Mwanaume kushindana na mwanamke ulieachana nae hasa kwa maneno ( mipasho ) ni kujidhalilisha mwenyewe. Mwanamke akiongea mwanaume fanya kwa vitendo maana wanawake wameumbiwa kuongea na ni wepesi kutoa ya moyoni. Lakini mwanaume mtimilifu tumeumbiwa kifua na uwezo wa kuchuja tunachotaka kusema.
Kama alikuwa na akili zake timamu na alidhamiria kusema hayo AMEKOSEA. Kuna kila dalili za mhusika kutoa kauli hiyo akiwa amelewa.
Kauli za KIUME za kuonyesha huna bifu na X wako:-
1. Sina tatizo naye ndio maana nyumba niliyomjengea nimemuachia abaki nayo.
2. Na muheshimu kwa 1,2,3, aliyonifanyia japo tumegombana
3. Naendaga kusalimia na kuwa hudumia watoto kwake kama mmejaliwa kupata watoto enzi zenu.
Na mambo mengi ambayo hata mimi kijana nikisikiliza naona kweli jamaa KIDUME hana tatizo na X wake.
mimi naona kwa kauli kama hii, ni dalili kuwa mwanaume hakuna na jambo lolote la msingi analoweza kujivunia amelifanya kwa X wake zaidi ya kilichosemwa.
"ooohhh nimem............",
sasa unatafutiwa, unapikiwa, unatengewa, unanawishwa mikono na mara nyingine kulishwa ili iweje????? au alafu huduma ikushinde?
yaani Ng'ombe uilishe alafu isitoe maziwa .............. tupa kule
Hata hivyo shukuru Mungu kwa huo uwezo maana hiyo huduma ingeshindikana hata miezi sita isingefika....