TANZIA Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia

TANZIA Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia

Huyo mlevi na chapombe ulevi umeigharimu afya yake

Endeleeni kunywa na kujishindilia mi bia na miAlcohol kupitiliza kwa makusudi muue figo na maini

Mjifariji kwa kusema Kufa ni kufa

Mnamuona Dr Janabi ni Punguani hajui starehe anapowapa ushauri
Janabi na mahubiri yake yoote Yale Kuna siku atalamba ardhi! Na hata yeye hajui atakufa kwa lipi!
Figo zinakufa kwa sababu nyingi sana, wala Sio pombe tu, chumvi kwa mfano inajua figo, Ni nani hatumii chumvi,
 
Huyo mlevi na chapombe ulevi umeigharimu afya yake

Endeleeni kunywa na kujishindilia mi bia na miAlcohol kupitiliza kwa makusudi muue figo na maini

Mjifariji kwa kusema Kufa ni kufa

Mnamuona Dr Janabi ni Punguani hajui starehe anapowapa ushauri
Poa mkuu

Wewe utaishi milele

Hongera sana kwa kuhukumu wazima na wafu
 
Poleni wote mlioguswa na Msiba huu

Kuna mdau humu alitabiri kuhusu hili mara baada ya Kifo cha Ruge, then Efrahim Kibonde wakasema anayefuata atakuwa Gardner G. Habashi

Angekuwa Mkuu GENTAMYCINE angesema kuhusu wale wadudu wa Uganda

Pumzika Kwa amani Le Captain 😭
Tunaoijua vyema hiyo Ofisi yao na kinachowakumba hasa tokea wakiwa kule Kitega Uchumi wala hatushangazwi na Vifo vya hawa Watajwa wako watatu. Tujitahidi sana Kuutumia huu Umaarufu wetu vizuri na ikiwezekana Watu wajitahidi Kuukataa kwani una Athari zake nyingi sana.

Ngoja nitafute nyimbo za Wakongo hasa zile ambazo Gitaa la Solo limepigwa na Mwamba Dally Kimoko niburudike zangu.
 
Namuonea huruma binti yake
Mimi naogopa mtu wangu wa karibu kufa😒 yaani inakua ndo humuoni tena?😭
Mfano wa kifo ni kama mpo darasani wanafunzi , mnapiga kelele mwalimu kaja na fimbo akasema anapiga darasa zima .

Anaanza mwanafunzi wa kwanza kuchapwa alafu wewe wa huko dawati la mwisho unatetemeka na kuogopa wakati kama ni kuchapwa utachapwa tu .
 
Binafsi Mimi nilikua mpenzi sana wakusikiliza JAHAZI hasa segment ya Mastory ya town kipindi kibonde akiwepo, kibonde alipofariki ndio nikaacha kabisa, Sasa Gardner nae kaenda, kile kipindi kina PENGO KUBWA
Screenshot_20240420-102537.jpg
 
Loh! RIP. This kind of lifestyle is so problematic. Pombe, nyama, magari, starehe, vitakula vichwa vingi sana vya vijana/watu wazima
Mimi ndiyo maana (sisemi sitakufa) nimeamua rasmi ule muda wangu wa ziada niwe nafanya mazoezi ya kukimbia na kutembea na kula chakula na familia yangu tu.

Ni program nimeianza hii wiki ya pili imani yangu Mungu atanisaidia,lakini ukweli usemwe tunaoishi mijini kuna maisha fulani ya kizembe sana tunayaishi ambayo ukitafakari kwa kina ndiyo yanayotumaliza,vijijini case za moyo huzisikii kwa vijana au rika la kati hizi ni kwa wazee na tena ni chache mno
 
Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM, Gadner G. Habash (50) amefariki Dunia Leo April 20, 2024.

Gadner maarufu kama ‘Captain’ aliejizolea Umaarufu Mkubwa kupitia Kipindi cha Jahazi, alikua amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na Pressure (Shinikizo la Damu).

Wasafi Media Tunatoa Pole kwa Familia , Clouds Media Group , Ndugu Jamaa na Marafiki . Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi Amein

Wasafi Media

View attachment 2968923

Pia soma
- Mtangazaji Captain G. Habash alazwa JKCI kwa tatizo la Shinikizo la Damu
Duh Lady Jay Dee Si ataumia sana!
 
Back
Top Bottom