Fursa za Nje ya Nchi: Scholarship (kusoma), Ajira/kujiajirina Biashara/kuwekeza

Huwezi kufikiria kubadili hali ya mambo kwenye nchi yako kwa kumwangalia mwanasiasa anayetembelea V8, huko ughaibuni na kwenyewe wapo wanasiasa ambao wanafuja pesa za umma lakini raia wapo independent kutumia akili zao kujijenga wao na vizazi vijavyo......huwezi kumsusia ngedere shamba la mahindi lakini utahakikisha unamdhibiti ngedere ili mahindi yapatikane shambani......
 
Bro, ni hivi! Kitembea tu kunampa fursa mtu kujifunza vitu vingine. Mfano, kuna jamaa alikwenda India aliporudi karudi na idea ya biashara mpya na anapiga hela sana kwa sasa!! Kibongobongo ilikuwa ngumu kuwa na idea kama hiyo! Exposure, si lazima ukakae maisha yote huko!!

Pili! Kama kijana wako kakosa maisha yaliyosimama hapa nchi, kuna ubaya gani akatoka kuangalia sehemu zingine? Mwisho wa siku opportunities hizi tunawaachia wanasiasa na familia zao tu sisi tunaamini haziwezi kutufikia. Kuzunguka kutafuta maisha duniani kupo, maovu ya wanasiasa yapo kila mahali lakini kama kuna mahali mwanasiasa anafanya uovu na wewe maisha yanakwenda unavyoplan kwa nini usijitose!?

Iko hivi badala ya vijana kulia lia hapa nchini hakuna kazi wala mazingira mazuri ya wao kupata kipato! Watokee tena nahamasisha wizara ya mambo ya nje itanue wigo na kushawishi mataifa mbalimbali yaite vijana kutoka TZ, pengine tabia za majungu na uvivu zitaisha tukianza kujichanganya
 
umeandika sahihi kabisa, huu mwaka hautaisha lazima nitoke hapa bongo nikapate oxposure hata ya siku 30 tu.
 
Wana fanya hivyo kupunguza jam, na kuna muda ni ubinafsi ulio pitiliza ambao msingi wake ni kuanzia katika koo, familia (undugu)
Ni ubinafsi tu ns roho ya umasikini..

Ubinafsi /umimi ...unaisumbuwa sana nchi yetu kuanzia katika level ya undugu mpaka kwa viongozi wetu wajuu..

Ndio maana unakuta ni vigumu sana mtu kukuonesha fursa ya biashara anayoifanya kama inamlipa ipasavyo... akikuonea huruma ataisha kukupa maelezo tu ya jujuuu.
 
Uko sahihi kabisa lakini...
Hakuna mwanasiasa wakufanya hivyo labda kwa nchi niyingine na sio TZ , ubinafsi umetawala sana fursa hapa bongo ni za kupeana "kimya kimya"..
Kama kenya rais wao alipoenda U.k kawapigia pande huko wanatarajia kupeleka wafanya kazi kama 30,000...

Angalia mshahara wa nurse UK , kisha mtu arudi hapa uniambie masuala ya uzalendo
 
Mkuu elewa mada kwanza , hapo nilikua namjibu mtu anasema si vyema kwenda nje kwa maana tutakuwa manamba kwa mabeberu ili hali hapa bongo graduate hatma yao ipo kwa hao wanasiasa wanaotembelea V8
 
"Madakatari huko bush wanalalamikia vifaa tiba hakuna mazingira magumu ya kazi na hakuna solution mtu kama huyu akiona fursa nje kwanini asiende??" hapa inaonyesha jinsi gani usivyo na uelewa, wewe ukikimbilia nje ndo vifaa tiba na mazingira ya kazi yataboreka huko bush? au unategemea mzungu atoe kwao ndo akawatibu huko bush......huna hoja zilizoshiba zaidi ya mihemko, kujaribu kumsusia ngedere shamba la mahindi.
 
Ndio mkuu tunategemea misaada ya vifaa tiba na madawa kutoka taasisis za nje zitusaidie..
nasio mpaka wakutangazie kuwa ni kwa hisani ya watu wa marekani etc.


Tuachane na hayo tu discuss fursa za nje ya mipaka yetu kama ilivyo dhumuni la uzi huu!!
 
Ndio mkuu tunategemea misaada ya vifaa tiba na madawa kutoka taasisis za nje zitusaidie..
nasio mpaka wakutangazie kuwa ni kwa hisani ya watu wa marekani etc.


Tuachane na hayo tu discuss fursa za nje ya mipaka yetu kama ilivyo dhumuni la uzi huu!!
Fursa zipo, sema tofauti na wakenya sisi hatujawa na watu wengi huko ambao wangeweza kusaidia kupata michongo au kualika wenzetu kwenda huko kama watalii ili mambo mengine yaendelee. Pia vijana wanaweza kwenda kupitia fursa za scholarship, ambapo wanaweza ku opt kuendelea na maisha huko. Kuna dada mmoja mkenya yupo marekani huwa anatoa video U-tube kujaribu kutoa uzoefu wake mfano kazi ambazo unatakiwa kuanza kufanya ili kuweza ku settle kabla hujatafuta fursa zaidi.......ni vizuri wale wachache wanaopata fursa kutengeneza network na wakenya kwa sababu wao tayari ni wengi huko kuweza kuwasaidia na wabongo....na pia hili la kutengeneza network na wakenya litasaidia kupata company kupunguza upweke kwa sababu watanzania wengi hawana ustahimilivu wa kuishi nje ya mipaka ya nchi yao.
 
Hapa umewasilisha vitu muhimu sana... !
 
msaada tutani, huyo dada mkenya anatumia jina gani youtube?
 
Saivi vyuo vyote haijalishi ni vya Asia au Europe ni lazima uwe na cheti cha lugha.
 

Tatizo wabongo sasa mtu anaweza akajitoa hivyo ndo kwanza wakaenda kumroga au kumfitinisha… bongo siku hizi roho nzuri ni kujitafutia matatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…