Fursa: Nafasi 700 za Kazi za Kuangalia Wazee New Zealand (Kupitia Danvast Career Search)
Habari wanajamii,
Nimekutana na tangazo la kazi ambalo naona linaweza kuwasaidia baadhi yetu humu. Kuna nafasi 700 za kazi za kuangalia wazee (Caregiver Jobs) katika nyumba za kulelea wazee New Zealand, kupitia tovuti ya Danvast Career Search.
Kazi hizi zinahusisha huduma kwa watu wazima na wazee, kwa wale waliopo kwenye mazingira ya nyumbani au vituo vya malezi.
Mahitaji yanayojitokeza ni pamoja na:
Umri wa miaka 21 na kuendelea
Uwezo wa mawasiliano kwa lugha ya Kiingereza
Uzoefu katika huduma za afya au malezi ni faida
Nidhamu, huruma na moyo wa kujitoa kwa huduma
Faida zinazotajwa:
Nafasi 700 zenye mazingira salama ya kazi
Mafunzo kwa waombaji wapya
Msaada wa kupata Visa upo, kupitia waajiri waliopo New Zealand
Naomba mwenye uzoefu au anayejua zaidi kuhusu hawa Danvast Career Search, atoe mrejesho ili kuelimishana. Pia kwa waliowahi kuomba kupitia huko, feedback yenu itasaidia sana.
Nawasilisha kwa nia ya kusaidiana.