Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kudai mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo haudhurii vikao, mbunge huyo amesema suala hilo linahitaji elimu kwa sababu yeye ni mbunge na ana vikao vya Bunge.
"Mimi sio ofisa tarafa, siyo mtendaji wa mtaa wala kata, mimi ni mbunge wa wananchi ambaye kazi yangu kubwa kwenda kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kuwawakilisha wananchi wa Arusha Mjini.
"Katika Bunge yeye sio mjumbe, sasa anaposema sihudhurii vikao anamaanisha nini? Anatakiwa afafanue, maana kumuongelea mjumbe hupaswi kuongea jumla jumla tu," amesema Gambo.
Soma Pia: Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha
Jana, Jumatatu Januari 6, 2025 wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyekuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa- Sambasha- Tumbolo ya kilomita 18 kwa thamani ya Sh23 bilioni, Makonda alidai Gambo haudhurii vikao.
Makonda alisema hayo, baada ya Gambo kuelezea changamoto za barabara za Mkoa wa Arusha, akimuomba Ulega ampatie majibu.