Fursa za biashara U.A.E (Dubai)

Kwa wenye uzoefu naomba kufahamu kama ukinunua simu 100pcs na ukazitoa kwenye mabox yake na kuziweka kwenye begi ambalo unasafiri nalo kama mzigo (cargo) na kushuka nao hapo Dar airport kuna kufunuliwa na TRA na kuanza kuombana ushuru? Otherwiz Goodchance jiandae kunitembeza hapo Dubai soon hata kama ni kwa kuja kujionea tu...
 

Simu mpya mwisho ni 5 tu zaidi ya hapo unalipia ushuru.
 
Simu mpya mwisho ni 5 tu zaidi ya hapo unalipia ushuru.

Ahasnte Lucky Sabasaba...naomba kama unajua base ya Revenue ya simu wanayotumia TRA unisaidie maana utakuwa umeokoa muda wangu wa kufuatilia hili jambo kwa TRA. na maanisha wanabase kwenye bei ya kununulia au wanafanyaje na hiyo kodi ni asilimia ngapi?
 

Umenichekesha sana, yaani huyu makanisa yote TZ hayaoni anataka kwenda kusali Dubai.
 
Nakubaliana na wewe Goodchance fursa zipo, nimeishi hapo miaka mitano kabla ya kuamua kurejea..... siyo punde tu ntakuwa na mawasiliano nawe kuanza kuagiza tena mzigo, nikiwa huko nilijaribu kuwaunganisha baadhi ya marafiki kuagiza vifaa vya printing, spea na elektroniki na pia nilijikita kwenye kutuma wino na kuamua kurudi kufanya mambo yangu kwanza lakini baada ya kukaa bongo miaka mitatu nimeanza kupoteza contacts.

Contacts wengi wamehama au kurudi nchi zao na baadhi kupoteza uaminifu.

Export formalities UAE ziko vizuri ila bwana hapa kwetu TUNAUMIZWA na hizi HS codes na system mpya kila kukicha TRA, sijui wewe hapo unaonaje.

Pia Una ushauri wowote kuhusu transport agencies ambazo zitakuwa affordable?
 
Hi vipi waweza kujua bei ya flash Adata original 4gb na 8gb zinapatikana kwa bei gani, pia gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi inatakiwa uwe na burget ya bei gani
 
Hi vipi waweza kujua bei ya flash Adata original 4gb na 8gb zinapatikana kwa bei gani, pia gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi inatakiwa uwe na burget ya bei gani

Hapo kwenye ndege ipo fly Dubai rahisi sana usd430
 
Hiyo Fly Dubai ina Offer maana wanatengeneza jina la ndege yao(ni route mpya)kuanzia sasa mpaka mwezi wa kwanza katikati sikushauri kuja Dubai maana kwa ajiri ya holiday ambazo zimekwishaanza hoteli na bidhaa zipo juu sana,Formula one inaanza Abu dhabi Jmosi hii Hoteli zipo full na cost ya vitu imepanda sana,December yote ipo busy.Kibiashara au Kimatembezi si wakati mzuri kama pesa yenyewe ni ya kuungaunga...
 

Kuna ile hotel Gold plaza bei yake still the same, sama hotel , lapaz na tara hotel sana ndio nnapo fikia.. Bidhaa kwangu napata same price Kama mwanzo sioni kupanda au ikizidi ni kawaida.
 
Ebu ingia booking.com na utazame bei ya hizo hoteli kwa December hizo ni hoteli ndogo sana na ndio kimbilio la waafrika lakini pamoja na udogo wake December zinakuwa juu check Booking.com lakini miezi ya 3-9 ata kwa tsh 28,000/ unapata chumba
 
Ebu ingia booking.com na utazame bei ya hizo hoteli kwa December hizo ni hoteli ndogo sana na ndio kimbilio la waafrika lakini pamoja na udogo wake December zinakuwa juu check Booking.com lakini miezi ya 3-9 ata kwa tsh 28,000/ unapata chumba

Booking.com lazima itakua bei juu hata Kama ikiwa sio peak time ila mie nawapigia cm halafu nawatumia email wana niletea confirmation via email... Anyway sijui kwa wengine Lakini I get best rate always...
 
Je kaka mi naweza pata solo la Asali mbichi nje ya nchi kama kuna soko nitaarifu
 
Booking.com lazima itakua bei juu hata Kama ikiwa sio peak time ila mie nawapigia cm halafu nawatumia email wana niletea confirmation via email... Anyway sijui kwa wengine Lakini I get best rate always...

Sijui point unayojaribu kujenga,Dubai ni kivutio kikubwa sana cha holiday duniani na kipindi cha holiday mid Nov to mid Jan ni msimu wa watalii wengi sana,hoteli zinakuwa juu sana hiyo Tara unayosema japo standard yake ipo chini inakuwa juu pia,ebu wapigie sasa hivi namba yao ni +97142272424 ulizia booking ya December.Dubai miezi ya summer ata Kempinski mall of Emirates utalala kwa Tsh 60,000 lakini sasa ni zaidi ya Tsh 300,000(nimefanya sana booking).Nipo kwenye hospitality Industry hapa Dubai mwaka wa kumi sasa nawashauri msimu huu si mzuri kwa biz mpaka Feb mambo yatapotulia.Lakini pia wawezakuja kupata experience.Kuna jamaa yangu alikujatafuta kazi kipindi cha Ramadhan nikamshauri asubiri akapinga matokeo alikuja kuyaona....Labda umsaidie mleta mada Tara hoteli uwa unalipa Tsh ngapi kwa siku ??
 
Nia yangu ni kukujulisha kua hata Kama ghali sio ghali kiasi hicho kwa hotel Kama hizo, Tara aed200-250, Gold plaza 200, sima 255 na ile ya wa Yemen ilokua karibu na sima opp na chinese commodity pia wana nipa best rate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…