Siwezi kiwa na wivu kwenye liabilities. Gari kama hili kwa kazi kama ya Makonda ni liability.
Zaidi.
Sina ulimbukeni na magari.
Nimepark Mercedes Benz GLE 450 4Matic hapo nje, kijana wangu hajafika miaka 18 nimempa BMW X5 anaendesha kwenda nayo shule na gym, azoee haya magari tangu mtoto asilimbuke nayo ukubwani. Kama mimi nilivyoanza kuyaona utotoni.
Nimenunua kwa pesa yangu sijafanya kazi serikalini hata siku moja, sijakula rushwa hata senti moja. Ni pesa yangu kwa kazi yangu halali, hata ukiangalia kipato changu unaweza kuona namudu kuwa na hizo gari bila utata.
Wabongo wengi kama wewe hamuwezi kujadili kitu kidhahania. Hamuwezi kujadili hoja kwamba serikali ya nchi masikini jaitakiwi kuwa na mawaziri wanaoendesha magari ya anasa wakati watu wanakufa kwa kukosa dawa mahospitalini. Watu wanakufa for some basic shit.
Mtu akijadili hoja, lazima mnaweka personal things nje ya hoja.
Kwa sababu ndiyo uwezo wenu unapoishia.