Pre GE2025 Gambo: Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali ni Mbunge, Makonda anahitaji kuelimishwa

Pre GE2025 Gambo: Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali ni Mbunge, Makonda anahitaji kuelimishwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makonda analitaka jimbo la.arusha kashaanza fitina kama kawaida yake. Kigamboni.wanamuachia.mwijaku
 
Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kudai mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo haudhurii vikao, mbunge huyo amesema suala hilo linahitaji elimu kwa sababu yeye ni mbunge na ana vikao vya Bunge.

"Mimi sio ofisa tarafa, siyo mtendaji wa mtaa wala kata, mimi ni mbunge wa wananchi ambaye kazi yangu kubwa kwenda kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kuwawakilisha wananchi wa Arusha Mjini.

"Katika Bunge yeye sio mjumbe, sasa anaposema sihudhurii vikao anamaanisha nini? Anatakiwa afafanue, maana kumuongelea mjumbe hupaswi kuongea jumla jumla tu," amesema Gambo.

Soma Pia: Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Jana, Jumatatu Januari 6, 2025 wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyekuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa- Sambasha- Tumbolo ya kilomita 18 kwa thamani ya Sh23 bilioni, Makonda alidai Gambo haudhurii vikao.

Makonda alisema hayo, baada ya Gambo kuelezea changamoto za barabara za Mkoa wa Arusha, akimuomba Ulega ampatie majibu.
Malalamiko ya Makonda ni Gambo kutokuhudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha. Katika majibu yake Gambo kwanini ameweka mkazo zaidi kwenye mahudhurio ya vikao vya Bunge ambayo Makonda hakuyahoji?
 
Gambo aende kwenye vikao kufanya nini? Ndiko anawajobika? Vikao vyake ni vya Bunge na sio vya Watendaji.

Mjinga ni Bashite
Mbunge ni mjumbe wa vikao fulani ndani ya mkoa wake. Hivyo ndivyo vikao ambavyo Gambo anadaiwa kutokuhudhuria!
 
Mbunge ni mjumbe wa vikao fulani ndani ya mkoa wake. Hivyo ndivyo vikao ambavyo Gambo anadaiwa kutokuhudhuria!
Halazimishwi kuhudhuria maana ni vikao vya Watendaji kutoa mrejesho.

Makonda na watu wake watatue shida za watu na sio kumkataza Mbunge kubainisha Changamoto za Wananchi.
 
Halazimishwi kuhudhuria maana ni vikao vya Watendaji kutoa mrejesho.

Makonda na watu wake watatue shida za watu na sio kumkataza Mbunge kubainisha Changamoto za Wananchi.
Kumbuka, mbunge kwa nafasi yake pia ni mjumbe wa Baraza la madiwani. Mbunge mwenye nia ya kutatua shida za wapigakura wake hakosi kuhudhuria vikao ambavyo yeye ni mmoja wa mjumbe wake, bila sababu ya msingi.
 
Kuwa mjumbe ndio kunazuia yeye asiongee Changamoto za eneo na Wananchi wake Kwa viongozi?
 
Inaonekana kuna mwingilianp wa madaraka na hili linasababishwa na katiba mbovu,kwani anayetakiwa kumwajibisha mbunge ni nani
 
Back
Top Bottom