Gari la mafuta linawaka moto muda huu maeneo ya Ubungo

Wakuu nimeambiwa kuna moto unaendelea kuwaka maeneo ya kimara ubungo kuna moto mkubwa na mlipuko mkubwa sana unaendelea na nimeambiwa nyumba zinaungua moja baada ya nyingine.....

Sina uhakika bado kuwa ni nyumba au vituo vya petrol
Ni nyumba apa zishaungua kama 13 ivi, boda boda 26 teyari ni vyuma chakavu. Magari 9 yote Amna kitu ..yani kwa ufupi ni moto fire 🔥🔥🔥
 
Kwa hali ya moto ulivyo watu wengi watakufa na huo moto unasambaa kwenye Maeneo ya watu Mungu wetu sote aepusha hili janga ni hatari ni hatari ni hatari sana
Moto ushazimwa hali ipo kawaida uzuri haikuwa petrol maana lazima kungesikika mlipuko mkubwa na madhara yangekuwa zaidi
 
Nilikuwepo eneo la tukio hakuna vifo Wala majeruhi (serious injury) ,mali zilizoteketea ni gari yenyewe ya mafuta ,piki piki mbili na vibanda kadhaa vya wafanya biashara gari limeangukia mtaroni kwahy Yale mafuta yamemwagukia kwenye mtaro.

Sababu ya ajali ni uzembe wa deleva alikuwa anawahi asikae kwenye foleni mataa , wakati amekaribia mataa alitaka kuchepuka njia ya pembeni(za kupigia u turn) sasa ni kama aligairi wazo lake la kupita pembeni, akairudisha gari main road .

Kilichotokea gari ikapanda juu ya matuta ya pembeni tire za nyuma zikawa zinaning'ing'a mtaroni sasa kutokana na mzigo mzito alioubeba chuma ndio ikapiga chini.

Ila moto unatisha jaman hiyo sauti yake sio poa kabisa ,hadi fire wenyewe tulikuwa tunashindana nao kukimbia, Kuna mama alikuwa na mtoto mgongon lakini zile mbio kama kalibeba chungwa aliliruka bango kama swala
 
Hawajaenda kuzoa mafuta kama kule morogoro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…