Gari aina ya IST imeibwa leo. Yeyote atakayeiona naomba atupe taarifa

Gari aina ya IST imeibwa leo. Yeyote atakayeiona naomba atupe taarifa

3F69E2E6-6E04-42F5-8895-539E3C3C1549.jpeg
 
Ahsante Mkuu
Ukimiliki gari Bongo na hasa kama inalala sehemu ambazo siyo salama sana unatakiwa uwe walau na ma-ujanja ujanja. Pale inapolala chimbia chuma kubwa liende chini kabisa na lisionekane kwa juu. Chomea chuma kama komeo lakufunga kufuli na gari uwe unapaki juu ya hilo chuma. Baada ya kupaki ingia uvunguni mwa gari, funga nyororo kwenye lile komeo lishikane na difu ya gari kwa chini. Mwizi akipiga moto na kukanyaga mafuta gari haisogei. Njia nyingine ni kuweka alarm ya kuchimbia chini, ambayo unapaki gari na tairi inakanyaga ile alarm. Mwizi akisogeza gari tu uzito wa tairi ukiondoka una activate ile alarm.
 
Ilishawahi tokea jamaa alipiga konyagi kapotea kabisa gari kaliacha alipolipaki karudishwa home na gari ya jamaa yake asubuhi kaamka halioni gari home kaenda ripoti polisi ile anawasiliana na jamaa aliokuwa nao wakamwambia rudi pale tulikuwa tunakunywa akaliona kumbe hakurudi nalo
Mkuu hii ipo na ishawahi kunitokea. Mapombe makali haya sio issue, yanakata kumbukumbu
 
Umeibiwa maeneo gani, mji gani, mkoa gani.
Weka namba ya gari lakini pia chassis number.
Last but not least, saa nane usiku ulikua unatoka wapi? Isije ikawa gari uliiacha ulikotoka.
Au washkaji walikurudisha home ukiwa mbwi Kisha wakaenda kulihifadhi kwao.
Nane usiku ndio unarudi home? Hata walinzi hawarudigi muda huo.
Hii iliwahi kunitokea, niliacha gari bar.
 
Hari zenu wana Jf
Kuna gari aina ya IST imeibiwa leo yeyote atakae iona Naomba atupe taarifa simu 065 954 6653
078 495 5561
T. 441 DZD
Kuna zawadi nono kwa atakae fanikisha kupatika
Pole sana Mkuu, huyo dawa yake ni ndogo sana, nenda kwa Sheikh mchezo utakuwa umeumaliza. Vijana tunakumbwa na tamaa sana. Gari ya ml 12 wataenda kuuza kwa bei ya kuvunja hata ml 5 ili liuzwe faster. Zilinde mali zako. Mali bila ulinzi utataftia wenzio.

Hapo atauza ataenda kuhonga Malaya baada ya wiki hiyo hela inakuwa imeteketea.

Nakumbuka mwaka 2019 nikiwa IRINGA kuna Mkinga mmoja anaitwa MALAGALILA alinitapeli hela yangu kama Milioni 4 enzi hizo nikabaki mikono mitupu hata mia mbovu nikawa sina, Mungu saidia mwaka 2020 nikapataga ajira Serikalini.

Jamaa aliniachia kovu la milele, usimwamini mtu, linda mali yako, hao wezi wanyoshe.
 
Mkuu hii ipo na ishawahi kunitokea. Mapombe makali haya sio issue, yanakata kumbukumbu
Mimi nilirudi mida hii hii ya mdau saa 8+ ile nime park tu nkashuka hata sijazima taa ndani kulala, asubuhi nakuta gari inanguruma tu.

Ni bahati kuna geti na wahuni hawakupita maana geti lenyewe ni kama sikufunga.

Sasa jamaa kama angekuwa mtu wa vyombo ningesema labda hakuzima gari au karudishwa na washkaji home.

Ila mdau pole sana aise sio poa kabisa
 
Daaah umenitisha kiongozi uwizi umerudi kwa Kasi ya 5G yy kizimkazi anasafiri tu wala asomi ripoti yyte pale chamwino.



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Sasa Mkuu mbona taarifa imechelewa sana? Gari iibiwe saa nane usiku, uje kutafuta after 15+ hours?

Ile asubuhi ungeamka na uzi. Ukasambaza kwenye makundi sogozi yote ya WhatsApp na FB, muda huu ungekuwa walau na tetesi.

Kama walishika njia ya Arusha, muda huu wapo Nairobi wanajipongeza tayari.

Mungu akusaidie na pole sana.
 
Back
Top Bottom