Gambo amwambia DED na viongozi Arusha hatishiwi Nyau

Gambo amwambia DED na viongozi Arusha hatishiwi Nyau

Siku zote mambo yasiyo na Mungu huwa na migogoro daima! Gambo unajua kuwa ushindi wako haukuwa halali, dhambi hii itawaandama hadi ndani ya vizazi vyenu.
 
....chickens coming home to roost.
 
Gambo yupo sawa, unamfungiaje mtu biashara, atailipaje hiyo kodi kama haingizi chochote...

Cc: mahondaw
 
Nakaona hako kaDC ka arusha kama kanaharajati flani hivi kajinga kasikojua la kufanya .kana dhani ofisi ya DC ni sawa na ile ya uvccm iringa
Gambo ni nani wako?
 
Vyuma vinasigana. Mtasagana mpka mchambuke chambuke
 
Ndiyo tatizo kwa mtu aliyekuwa mkuu wa mkoa, tena mkoa huo huo halafu anakuwa mbunge mmojawapo katika mkoa huo huo. Anajisahau kuwa yeye sasa ni mouth piece tu ya wananchi wa jimbo lake kwa serikali ya wilaya au mkoa wake au taifa kupitia bunge la nchi. Anashindwa kujua kwamba yeye si mtendaji tena wa serikali. Anashindwa kujua kuwa yeye hana tena mamlaka ya kiserikali. Anashindwa kujua kwamba yeye sasa yuko chini ya mamlaka ya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ambao ni wawakilishi wa rais wa JMT katika maeneo yao. Anashindwa kujua kuwa watu hao yaani DC au RC wana mamlaka ya kisheria ya kumsonda ndani (mahabusu) kwa kipindi cha zaidi ya masaa 48 kwa sababu yo yote ile au hata bila sababu yo yote. Ni wakuu wake na wanainchi wote walio kwenye maeneo hayo. Yeye kuwa ni mbunge kupitia chama tawala hakimfanyi kuwa tofauti na yule mbunge aliyepitia chama cha upinzani hususani yule Lema.
Huyo jamaa ni mjinga sana sijui alidhani ubunge ndio fainali kwa sasa yeye ni beggar kwa Mkurugenzi, bila Mkurugenzi yeye hatoboi hata tone halafu nawanganinia watumishi kuwepo kwenye kikao kwa msingi upi?? Mtumishi wa Serikali hawajibiki kwake yeye apambane na uongozi wa CCM WILAYA hana tena mamlaka.
 
Gambo ni nani wako?
Ni
huyo jamaa ni mjinga sana sijui alidhani ubunge ndio fainal kwa sasa yeye ni beggar kwa Mkurugenzi,bila Mkurugenzi yeye hatoboi hata tone halafu nawanganinia watumishi kuwepo kwenye kikao kwa msingi upi??,Mtumishi wa Serikali awajibiki kwake yeye apambane na uongozi wa CCM WILAYA hana tena mamlaka.
Sema yeye anawazidi mpunga hao kina Ded na mkuu wa mkoa na marupurypu
 
Acha wachapane wao kwa wao sasa! Arusha tena! Mitano tena
 
Ni

Sema yeye anawazidi mpunga hao kina Ded na mkuu wa mkoa na marupurypu
Kwa mshahara hawazidi chochote. Tena mshahara wa mkuu wa mkoa ni mkubwa kuliko wa mbunge. RC analingana na waziri kimshahara. Anachowazidi ni hayo maposho waliojiwekea wabunge ambayo Rais anaweza yafyeka wakati wo wote.
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amewaambia viongozi wa wilaya ya Arusha na mkurugenzi wa jiji la Arusha(DED) kuwa hatakubali kukwamishwa na viongozi wa jiji la Arusha wakati akitekeleza majukumu yake.

Gambo ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mkutano wa Baraza la wanawake wa UWT uliofanyika kwenye hotel ya Mount Meru jiji hapa na kusisitiza kwamba hataacha kuwatetea wananchi licha ya vikwazo vingi anavyopitia kwenye mikutano yake ya kutatua kero za wananchi.

"Nimesikia kwamba wamepanga kunikamata, sitaogopa mtu Mimi ni mbunge ninayetimiza wajibu wangu sitishiwi Nyau na waache kufanya Mambo ya kishabiki" Alisema Gambo

Aliongeza kuwa Kuna mkakati unaoendeshwa na mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt. John Pima wa kuwazuia watendaji kushiriki mikutano yake inayoendelea katika mitaa mbalimbali katika Jimbo la Arusha.

"Mkurugenzi amewahi kuwatoa watendaji wa halmashauri katika kikao changu lakini kwa sababu ni mgeni naamini anaendelea kujifunza atazoea" Alisema

Gambo anatuhumiwa kuwashawishi wafanyabiashara wa maduka wasilipe Kodi baada ya kuamuru maduka yaliyofungwa kwa sababu ya kutolipa Kodi yafunguliwe Jambo ambalo linaikosesha mapato serikali.

Acha wafu wazike wafubwao
 
Gambo is followed by Karma. Alitumia sana mamlaka yake alipokuwa RC kumsumbua Lema. Akaendelea mpaka kuwasumbua akina Msando . Kwa Arusha kulivyo Gambo wameshaanza kumfanyia figisu wenyeji na wamepata urahisi sababu kapelekewa DC sahihi kabisa.

Ajiandae kisaikolojia kuwa mbunge wa muhula mmoja. Wenyeji hawajafurahi sana mgeni kuwa mbunge wao. Watu wa kaskazini wote wzna huo ubaguzi
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amewaambia viongozi wa wilaya ya Arusha na mkurugenzi wa jiji la Arusha(DED) kuwa hatakubali kukwamishwa na viongozi wa jiji la Arusha wakati akitekeleza majukumu yake.

Gambo ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mkutano wa Baraza la wanawake wa UWT uliofanyika kwenye hotel ya Mount Meru jiji hapa na kusisitiza kwamba hataacha kuwatetea wananchi licha ya vikwazo vingi anavyopitia kwenye mikutano yake ya kutatua kero za wananchi.

"Nimesikia kwamba wamepanga kunikamata, sitaogopa mtu Mimi ni mbunge ninayetimiza wajibu wangu sitishiwi Nyau na waache kufanya Mambo ya kishabiki" Alisema Gambo

Aliongeza kuwa Kuna mkakati unaoendeshwa na mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt. John Pima wa kuwazuia watendaji kushiriki mikutano yake inayoendelea katika mitaa mbalimbali katika Jimbo la Arusha.

"Mkurugenzi amewahi kuwatoa watendaji wa halmashauri katika kikao changu lakini kwa sababu ni mgeni naamini anaendelea kujifunza atazoea" Alisema

Gambo anatuhumiwa kuwashawishi wafanyabiashara wa maduka wasilipe Kodi baada ya kuamuru maduka yaliyofungwa kwa sababu ya kutolipa Kodi yafunguliwe Jambo ambalo linaikosesha mapato serikali.

Umeanza.Ulimwona Lema hafai sasa pambana na wana ccm wenzio pamoja na hali yako.
 
Mh. Gambo:
Kuna kajimsemo eti " Dhuluma haidumu na ikidumu huangamiza"
Hebu tuone sasa.
 
Back
Top Bottom