Game station business: Naomba taarifa kuhusu hii biashara

Hiyo ya kuharibu pad ndo kawaida kabisaa, kukuta log imelegea kama jino la kikongwe
 
Ila pia kuna Game centre zile za high standard kuna kipindi walikua wanachezesha Ps4 lisaa ni 5000/=,Ps5 lisaa ni 10000/= na virtual reality dakika 20 ni 10000/=
Na ndio ninachotaka kukifungua, Not only high Standard but Also Quality and Premium Office.

Sitaki Games za 500 au 700 au Buku, nahitaji wateja watakaoweza Afford gaming time kuanzia 5000 kwenda mbele.

Hiki ni kitu kinachopendwa na wengi ni lazima kuwe na mchujo wa aina ya wateja.

Nimelenga Watu wakishua,wasio na shida hata kidogo hivyo sitegemei Kupata Mtoto au mtu asie na kipato.

Minimum Budget ya Hii Project niliyopanga itumia katika Vifaaa tu, ni 20m

Hii 20m nataka iingie katika ununuaji Games aina zote. Budget ya kubrand Ofisi najua haiwezi isha 10m...

so Plan ni 30m kwa kuanzia, the rest of the cost sizijui ndio mana nahtaji miongozo Yenu.
 
Hizo ulizoonuesha hapo ni next level sio hz za kimtaani mtaani.

Hapo unaongelea ps5 na gaming pc ambazo bei ni za gari.😂
Mtaji nilioplan kuwekeza sio wa Hizi Ps za kimtaaani ndugu zangu.

Hii ni biashara kama biashara zingine, hivyo Mtaji ulio mezani ambao nipo willingly kuutoa kwa kuanzia ni 20m kwa Vifaaa.

Branding Office nnje na Ndani ni 10m so jumla Kuuu Ofisi nataka isile zaidi ya 30m na kama itazidi basi mnielekeze nini kitahitajika cha muhimu.

TARGET ya wateja ni HIGH INCOME customers

Si deal na Watoto labda Mzazi amlete mtoto wake maana sitokua na Game ya Bei rafiki kwa MTOTO.
 
Kwa flexibility hizi hizi Gaming pc zinakua Vr na hayo magari.

Mfano hicho kiti na Gari ni Controller ya Game inaweza kuwa ya Ps ama Pc ama vyote.

Hata hio VR unayoiona ina waya ina maana ni Highend hizi za Ps na Pc.

Zipo Vr portable ambazo ni standalone sema hizi hazina Content nyingi kama Oculus Go.

Kwa bei rahisi zaidi Ps4+Vr Headstet itakucost around 1.5-2M hivi then una subscribe Ps+ Deluxe kwa mwaka Site za Magumashi around $40 hutapata games zote pengine utoe laki kadhaa kununua games nyengine.

Hivo viti vina bei pia andaa 1m+

Kuna mdau humu HansMapunda alikua akitengeneza Homemade ya hizo controller zenye usukani.

Cha muhimu mkuu nenda kacheze, ukijua jina la game ni rahisi kujua platform gani wanatumia na namna utakavyoweza kupata ama ku upgrade kuleta kilicho bora.

Kwa PC unaweza pia sema itakucost sana compare na ps4, 4m kupanda kama unataka Quality nzuri.
 
Location muhimu sanq kwenye hii kitu, unatakiwa eneo ambalo linajitangaza lenyewe.
 
Kwa PC unaweza pia sema itakucost sana compare na ps4, 4m kupanda kama unataka Quality nzuri.
Chief nashukuru kwa muongozo naomba nisaidie kuchanganua kulingana na mtaji huu niweke aina gani ya mashine kulingana na uzoefu wako wa haraka haraka kuhusu haya makitu.

Mtaji ni 20m

Nichanganulie hapo niweke vr ngap,ps ngap,viti vingapi yani nisaidie kuimaliza 20m yote katika vifaaa BORA kabisa.

Kama kuna Games za kununua zujumlishe ndani humo humo kwenye hiyo 20m yani staki izidi hiyo pesa hata senti kwenye vifaaa Tu.
 
Mkuu tafuta kwanza Eneo, sehemu ndio itakuonesha namna ya kupangilia hivyo vitu. Marketing ngumu sana Tafuta eneo linalojiuza hasa kwenye Malls.

Vyema tembelea Mkuki na Aura uone wenzako wanavyofanya kazi.

Vyema pia uwe na Machine za kampuni moja uweze ku share account, hii itasaidia kutonunua kitu mara 2 kama games.
 
Mkuu kuhusu eneo lipo under control,sihitaji Mall kuna sehemu tayari ni BEST nimeshaiona ni swala la kusimamisha tu tofali.

Eneo ni swala liko ndani ya uwezo wangu kwa asilimia 100 na zaidi,Wateja sio tatizo ninachoamini ni mahali ulipotega OFISI ndio pana asilimia 90 kukufanikisha/kukufelisha ktk biashara husika.

Mkuu katika hii ishu nahitaji tu mchanganuo wa namna ya kununua games na vifaaa,Kuhusu wateja wanapatikanaje hayo maswala niachieni mimi (ndio mechi zangu za nyumbani hizo)

Mimi changamoto kubwa n nini ninunue,nini niache,nini kianze nini kifate,nk HILO TU. (ndio sijui kitu)
 

Mkuu siwezi kukupa ushauri 100% ila kuna Tier kama 4 hivi za Hizo VR, unaweza uka mix kutegemeana na soko,

1. Standalone VR headset
2. Ps4 VR
3. Ps5 VR
4. Pc VR.

Nilikuuliza size ya Chumba ili ujue unaweka ngapi, mfano kama unaweka Machine 2 ama 4 za VR vizuri utafute PC sababu Budget yako ni kubwa, ila kwa Ps5 pia si mbaya sababu jina tu Ps5 linauza, mtu ambaye si mjuzi sana wa Games ukimtajia Ps5 ni rahisi kumconvince kuliko ukimwambia Oculus.

Kama una plan ya kuweka VR nyingi ili upate hela nyingi kwa mpigo basi hizo Ps4 VR maana budget hio unaweza weka system hata 10.

Pia Ps4 na ps5 unaweza mix pamoja zinatumia Account moja kuna benefit unapata, mfano hio ps+ unatumia machine zote 2.

Vitu kama PS, VR headset si kazi unaweza agizishia online ama ukanunua hapa hapa, issue kubwa ni hicho kiti na usukani wake. Racing wheel za Logitech kibongo bongo bei kubwa kushinda Ps yenyewe na kuileta toka nje pia ni changamoto kutokana na uzito wake, unless ununua vyote nje vije na Meli.
 
Mkuu ukifikia kwenye stage ya designing the place naomba nipe hio kazi mkuu.
 
Je ni watoto tu wanacheza hizi games?
VIpi kama ukiweka age restriction 18ys or 15yrs wateja watapatikana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…