Pre GE2025 Gambo: Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali ni Mbunge, Makonda anahitaji kuelimishwa

Pre GE2025 Gambo: Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali ni Mbunge, Makonda anahitaji kuelimishwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao ni km mwashamba na tlaatlaah, wasituchoshe tuko busy na uchaguzi wa Chadema..!
Wamwambie mama yao awaandalie ulingo wazichape
 
Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Mrisho Gambo amemjibu Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda mara baada ya kuumbuliwa hadharani kwa kutoshiriki kwenye vikao na kuambiwa "Anatafuta umaarufu wa Kijinga"

"Lazima afahamu kwamba mimi sio Mfanyakazi wa Serikali, mimi ni Mwakilishi wa Wananchi, mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mtu ambaye anaweza kutoa taarifa na rekodi kwamba sihudhurii vikao kwa mujibu wa sheria ni Bunge na sidhani kama yeye kwa nafasi yake ni sehemu ya Bunge"

Pia, Soma: Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

"Ule mkutano haukuwa mkutano wa Mkuu wa Mkoa, ile ziara haikuwa ziara ya Mkuu wa Mkoa, ilikuwa ni ziara ya Waziri wa Ujenzi na mimi niliyemuuliza ni Waziri wa Ujenzi nilitegemea yeye ndiye angeweza kutupatia majibu ya changamoto yetu lakini cha kushangaza zaidi nikaona Bwana Makonda ametoa majibu ambayo kimsingi hayakuhusiana na hoja ambazo nimezijenga"
View attachment 3194787
Hiyo ni sehemu ya aliyoyaongea Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akiongea leo Januari 7, Arusha kumjibu Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda ambaye jana alisema Mbunge huyo haudhurii vikao kama inavyotakiwa.
Kwenye vikao vya halmashauri ambavyo vinaundwa na madiwani ambao pia ni wawakilishi wa wananchi kikata mbunge ni mjumbe kwa hiyo ni lazima ahudhurie vikao full stop.Vikao vya bunge vinajulikana na wabunge wengine wakisikia kuna kikao cha halmashauri ambamo jimbo lake limo huomba udhuru kwa spika na kuhudhuria kwanini huyu mndege_hay haelewi?
 
HUYU NAE NI MJINGA TU.
HOJA YA MAKONDA NI AWE ANAHUDHURIA VIKAO BASI.

MIMI NAMUONGEZEA,KAMA HAWEZI KUHUDHURIA VIKAO,BASI AWE NA MWAKILISHI KILA KIKAO.

NJE YA HAPO HUU NI UJINGA WA MBUNGE.
What goes around comes around msemo wa wazungu, akiwa mkuu wa mkoa miaka ya JPM alikorofishana na Lema akiwa mbunge hapo Arusha mjini, leo yeye ni mbunge anagombana na mkuu wa mkoa tena kwa namna ile ile ya hadharani mbele ya kamera za runinga.
 
Wanagombania nini??
Gambo ahudhurii vikao vya ngazi ya mkoa anakuja kuuliza maswali mbele ya waziri wa uchukuzi katika mkutano wa wazi mbele ya wananchi, Makonda kamshukia kwa kumwambia awe anahudhuria vikao kwani huko hujibiwa hata hizo hoja anazoziuliza katika mkutano huo wa hadhara.
 
Point ya makonda ipo clear, Gambo hahudhurii vikao halafu anakuja kuuliza vitu public ili kuwachafua
Makonda alikuwa clear kabisa - kwamba anaongelea vikao tofauti na vikao vya Bunge Dodoma. Mnyonge mnyongeni lakini this time around, Makonda yupo sawa
 
Back
Top Bottom