Gambo amwambia DED na viongozi Arusha hatishiwi Nyau

Mkuki kwa nguruwe........ hata bado, soon utavuliwa uanachama wa CCM kwa utovu wa nidhamu. Ulikuwa RC tamaa yako na majisifu yamekuponza.
 
Juzi kati hapa baada ya kutoka kwenye mkutano wa urasimishaji ardhi kule muriet kuna maneno nilisikia akiyatamka backstage,nikajua tu sasa anaanza ile "kazi"yake rasmi!! Anayemlenga hapo ni mkurugenzi, yaani anataka mkurugenzi awe anaenda kumuomba ruhusa ya kufanya kazi zake,hakumbuki jinsi mwaka ule wa mwisho kwa mkuu Felix Kijiko ntibenda alivyopata fadhaa baada ya yeye gambo aliyekuwa mkuu wa wilaya miaka hiyo alipowanyima watumishi wa halmashauri wasiende kwenye viwanja vya nanenane ambapo mheshimiwa ntibenda alikuwa akizindua maonyesho ya wakulima!! Tena akawaambia kabisa watumishi hao kuwa yeye ndiye bosi mpya,na atakayekaidi agizo lake na kwenda uwanjani basi ajihesabie kuwa kazi imeisha! Ntibenda akajikuta uwanjani bila wasaidizi!! Na baada tu ya muda ntibenda akaondolewa arusha na gambo akachukua nafasi yake! Baada ya hapo gambo akahamishoa majungu kwa mkurugenzi wake,akavimba hadi akaondoka naye,mara kamanda wa uvccm mbaya,mara mbunge mbaya,mara polisi,yaani huyu gambo anatamani afanye kazi peke yake,na magufuli anamjua vizuri sana ila hana jinsi,mtoto mbaya sana huyu gambo
 
Gambo hajui tofauti ya mbunge na mkuu wa mkoa..

Anataka kutoa amri Kwa watendaji wa wa mkoa wakati yeye ni mbunge Tu
Alidhani u CCM wake utambeba, matokeo yake anaambiwa afuate taratibu, anaanza kuliga kelele kama mbayuwayu.
 
Igizo tu ili wavute watu baada ya kuona watu wa Arusha wamempotezea. Anadhani akijifanya anataka kukamatwa ndio atapata umaarufu au uungwaji mkono kama ilivyokuwa kwa Lema.
Yaani iwe kiki awalaumu viongozi mbele ya media??
 
Kwanini DC asimtupe ndani tu huyu ili na yeye aonje radha ya kule ndani? Akiendelea kuropoka hivi aswekwe ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…