FY2021/22 Serikali kutoa Trilioni 11 kulipa madeni ya nyuma

Uchaguzi wa 2025 tayari CCM ilishashinda kabla ya Uchaguzi kuanza Pole sana " roho mbaya "
 
Ninafikiri huyu ni Samia mwenyewe anajipigia promo..maana post zake ni kujikweza tuuu mwanzo mwisho.

Fanya kazi mama, ni wajibu wako. Huna sababu ya kujinadi kiasi hicho.
Kibaya kinajitembeza ila kizuri siku zote hujiuza.
niwapi kasifiwa Rais hapa,Chadema mtateseka sana kwa speed ya mama,
 
Chama kinakopa tangu lini wewe CHADEMA,
Madeni ni kwa maendeleo ya nchi,
Hayo madeni hata wewe yamekunufaisha kwa namna moja ama nyingine,

Hongera Sana Rais Samia tuko nawewe sana tu,
CHADEMA kilishakufa kitambo sana,
 
kutokana na Deni la taifa kupaaa, tunaiomba Serikali ihakikishe inadhibiti na kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa mfano;

1. Safari za nje zisizo za lazima zizuiwe/zipunguzwe.

2. Vikao vya Bunge vipunguzwe, ratiba ya vikao iangaliwe upya kuanzia mwakani.

3. Matumizi ya magari ya V9/v8 ambayo ni gharama kubwa kuyahudumia,

4. Semina na vikao visivyo vya lazima vipunguzwe.

5. Mishara mikubwa kwa baadhi ya watendaji ipunguzwe, isiwe zaidi ya milioni 10 kwa mtendaji 1.
maana kuna baadhi ya taasisi za serikali watu wanalipwa hadi milioni 15 kwa mwezi.

Kama kweli Serikali yetu pamoja na watendaji wake wana uchungu na watanzania basi lazima wafanye kitu ili kuinisuru nchi na kuelemewa na madeni.

haiwezekani nchi imeandamwa na madeni mpaka puani halafu kuna baadhi ya watu/watendaji wanazidi kunyonya tu bila huruma.
hapana, tunataka kuona hatua zinachukuliwa haraka.
 
Wakandarasi vicheko,
Wazabuni vicheko,
Watumishi vicheko,
Watoa huduma vicheko,

Tuacheni utani huyu mama anapiga kazi sana tu,
 
tafuta namna nyingine ya kumpongezq mama,sio inshu ya madeni ,mwal.aliacha madeni,mwinyi aliacha madeni,mkapa aliacha madeni ,jk pia.hakuna ambae ataweza kuyamaliza au kutokukopa.tunachotaka maendeleo basi
 
Naungana na wewe kwa 100% kwenye hili
 
Tulisema tukaonekana wendawazimu, Leo nyie ndio mmethibitisha kuwa MNA matatizo makubwa, niwakumbushe tu kuwa jengeni mifumo na sio mtu, SSH akiondoka mtamsema pia. Samia hatoi pesa na wala haipaswi kutamkwa hivyo ila kwakua ujuaji mwingi hamtakubali

Naungana na wewe mia kwa mia ili nchi iwe na Maendeleo endelevu ni lazima kuwepo na TAASISI IMARA [ STRONG INSTITUTIONS] ambazo zitaleta maendeleo kwa nchi hata kama kutakuwa na mabadiliko ya uongozi!!!

Mnarudia makosa yale yale ya kufikiri Magufuli alikuwa anatoa fedha mifukoni mwake kumbe ni kodi zenu!!
 
tafuta namna nyingine ya kumpongezq mama,sio inshu ya madeni ,mwal.aliacha madeni,mwinyi aliacha madeni,mkapa aliacha madeni ,jk pia.hakuna ambae ataweza kuyamaliza au kutokukopa.tunachotaka maendeleo basi
Daah madeni ya watumishi,
Daah madeni ya wazabuni,
Daah madeni ya wakandarasi
Daah madeni ya watoa huduma

Kweli haya yaliachwa na Mwl, Mwinyi,Mkapa na JK,??!!

KWANINI HAMTAKI KUONA UIMARA WA MAMA?
 
Mama ametoa,mama ametoa.
Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Naona watu wamejipanga kweli kweli kwenye hili
Siasa ni hatari sana
 
Madeni mpaka China na USA wanadaiwa. Hawapati madeni kwa nia ya kujifurahisha tu ni katika kutimizamalengo ya muda mfupi na mrefu.
 
Unayohoja hoja mkuu ila usiogope deni ni stahimilivu kwa kipindi kifupi, chakati na kirefu hii ni kimataifa so relax nchi iko salama sana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…