Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo

Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo

Chama kimebadili jina kinaitwa CCMAGEREZA(soma sisi magereza)
 
Unalipa magereza, hilo sio tatizo.
Litakuwa tatizo kama watatumiwa bila malipo, i.e serkali kupitia magereza wasilipwe.

Hata wewe unaweza kuwaita kulima au kazi yoyote halafu unalipa.
Ni sawa na kuchukua polisi akulinde unailipa serkali
Kwa hio magereza wanawanyonya wafungwa
 
Mbona hiyo kawaida kama una kazi yoyote nenda ukawatafute mbona watakufanyia kazi ! Hapo sion i tatizo hata nyumba ukiwahitaji wanakujengea
 
Unalipa magereza, hilo sio tatizo.
Litakuwa tatizo kama watatumiwa bila malipo, i.e serkali kupitia magereza wasilipwe.

Hata wewe unaweza kuwaita kulima au kazi yoyote halafu unalipa.
Ni sawa na kuchukua polisi akulinde unailipa serkali
Sisi tunalipa Kodi ili wao wale na kulala bure Sasa kuwatumikisha huo ni unyonyaji.
 
Kazi yao ni kupiga, kujeruhi na kuteka.
Then wanapewa teuzi,cv namba moja ni uwezo wako binafsi wa kuwashughulikia wapinzani,kuwabeza, kuwatukana hapa teuzi nje nje.Baada ya kutishia kuwauwa wapinzani akapewa uDC Arusha Kama fadhila.
 
Mbona wafungwa wanatumika kungoa visiki barabarani, Kuna wakati Ukienda wizarani mambo ya ndani utawakuta wanapiga usafi.....

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanasema kama una kazi yako unaweza kuwakodi.Chukua mfano CHADEMA au ACT,NCCR nao wakahitaji hiyo huduma ya kupandishiwa bendera mji wote na mabango MKUU wa Gereza atakubali kweli?
 
Ukiukaji mkubwa wa sheria ,katiba na maadili ya nchi.
IMG_20200707_174617.jpg
 
Back
Top Bottom