Uchaguzi 2020 Furaha Dominic Jacob mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Kawe ni nani?

Mimi nazani ishu isiwe kwamba hatumjui huyo Furaha Dominic,

Kwa hiyo inamaana tusiojulikana tusije kugombea?

La hasha!

Hoja ya msingi ni kuwa ataweza kuaminika na kushawishi wapigakura kuwa ana uwezo wa kuchapa kazi na kushirikiana na serikali katika kuondoa matatizo sugu ikiwemo migogoro ya ardhi katika kuwapatia watu haki zao?

Je ataweza kuwa karibu na wananchi katika kusikiliza kero zao na kushirikiana na serikali kuziondoa kwa wakati?

Je atakuwa na ushawishi na kukubalika huko serikalini katika kushirikiana kutatua matatizo na kero za wananchi?

Tuyatafakali hayo na mengineyo kabla ya kuamua kufanya uchaguzi .

Mimi nazani kama anko Magu atampisha huyu FUraha basi tumpe nafasi tumsikilize wakati wa campaign atasemaje?

Kisha tutamhoji tunaona majibu yake!
 
Hakuna kushinda kisa ni Kijana au Mzee!
Utashinda tu kwa mbinu zako,ushawishi na watu wanaokuzunguka wanataka nini..Over
 
Huyu dogo ametemgenexewa genge la vijana wa uvccm, ili ainekane kama stars mfano wa kina diamond.

Atakuwa kila akipita na msululi wa walinzi etc .


Wasukuma kipindi hiki.mna raha..[emoji1][emoji1][emoji1]
 
In short wajumbe wamehongwa bahasha zimetoka chamwino
 
Kura zitagesabiwa na police.. nimeota hakuta kua na uchaguzi kawe..
 
Naona hamna mtu anayemjua vizuri humu. Watu wanaongeaongea tu
Nilivyosikia kutoka kwa wadau ni kuwa huyu jamaa ni mtu wa kitengo halafu ana undugu kabisaaa na mheshimiwa sana.

..ila kwa confidence ile aliyokuwa nayo dogo si bure inaonyesha kabisa kulikuwa na nguvu kubwa nyuma yake, kwani hakujisumbua kabisa kuzungumza sana, alijitambulisha tu, na kisha kuwatakia kila la heri wajumbe wapiga kura..! Tofauti na wengine waliotoa mapovu na kupiga magoti kabisa lakini waliambulia kura 2...!
 
Shati lake limepaukaaaaaa....inaonekana kabisa choka mbayaaaa...kashindaje ati?
 
In short wajumbe wamehongwa bahasha zimetoka chamwino



Nasikia wote walopita kwa rushwa itakapothibishwa nasikia kutangazwa mgombea rasmi itategemea na Anko Magu atavyoamka!

Sasa itakapothibitika hayo yalifanyika anawezwa kuwekwa mshindi wa 2 au 3 hata 4

Kwa hiyo hata hapo itategemea na mwandamo wa mwezi!

Ni wazi kuwa Kawe kuna sintofahamu!
 
Kumbe. Sasa hiyo influence kwa wajumbe aliifanya lini ?Au kakulia Osterbay kwa Magufuli ?Mtoto wa dada yake yupi ?
Mkuu hii nchi ina mambo mengi usiyoyajua....
Hapo unaweza kuta maelekezo yalitoka juu kwamba dogo ni lazima ashinde!!
 
Inaonekana Furaha hajulikani kwa wana-kawe wengi ila anajulikana kwa wana-ccm Kawe.
Ili kuthibitisha ubora wa bidhaa, ifanyike litmus test ya jukwaani.
Furaha, Angela, Askofu Gwajima na wengine wawili wapelekwe Zenji kwenye utambulisho wa Hussein Mwinyi na kupewa dakika kadhaa kushawishi wazenji kumtambulisha Hussein; hapo wataweza kujua ipo mbivu ipi mbichi.

Kujinadi kwa mtindo aliotumia jana, hakuwezi kumthibitisha kama mwanasiasa mwenye ushawishi wa kumwangusha Mdee au uwezo wa kujenga hoja mjengoni ili kuitaka serikali itekeleze miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya Kawe.

Ila huenda wana-CCM Kawe wanajua nini wanataka
 
Umesikia wasukuma pekee ndio wanaosha nyota!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…