Gari la mafuta linawaka moto muda huu maeneo ya Ubungo

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
6,736
Reaction score
10,669
Mliopo maeneo ya Ubungo na Kimara kibo, tupeni update ya hapo maana wengine wanakimbilia hatari.

===

Lori linalosafirisha Mafuta limepinduka na kusababisha Moto mkubwa katika maeneo ya Ubungo jirani na Kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi cha Kibo jijini Dares Salaam.

Jeshi la Zimamoto limefika eneo la tukio lakini kutokana na ukubwa wa Moto unaowaka eneo hilo, kazi ya uzimaji imekuwa na changamoto.

Hadi sasa bado haijafahamika madhara kamili yaliyopatikana kutokana na Ajali hiyo ingawa taarifa za awali zinaeleza baadhi ya Nyumba za jirani na Pikipiki 2 zimeteketea kwa Moto huo.



Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Wakuu nimeambiwa kuna moto unaendelea kuwaka maeneo ya kimara ubungo kuna moto mkubwa na mlipuko mkubwa sana unaendelea na nimeambiwa nyumba zinaungua moja baada ya nyingine.....

Sina uhakika bado kuwa ni nyumba au vituo vya petrol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…