Kwa umri wangu huu mdogo nimepata fursa ya kutembelea baadhi ya nchi hapa Afrika,ktk fursa hii nimebahatika kwenda nchi ya Morocco.
Nilienda morocco kupitia Mali kwa Tombouctou airport ya mali to Duarzazate airport ya morocco.
Nikiwa morocco nimetembelea majiji tofauti tofauti km unavyojua tunaojitafuta kila tulipo tunaangalia furasa, kati ya majiji niliotembea ni pamoja na Nador, Tetouan na Tangier(mji wa kibiashara sana,maana hapa watu utoka ulaya kuja kufanya biashara hapa).
Kuna fursa nimeliona morocco, kwa mtu mwenye connection na mtaji unaweza ukaifanya. Morocco biashara ya Mbuzi inalipa sana, kule wanapenda sana nyama choma hasa ya mbuzi, wazungu wanatoka Spain kuja kununua mbuzi Morocco. Mbuzi mwenye ubora mzuri anauzwa hadi laki tano(500,000/=)kwa ela ya kitanzania na wakati mwingine mbuzi zinakuwa hadimu bei upanda.
Kule warabu wana ela hawalili bei kiasi hicho,km anaitaji atachukua.lkn mbuzi wengi sana wanaenda ulaya,nimeona niwasanue kwa hili.