Fursa nchini Morocco: Biashara ya mbuzi inalipa sana

Hao waliokufanyia ubaguzi labda uliwaudhi , mbona mimi nimekaa nao miaka 5 sijaona ubaguzi wowote ?? Tena kuna wakati naumwa nilikuwa na rafiki yangu akisoma mwendo wa masaa mawili na nusu kwa train na alikuwa akija kuniangalia
Itakuwa alieenda na mzungu wake
Akaona wanamchangakia zaidi kuliko yeye huwa wanajua mtu mweusi hatoi tip
 
Sio kwamba wafanyabiashara hawajui. Tatizo ni namna ya kuwasafirisha na gjarama zake. Hizi ndege za kuungaunga hadi Morocco sio rahisi. Miuondo mbinu ya usafirishaji wa meli poa migumu.
 
Kingine watanzania wavivu kutafuta masoko mengine,na hili la kingereza ni tatizo pia anashindwa kuconnect na watu wapya. Nnimetembelea sehem izo sijakutana na mtanzania kwenye biashara izo.
Watanzania ndio jamii ya watu ambao hufasiri kwa uchache zaidi.. yani unawezakuta katika mtaa ni mtu mmoja au hata watu 2 ndio wametoka nje ya mpaka wa Tanzania
 
Si kweli,mpaka mbuzi. Cha msingi uzifikishe salama. Mbuzi wanauzwa wengi
Mkuu, kuna vitu navijua vizuri sana kwenye biashara hiyo, kusafirisha mbuzi wazima ni biashara kichaa,unaweza kusafirisha,ila sahau kuhusu faida,kwanza waarabu wanachagua sana sana!! Ukimpelekea mbuzi mkubwa sana hanunui, ukimpa aliyenona sana hanunui, waarabu wanapenda mbuzi wadogo,ambao hawajakomaa, angalau ukipeleka nyama kwanza wateja ni wengi, pia ni vigumu kidogo kuanza kuchambua nyama ya mbuzi wa miaka miwili kwenye cold room lenye miili ya mbuzi 2000, kikubwa ni uaminifu, ukipata mteja akakwambia sitaki mbuzi wazee wewe jiongeze, kuna waarabu hawanunui mbuzi sababu tu ya rangi yake, mwingine akiona tu hata mkwaruzo kwenye ngozi hanunui, jifunze zaidi mkuu,nipo kwenye hiyo industry,so najua 1i-2-3
 
shukran...
 
anzia ubalozi wa Morocco hapa tz wakupe details zaidi. Au cheki na ubalozi wa tz huko Morocco ili wakupe info sahihi
 
Tanzania si nasikia tuna export nyama ya mbuzi huwa wanapeleka wapi?

Nahisi ni either Oman au Saudi, Ila nyama ya mbuzi ni dila sana uarabuni, kule sio sana kula nyama ya ng'ombe, wao ni mbuzi na kondoo tu. bado sana hatujawa serious kwenye hiyo ishu, Saudi, Oman, UAE, Qata, Kuwait, Bahrain, Morocco, Tunisia, Algeria yani soko lipo kubwa sana ila sisi tu tumelala
 
Wale siyo waarabu ni moors
 

mkuu mtaji kama ngapi unaohitajika kwa kuanzia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…