Fursa nchini Morocco: Biashara ya mbuzi inalipa sana

Fursa nchini Morocco: Biashara ya mbuzi inalipa sana

Kwa umri wangu huu mdogo nimepata fursa ya kutembelea baadhi ya nchi hapa Afrika,ktk fursa hii nimebahatika kwenda nchi ya Morocco.

Nilienda Morocco kupitia Mali kwa Tombouctou Airport ya Mali to Duarzazate airport ya morocco.
Nikiwa Morocco nimetembelea majiji tofauti tofauti km unavyojua tunaojitafuta kila tulipo tunaangalia furasa, kati ya majiji niliotembea ni pamoja na Nador, Tetouan na Tangier(mji wa kibiashara sana,maana hapa watu utoka ulaya kuja kufanya biashara hapa).

Kuna fursa nimeliona Morocco, kwa mtu mwenye connection na mtaji unaweza ukaifanya. Morocco biashara ya Mbuzi inalipa sana, kule wanapenda sana nyama choma hasa ya mbuzi, wazungu wanatoka Spain kuja kununua mbuzi Morocco. Mbuzi mwenye ubora mzuri anauzwa hadi laki tano(500,000/=)kwa ela ya kitanzania na wakati mwingine mbuzi zinakuwa hadimu bei upanda.

Kule Waarabu wana hela, hawalili bei kiasi hicho. Kama anahitaji atachukua. Lkn mbuzi wengi sana wanaenda ulaya, nimeona niwasanue kwa hili.
Mbuzi ni wengi sana west Africa na Sahel ambayo ni karibu na Morocco. Halafu Morocco ni wabaguzi sana kwa waafrika weusi hao mbuzi sidhani hata watakubali kuwauzia.
 
Hapo gharama ya kupeleka kiwandani kuchinja na packaging, uwe na vibali vyote vya usafi, export na mkemia
Hii sio fursa ya kuletwa JF
Kuna nchi nyingine zinafanya biashara hii, kwani wao wanafanyaje hadi wanaweza? Shida ya tanzania hakuna uhusiano rafiki kati ya serikali na wafanyabiashara hivyo hata vibali utapitia process nyingi si km nchi zingine
 
Mbuzi ni wengi sana west Africa na Sahel ambayo ni karibu na Morocco. Halafu Morocco ni wabaguzi sana kwa waafrika weusi hao mbuzi sidhani hata watakubali kuwauzia.

Hao waliokufanyia ubaguzi labda uliwaudhi , mbona mimi nimekaa nao miaka 5 sijaona ubaguzi wowote ?? Tena kuna wakati naumwa nilikuwa na rafiki yangu akisoma mwendo wa masaa mawili na nusu kwa train na alikuwa akija kuniangalia
 
Warabu wana ubaguzi ila sio kiasi hicho, ivi mtu anauitaji na kitu alaf unacho ashindwe kukinunua?

Ndio hapo , ubaguzi kila mahali upo hata kwa waafrika kwa waafrika . hawa wanapoenda nchi za watu huwa wanafikiria zinaa kwanza na kitu hicho wewe mweusi kwa mwarabu si rahisi hata kwa wazungu pia
 
Ndio hapo , ubaguzi kila mahali upo hata kwa waafrika kwa waafrika . hawa wanapoenda nchi za watu huwa wanafikiria zinaa kwanza na kitu hicho wewe mweusi kwa mwarabu si rahisi hata kwa wazungu pia
Mimi morocco nilikuwepo kwa shughuli nyingine ila nikaona hili nikaona niwaletee uzi, nenda zambia hapo wana ubaguzi kinoma aisee, nimekaa nao nimefanya nao kazi, wanabagua watu kuja
 
Hao waliokufanyia ubaguzi labda uliwaudhi , mbona mimi nimekaa nao miaka 5 sijaona ubaguzi wowote ?? Tena kuna wakati naumwa nilikuwa na rafiki yangu akisoma mwendo wa masaa mawili na nusu kwa train na alikuwa akija kuniangalia
Racism ipo mkuu. Hasa Marrakesh wanajiona ni wa Spain
 
Kuna Taarifa kwamba hao jamaa ni wabaguzi sana haswa kwa weusi, hiyo hali uliiona? Unaizungumziaje..

Hebu weka wazi ili anayeifuata hii fursa ya mbuzi ajiandae kisaikolojia.
Mkuu sisi watanzania ndo tunajifanyaga wema kwa watu kuja kuliko wazawa ila nchi nyingi wabaguzi. Morocco hata km ni wabaguz lkn sio kwa kila kitu, km biashara utafanya tuu bila Shida
 
Back
Top Bottom