Furahia upishi wako na gesi janja (M-GAS) yenye mita janja wala huhitaji kununua mtungi wa gesi tena

... mwanzoni nilidhani gesi ikiisha unalipia na kupata huduma kama ilivyo LUKU; kumbe hadi usubiri uletewe! Hilo ni tatizo na customer service za kibongo zilivyo za kindezi unapigia jitu ambalo ni wajibu wake litoe huduma halipokea simu au haipatikani kabisa.

Kwa bongo hii huduma za aina hii bado sana. Kwanini nikiishiwa gesi nisivuke tu mtaa wa pili nikabadili mtungi au nikamtuma boda chap! This is more reliable kuliko huo uzungu tunaojaribu kuuiga wakati tabia na desturi zetu bado sana.
Kwani wewe unaishi mtaa gani boss. Huduma zetu ni nzuri sana boss. Ukipata matatizo kama hayo tena wasiliana na mimi nikutatulie tatizo lako kwa wakati.
 
Hatakiwi kuhama na mtungi wake
Haitakiwi apitishe wiki 2 bila kununua gesi
Gesi yenu bei juu ya buku ni dk 0 tu, mtungi wenu ule mdogo mpaka unaisha anajikuta kaishalipia zaidi ya 40-50 elfu, wakat kampuni nyingine ni 22k.
Boss gesi zote gharama ni sawa tu na inategemeana na matumizi yako.
 
Wakenya kwa kukopesha tu hamjambo,ubaya wake ni kwamba huwa hizi huduma zenu zinaenda na zinapotea.

Mtaacha watu kwenye mataa hawatoamini macho yao,M-GAS nawakumbuka na M-KOPA yani mkianzaga tu mnaanzaga kwa speed ya kimbunga

sasa hivi humalizi dk 5 haijakatza pikipiki ya M-GAS nasikitika kimoyo moyo kwasababu nyie ni mabinga wa kuanzisha ila kuendeleza na kudumu katika mlichoanzisha ni jambo lingine kabisa.

Siharibu biashara yenu,najua wakati mnaifanya hii biashara hamtakua na kasoro ila shida yenu ni hamdumu ktk mlichoanzisha,mtawaacha raia kwenye mataa najua.

Biashara ya kukopesha Gas hamtoboi tena kwa Watanzania hawa hawa Hamtoboi hilo nina uhakika nalo.

Wateja mtawapata ila wateja wanaochakecha na kupembua vitu kabla ya kufanya maamuzi hao hamtowapata,Hivi Dar es Salaam yote ni mjini wakuu?

nilikua nataka washauri hawa ndugu zangu wajikite Daslamu vijijini kule wateja ni wengi kwasababu ya uhaba wa gas hata hizi za kawaida ila kwa walioko daslam mjini kwenye gas hadi za 13k kujaza,Kuwapata ni ntiti.
 
Mteja ataamua akope M-Gas au anunue kwa cash mtungi wa KG 3 kwa 35,000

ambao upo complete na gas yake yani akinunua ni anaenda kupika direct,mtungi huo

ambao ukimuishia ataujaza kwa 13,000 tu kisha ataendelea na matumizi yake kama kawaida.

Au anaweza nunua mtungi wa kg 6 kwa 38,000 (kampuni ya puma) atumie kwa amani na mustarehe bila madeni,ukimuishia ataujaza kwa 22,000, Maamuzi ni kichwani mwa mteja.

Msipende kukopa kopa hizi huduma asee,kopeni mapesa huko hawa watu wana mahesabu makali sana,hela yao ikirudi wanawaachia vumbi.
 
Wakenya kwa kukopesha tu hamjambo,ubaya wake ni kwamba huwa hizi huduma zenu zinaenda na zinapotea.

Mtaacha watu kwenye mataa hawatoamini macho yao,M-GAS nawakumbuka na M-KOPA yani mkianzaga tu mnaanzaga kwa speed ya kimbunga

sasa hivi humalizi dk 5 haijakatza pikipiki ya M-GAS nasikitika kimoyo moyo kwasababu nyie ni mabinga wa kuanzisha ila kuendeleza na kudumu katika mlichoanzisha ni jambo lingine kabisa.

Siharibu biashara yenu,najua wakati mnaifanya hii biashara hamtakua na kasoro ila shida yenu ni hamdumu ktk mlichoanzisha,mtawaacha raia kwenye mataa najua.

Biashara ya kukopesha Gas hamtoboi tena kwa Watanzania hawa hawa Hamtoboi hilo nina uhakika nalo.

Wateja mtawapata ila wateja wanaochakecha na kupembua vitu kabla ya kufanya maamuzi hao hamtowapata,Hivi Dar es Salaam yote ni mjini wakuu?

nilikua nataka washauri hawa ndugu zangu wajikite Daslamu vijijini kule wateja ni wengi kwasababu ya uhaba wa gas hata hizi za kawaida ila kwa walioko daslam mjini kwenye gas hadi za 13k kujaza,Kuwapata ni ntiti.
Kopa-Gas tutaendelea kuwepo siku zote boss usiwe na hofu. Karibu upate huduma yetu.
 
Ni siku ya 3 toka nijiunge illa sijapata huduma,naaambiwa kadi ime expire na ni mteja mpya,sasa hapa hela ya kulipia ninayo kwenye simu naenda kuitoa nikamuungishe Rostalam niendelee na maisha yangu.
 
Nimeikuta sehemu nikaitamani,bahati nzuri wakati natafuta namba zao,ndo nimekumbana na hizi comments. Kumbe 90% hawajalidhia huduma zao.
Meneja mwenyewe,maelezo yake hayajitoshelezi. Sehemu moja wanadai mtungi ni bure. Tena eti ulipie elfu 40. Tena badae unaambiwa kuna hela ya jiko. Na mbona kwenye maelezo haipo? Hio itakuwa kama ile ya TANESCO.
Kwa ufupi,ni janja janja siyo! Sasa anapodai kwambakutompelekea mtu gesi,inatokana na wingi wa wateja, hiyo inamhusu nini alieishiwa gas? Hili ndo sijapenda mie.
Kwa nini msiweke vituo sehemu mbali mbali,basi kwa anaeona kusubili hawezi,awe anafata mwenyewe? Na ya nini muwe waongo, mkimwambia asubiri siku 2 mnapungukiwa nini? Japo kwa sasa huduma ya gesi si ya kusubiri?
 
Kwa ushauri wangu, tumia utaratibu huu, eneo ulilopo nenda kwa wakala wa M-Gas umwuulize kwasababu kila mtaa huwa unakuwa na wakala wa M-Gas. Ukishindwa kutatuliwa tatizo lako ndio uende makao makuu.
 
Bei ya jiko uliyotaja huenda ikawa chanzo ndo Sh ngapi? Na hukatwa kwa mda gani?
 
Yaan najuta hawa jamaa wameniingiza choo cha kike na 40,000 yangu
 
Nimeacha kujaza mtungi wangu,nikpapatikia hawa jamaa leo siku ya 3 nipo njia panda na simu zao hazipatikani zote.

Mje mchukue mtungi wenu,maana nitakuwa nimenunua jiko tu
 
Ni bora uende ofisini kwa wakala wa M-Gas aliye kwenye mtaa wako huyo ndio utaratibu mzuri ambao utasaidia kumaliza tatizo lako.
Ninapokaa hakuna wakala,mbona namba zenu hazipatikani????huku yombo hakuna wakala,harafu yule alieleta mtungi mbona akipigiwa simu anasema yeye hausiki???
 
Back
Top Bottom