Uchaguzi 2020 Furaha Dominic Jacob mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Kawe ni nani?

Leo tumeshuhudia wagombea wasiopungua 175 wa kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM wakipigwa chini na mtu anayefahamika kwa majina ya Furaha Dominic.

Inavyoonekana huyo Furaha anajulikana na wajumbe wa CCM Kawe tu, sisi wananchi wa kawaida hatumjui kabisa. Huenda 99.9% ya member wa JF leo ndio tumesikia kwa mara ya kwanza hilo jina.

Kwa maoni yangu, sidhani kama huyo ni mtu sahihi wa kuja kupambana na Halima Mdee.

Haijarishi atateuliwa yeye, ama ngazi za juu za maamuzi ndani ya CCM zitamteua mtu tofauti na huyo aliyeshinda kidemokrasia ndani ya CCM, bado CCM itakuwa kwenye mtihani mgumu wa kumnadi mgombea wake.

Aliyeshinda kidemokrasia hafahamiki kijamii na ikiwa mtu mwingine tofauti atateuliwa naye atakuwa hakubaliki kidemokrasia ndani ya CCM.
 
Bora kakosa. Gwajboy angepata angeligawa kanisa la Bwana. We unadhani kwa siasa zetu za bongo jinsi wabunge wanavyowananga wenye itikadi tofauti nao, unadhani ni mwanachamaa gani wa upinzani angebaki muumini wake!!?? Angebaki na waccm wenzake tu!!!
Mama Rwakatale mbona hakuligawa kanisa lake?
 
Namba 5 hiyo!!!
 
Kijana Furaha anaonekana mdogo lakini yuko vizuri sana kichwani na mtulivu pia
Kama ni mtoto wa dada kweli ni sawa lakini bila akili na bidii binafsi hilo halitoshi kumfanya kuwa bora kama alivyo. Kila la heri kwake👍
 
Katika uchaguzi mkuu ni chama ambacho kinatafuta kura. Wengi wanaompinga ni Chadema kwa hofu ya Halima kuukosa ubunge. Angechaguliwa kippi au anjela hapo halima ungalikuwa mtelemko ila huyu, halima atafute f Iranga amfunze yale majambo kama alivyomfunza Wema. Cc Mzigua90
 
Kwani Halima alishinda vipi mara ya kwanza? Mbona hakujulikana? Mwanzo wa 10 ni 1, go figure, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…