kawe ni nani?

Uchaguzi 2020 Furaha Dominic Jacob mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Kawe ni nani?

Yani unaweza kujua furaha ni mmama flani[emoji16][emoji16][emoji16]majina mengine kwikwi
Furaha ni jina lenye bahati Sana. Kijana wa pacha wangu anaitwa furaha. Ni watu wenye mikakati, wakarimu, Wana nidhamu Wana upendo, hawashindwi kirahisi, wapole lakini Wana msimamo na hawaonewi kijinga. Furaha atambwaga Halima Mdee mapema Sana, mapema Sana.
 
Acha uongo sisi ndiyo wapigakura wa Kawe Mdee hatutaki hata kumsikia alivyotutenda hii miaka mitano hatuwezi msahau. Tangu tumchague hajawahi itisha mkutano wowote wa wananchi!!
Wewe unakaa kungoja mkutano wakati yeye anafuatilia mikwamo tunayokutana nayo hasa ya miundo mbinu. Hizo akili za kukaa kusubiri mikutano tuu ni za kindezi kabisa.
Yeye anapambana bungeni hadi Kawe tunaona fahari
 
Furaha ni jina lenye bahati Sana. Kijana wa pacha wangu anaitwa furaha. Ni watu wenye mikakati, wakarimu, Wana nidhamu Wana upendo, hawashindwi kirahisi, wapole lakini Wana msimamo na hawaonewi kijinga. Furaha atambwaga Halima Mdee mapema Sana, mapema Sana.
Sawa kwa box la kura atapigwa mapema mpka aitwe happy,ila kwa kutumia DC,NEC na policeccm ndio atamshinda halima
 
hata kama hatakatwa, na apite tu
je Wakazi wa Kawe watamuacha Halima Mdee wampe Ngosha?
hilo Jimbo bado sana CCM kulikomboa kutoka Chadema
tusubirie mgombea wa ACT
maana NCCR atakuwepo Mbatia
Kama ACT nao wanaweka mgombea,basi dogo anachukua kirahisi tu.
 
Mgombea wa ccm jimbo la kawe aliye shinda kura za maoni ni waziri.wa zamani wa ujenzi na mwaka 2015 alipeperusha bendera ya ccm , na kushinda kwa bao la mkono wa NEC.
 
hao wajumbe 100 waliompa usidhani ni sawa na wakazi wa Kawe watakaomchagua Halima Mdee au mgombea yoyote wa ACT
jua kwanza katokea wapi hata kura haombi

Walipiga hesabu ya wajumbe. Wajumbe 100+ wakasetiwa. Tena labda kuna wengine walisetiwa ila walighaili na kumpa kura zao Gwajima,Sitta ama Kizila.
 
Sasa Mbona Kawe inabaki njia panda?!

Halima kwa kweli watu wameshamchoka sana na huyo Furaha hatumjui !

Labda tusubiri tumpe nafasi ya kumsikiliza kwenye campaign lakini hapo ni kama mashaka fulani hivi.

Kwanini hawakumpitisha Gwajima chapakazi jamani !

Yani mmeacha wananchi kwenye sintofahamu kubwa!

Safari hii watu wanatarajia mabadiliko ya kumtoa Halima
 
Kawe si mchezo, tuone km Mjomba wako atakuwepo siku ya kuhesabu kura
hapo watakuacha mbali na hakuna rangi au nyota utakayoitambua
kosa kubwa sana wamefanya
tutakimbia na box la kura na polisi anatulinda mtafanya nini?
 
Scientific research zimathibitisha pasipo shaka kuwa mabadiliko hupelekea ufanisi always!

Kwanini Halima apewe vipindi zaidi ya viwili?

Viwili alivyopata vinatosha.

Kwanza hata yeye mwenyewe amechoka kiutendaji graph yake imeshuka sana!

Haonekanagi jimboni kwa wananchi kabisa mpaka wakati wa uchaguzi kama hivi, hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa wananchi wa majimbo mengine sawa lakini kwa Kawe haikubaliki.

Namuombea anko Magu siku hiyo aamke vizuri atuwekee mtu sahihi ili yafanyike mabadiliko Kawe!

Binafsi siamini katika kuendelea na mbunge kwa vipindi zaidi ya viwili.

Atoke kwanza aje arudi badae panapo majaliwa!
 
Back
Top Bottom