Gari gani ya kwenda Arusha ni nzuri kwa mwendo na kwa muonekano?

Gari gani ya kwenda Arusha ni nzuri kwa mwendo na kwa muonekano?

Esther Luxury Coach linalosafiri usiku kupitia Bagamoyo, Saa 12 asubuhi na mapema mnaingia Chugga, vyakula vya usiku achana navyo hamna uhakika maana vingi linakuwa vimebakia mchana, by the way ukishakula chakula cha Jioni Dar huko njiani unataka Kula nini tena? Labda Juice au Soda
Kuna wasafiri kafiri wao kila chakula au kinywaji kinachopita usoni pake anataka anunue, hata yale mayai ya juzi atanunua, na akilimenya basi lote ...hapa weka neno lako kwani mimi nimekosa neno.
 
Hii gari ❌ Hili gari ✅

Hii basi ❌ Hili basi ✅

Tuendelee kuipenda lugha yetu.
 
Wakuu safari ni kesho
Nimeamua kupanda shabiby
Mniombee nifike safe
 
Wakuu heshima zenu,
Ninaomba kujua usafiri wa kwenda Arusha wa uhakika kwa muda wa usiku kutokea Dar es salaam.

Gari luxury kweli
Gari linalofika kwa wakati
Huduma nzuri (hotel ya chakula kizuri, wahudumu wenye kauli tamu zisizokera, na mengineyo)

Asanteni.
Hapo kwenye gari toa weka basi.
 
Nyie mnaocheka niliposema nna height phobia chekeni sana. Wengine pass Ilishajaa kwa safari za kimataifa. So ndege sio big issue.

Nchi zilizoendelea usafiri wa anga umerahisishwa ili kila mtu aumudu kwa ajili ya kurahisisha movement za watu.
So u heard it
Binti binti! Hicho kiinglish na michosho tunadanganyana kwa kujikweza hapa JF
 
KIDIA ONE. HUTAJUTA

WANATOA MAZIWA YA MOTO, CHAI, MAJI YA MOTO, KAHAWA.

CHOO NDANI KWA NDANI KWA HAJA NDOGO..
Mara ya mwisho kupanda kidia one ilikuwa kati ya 2017 -2019 sitosahau basi lilichemka moshi ukajaa ndani ikabidi tushuke, tulipigwa na mvua nililowa adi mifupa.
 
Binti binti! Hicho kiinglish na michosho tunadanganyana kwa kujikweza hapa JF
Boss nkudanganye nakujua??
Nlichoandika namaanisha. Kajinyonge na big G
 
Back
Top Bottom