milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Gambo awe mwangalifu anaweza asirudi tena bungeni katika bunge lijalo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Gambo awe mwangalifu anaweza asirudi tena bungeni katika bunge lijalo.
Malalamiko ya Makonda ni Gambo kutokuhudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha. Katika majibu yake Gambo kwanini ameweka mkazo zaidi kwenye mahudhurio ya vikao vya Bunge ambayo Makonda hakuyahoji?Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kudai mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo haudhurii vikao, mbunge huyo amesema suala hilo linahitaji elimu kwa sababu yeye ni mbunge na ana vikao vya Bunge.
"Mimi sio ofisa tarafa, siyo mtendaji wa mtaa wala kata, mimi ni mbunge wa wananchi ambaye kazi yangu kubwa kwenda kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kuwawakilisha wananchi wa Arusha Mjini.
"Katika Bunge yeye sio mjumbe, sasa anaposema sihudhurii vikao anamaanisha nini? Anatakiwa afafanue, maana kumuongelea mjumbe hupaswi kuongea jumla jumla tu," amesema Gambo.
Soma Pia: Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha
Jana, Jumatatu Januari 6, 2025 wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyekuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa- Sambasha- Tumbolo ya kilomita 18 kwa thamani ya Sh23 bilioni, Makonda alidai Gambo haudhurii vikao.
Makonda alisema hayo, baada ya Gambo kuelezea changamoto za barabara za Mkoa wa Arusha, akimuomba Ulega ampatie majibu.
Mbunge ni mjumbe wa vikao fulani ndani ya mkoa wake. Hivyo ndivyo vikao ambavyo Gambo anadaiwa kutokuhudhuria!Gambo aende kwenye vikao kufanya nini? Ndiko anawajobika? Vikao vyake ni vya Bunge na sio vya Watendaji.
Mjinga ni Bashite
Halazimishwi kuhudhuria maana ni vikao vya Watendaji kutoa mrejesho.Mbunge ni mjumbe wa vikao fulani ndani ya mkoa wake. Hivyo ndivyo vikao ambavyo Gambo anadaiwa kutokuhudhuria!
Kumbuka, mbunge kwa nafasi yake pia ni mjumbe wa Baraza la madiwani. Mbunge mwenye nia ya kutatua shida za wapigakura wake hakosi kuhudhuria vikao ambavyo yeye ni mmoja wa mjumbe wake, bila sababu ya msingi.Halazimishwi kuhudhuria maana ni vikao vya Watendaji kutoa mrejesho.
Makonda na watu wake watatue shida za watu na sio kumkataza Mbunge kubainisha Changamoto za Wananchi.
Kuwa mjumbe ndio kunazuia yeye asiongee Changamoto za eneo na Wananchi wake Kwa viongozi?Kumbuka, mbunge kwa nafasi yake pia ni mjumbe wa Baraza la madiwani. Mbunge mwenye nia ya kutatua shida za wapigakura wake hakosi kuhudhuria vikao ambavyo yeye ni mmoja wa mjumbe wake, bila sababu ya msingi.