Gari aina ya IST imeibwa leo. Yeyote atakayeiona naomba atupe taarifa

Gari aina ya IST imeibwa leo. Yeyote atakayeiona naomba atupe taarifa

Ukimiliki gari Bongo na hasa kama inalala sehemu ambazo siyo salama sana unatakiwa uwe walau na ma-ujanja ujanja. Pale inapolala chimbia chuma kubwa liende chini kabisa na lisionekane kwa juu. Chomea chuma kama komeo lakufunga kufuli na gari uwe unapaki juu ya hilo chuma. Baada ya kupaki ingia uvunguni mwa gari, funga nyororo kwenye lile komeo lishikane na difu ya gari kwa chini. Mwizi akipiga moto na kukanyaga mafuta gari haisogei. Njia nyingine ni kuweka alarm ya kuchimbia chini, ambayo unapaki gari na tairi inakanyaga ile alarm. Mwizi akisogeza gari tu uzito wa tairi ukiondoka una activate ile alarm.
Mimi gari yangu ya kwanza nilikuwa nafunga chain nne kama watu wa wrong parking nilijinyima sana kununua gari nikiwa na mshahara wa laki tano takeaway, mpaka nilipoamia kwangu na kuyazoea magari ,sasa ni mwendo wa Gps,camera na alarm kubwa kama ambulance acha nionekane mshamba.
 
Sambazeni kwenye magroup ya Whatsapp itapatikana tu. Pole sana mimi siwezi kupark gari nje kama hamna ulinzi hela imekua ngumu kweli na vijana wamecharuka wanataka kupanda juu ya meza.
Sawa Mkuu nalifanyia kazi hilo
 
Waliyokuibia wanakujuwa vizuri tu

Watakuwa

Ova
 
Back
Top Bottom