PreGE2025 G55 & COVID 19, kipimo sahihi cha kumpima Tundu Lissu kiuongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kuna ushahidi zaidi ya hao wahusika wenyewe?
Mahakamani ushahidi wa watuhumiwa wanapokubali kuwa wakitumia na fulani kufanya uhalifu unakataliwa?
Una maanisha G55 wamekiri hadharani kuwa wanatumiwa na CCM?
 
Wamekiri kwa wanaohusika kuwa kuna fedha imetembezwa kwa Mrema na genge lake toka ccm!! Kama walivyo tubu baadhi ya covid 19 kuwa ccm iliwarubuni !!
Unataka watubu hadharani sio? Ili iweje?
 
Sisi wananchi tunaamini taarifa zikitoka hadharani na kwa uwazi otherwise zikiwa za ndani bado tunabaki na maswali.
 
Hali ya sasa ndani ya CDM inahitaji leaderships character kuliko mihemuko, shutuma na visasi. Inahitajika utulivu mkubwa sana wa kiuongozi kufanya reconciliation ndani ya chama otherwise chama kinaweza kuparaganyika zaidi.

Hivyo kwa hali iliyopo kwa sasa ndio itakuwa kipimo sahihi cha kiuongozi kwa Mh. Tundu Antipasi Lissu namna atakavyoweza kurudisha utulivu ndani ya chama kwa kuhakikisha makundi yote ndani ya chama hasa G55 na mengine yanarudi kwenye mstari wa chama.

Swali linabaki, akishindwa kuweka msawazo ndani chama, Je changamoto kubwa za kitaifa ataziweza?

Mungu ibariki Tanzania.
Kumbuka VIRUS haina dawa, hawa ni VIRUS, dawa yao ni kuwafukuza tu, ukiwalea wanaweza hata kufanya uhaini, wameshaonesha waziwazi, unataka uone ishara gani ili ustuke?
 
Kama mbwa na iwe mbwa kudaadeeki. Hawa wote ni wakora na ni wa kufukuziliwa wakafie mbali. Huwezi kakaa na watu walioshindikana ndani ya chama watakifedhehesha. Hakuna muafaka hapa ni kuwatimua chamani tu waende huko watakapovumiliwa utovu wao wa nidhamu
 
Mie kw ayale niliyiyaona ya uchaguzi wa wenyeviti amabpo wapinzaninasilimia 98pct waliondolewa ,,je tunajuaje kama wagonbea wachadema Sasa form zao zitapitishwa na tume bila kufanyiwa figisufigisu?
 
Nyie chawa bakini na maswali , majibu yamekwisha patikana!
Sawa mkuu. Lakini niweke kumbu kumbu sawa sisi sio chawa ni watanzania tunaolisemea taifa letu.

Hoja zijibiwe kwa hoja na sio kashfa.
 
Kumbuka VIRUS haina dawa, hawa ni VIRUS, dawa yao ni kuwafukuza tu, ukiwalea wanaweza hata kufanya uhaini, wameshaonesha waziwazi, unataka uone ishara gani ili ustuke?
Hakuna mahala nimesema wafukuzwe au wasifukuzwe hivyo hakuna cha kunishtua.
 
Kama mbwa na iwe mbwa kudaadeeki. Hawa wote ni wakora na ni wa kufukuziliwa wakafie mbali. Huwezi kakaa na watu walioshindikana ndani ya chama watakifedhehesha. Hakuna muafaka hapa ni kuwatimua chamani tu waende huko watakapovumiliwa utovu wao wa nidhamu
Shida ilianzia kwenye uchaguzi ndani ya chama
 
Hali ya sasa ndani ya CDM inahitaji leaderships character kuliko mihemuko, shutuma na visasi. Inahitajika utulivu mkubwa sana wa kiuongozi kufanya reconciliation ndani ya chama otherwise chama kinaweza kuparaganyika zaidi.

Hivyo kwa hali iliyopo kwa sasa ndio itakuwa kipimo sahihi cha kiuongozi kwa Mh. Tundu Antipasi Lissu namna atakavyoweza kurudisha utulivu ndani ya chama kwa kuhakikisha makundi yote ndani ya chama hasa G55 na mengine yanarudi kwenye mstari wa chama.

Swali linabaki, akishindwa kuweka msawazo ndani chama, Je changamoto kubwa za kitaifa ataziweza?

Mungu ibariki Tanzania.
Lissu ameshafeli! Ujue hiyo ni timu ya watu 74 tayari! Na no wagombea potential sana! Wakienda ACT Wazalendo tumekwisha!
 
Lissu inabidi atulize kichwa na asikilize ushauri wa watu makini, sio watu tu wanaomsifia tu kwa mustakabali na hatima ya chama chake na yeye kubaki kama mwanasiasa mwenye ushawishi na kuheshimika nchini.

Kuna issue naziona huko mbeleni.
Kampeni zikianza July na yeye akiendelea kusisitiza no election, kukinukisha na kuzuia uchaguzi atapoteza support kubwa sana ndani na nje ya chama. Wengi zaidi wanajitokeza kumpinga.

Serikali inaweza kumkamata kumpa kesi ya kutaka kuvuruga takwa la kikatiba. Wakamweka ndani mpaka uchaguzi uishe. Sioni nchimbi na Samia wakiwa na huruma. Huruma anajua ndiye Rais ajaye hawezi kuchezea hiyo nafasi na Samia sababu hajamaliza kuuza kila rasilimali muhimu.

Baada ya uchaguzi, wanachama wengi wa Chadema watavunjika moyo, sababu hawataweza kuzuia uchaguzi. Mtaji wa kisiasa na ushawishi wa Lissu ndani ya chama chake utakuwa mdogo sana, uasi utaongezeka.

Baada ya October kutokana na kukosa kuungwa mkono itabidi ili aeendelee kuongoza kutumia ubabe, huku akifukuza wanachama wengi wanaompinga au ajiuzulu kwa kukosa support.
Mtu mzima hatishiwi nyau. Ccm itende haki siyo kutishiana maisha. Tumesha komazwa na utekaji, kuuawa na kupotezwa. Kilichobaki huku mtaani tutaanza kupotezana ili kulipiza kisasi
 
Hali ya sasa ndani ya CDM inahitaji leadership character kuliko mihemuko, shutuma na visasi. Inahitajika utulivu mkubwa sana wa kiuongozi kufanya reconciliation ndani ya chama otherwise chama kinaweza kuparaganyika zaidi.

Hivyo kwa hali iliyopo kwa sasa ndio itakuwa kipimo sahihi cha kiuongozi kwa Mh. Tundu Antipasi Lissu namna atakavyoweza kurudisha utulivu ndani ya chama kwa kuhakikisha makundi yote ndani ya chama hasa G55 na mengine yanarudi kwenye mstari wa chama.

Swali linabaki, akishindwa kuweka msawazo ndani chama, Je changamoto kubwa za kitaifa ataziweza?

Mungu ibariki Tanzania.
Mbinu za kimedani zilizotumika kuizima CUF ya Maalim Seif huko Zenji kwa kukivuruga hicho chama mpaka Seif kukihama Sasa zimehamishiwa kwenye Chadema ya Lissu
 
Mtu mzima hatishiwi nyau. Ccm itende haki siyo kutishiana maisha. Tumesha komazwa na utekaji, kuuawa na kupotezwa. Kilichobaki huku mtaani tutaanza kupotezana ili kulipiza kisasi
Maneno ya kijasiri kabisa. Mkiwa watu milioni kama wewe na bunduki mna nafasi ya kuzuia uchaguzi. Mnahitajika milioni kumi.

Utatokea siku hiyo kuzuia na mikono yako, tueleze mbinu utakazotumia. Tunaweza kukuunga mkono.
 
Atajifunza ama?
Mbinu za kimedani zilizotumika kuizima CUF ya Maalim Seif huko Zenji kwa kukivuruga hicho chama mpaka Seif kukihama Sasa zimehamishiwa kwenye Chadema ya Lissu
 
Maneno ya kijasiri kabisa. Mkiwa watu milioni kama wewe na bunduki mna nafasi ya kuzuia uchaguzi. Mnahitajika milioni kumi.

Utatokea siku hiyo kuzuia na mikono yako, tueleze mbinu utakazotumia. Tunaweza kukuunga mkono.
Siku ya uchaguzi tutalala barabarani ili mtupige risasi mimi na demu wangu. Kuliko kusubiri kutekwa na kuuawa kinyama
 
Back
Top Bottom