Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo

Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo

Salary Slip,

Hii ni kashfa kubwa sana. Yaaani hapa lazima watu wenye akili wajiulize kama watanzania tuna akili au la tukilifumbia macho hili.

Kutumia jeshi linalolipwa mishahara na posho kwa kodi za wananchi kwenye shughuli zako za siasa sio matusi tu kwa sheria na katiba ya nchi Bali ni matusi kwa wananchi wote wa Tanzania.
 
Hawa watu wameshajikatia tamaa na sasa wameamua semeni mtavyosema ila sisi hatujali.

Kama ni kupoteza,wameshapoteza sasa kwanini wahangaike huku hata muda umeshawatupa mkono?

Hata ile fomu yao kuandikwa ni ya kwenda kugombea uongozi wa vyombo vya dola sio tu ilikuwa lengo ni kutisha,bali ile ilikuwa ni dalili nyingine ya kukiri kukataa kwao tamaa na hivyo hawana tena cha kupoteza(hawawezi poteza mara mbili).

Hata kitendo hiki cha leo ni ishara nyingine ya wao kujikatia tamaa unless huduma hii ya kupandishiwa bendera wameilipa serikalini.

Wangekuwa wanaheshimu wapiga kura,wengeonyesha document kulipia huduma hii au kutoa ufafanuzi lakini kwakuwa hawajali na wamejikatia tamaa,wametuacha tuseme tunavyoweza ila wao hawajali.

Tunaomba document yenye control number kama uthibitisho wa kulipia hii huduma serikalini vinginevyo msilaumu watu kwa wanayoyasema mitandaoni kuanzia huko twitter,hapa JF na kwingineko.

View attachment 1500216
Ni aibu kubwa sana kwa chama kinachojiita kikongwe kuliko chama chochote barani Afrika, kikifanya mambo ya kitoto kiasi hicho!
 
Ndiyo hapo ujuwe kuwa lumumba hakuna mwenye uwezo wa kutumia angalau akili alizopewa bure na mungu
Aiseee ccm wamejichokea , hadi kupandisha bendera wanashindwa..wkt Kuna majo bless akina mgonjwa mtambuka, bia yangu..mama ntilie wa kawe..USSR, Yehova, sumve, na kipara kipya wapo tu na hawana kz yyte..au nao wamegoma??
 
Baada vyeo vya utumishi wa umma kugawanya bila hata ya aibu kwa makada kwa maelekezo maalum ktk tengua na teuzi zinazoendelea, pasipo hata kujali weledi ama mgongano wa kimaslahi, tena pasipo hata kuzingatia vyama vinaingia ktk kampeni za uchaguzi. Bado wanathubutu kufanya mambo haya ya aibu mbele ya umma wa Watanzania, tena ktk makao makuu ya nchi.
 
Alafu kuna mtu aliwaambia wapinzani wasipofuate sheria, wataishia jela!!!Sasa hapa sijui wao ndio wanazingatia hizo sheria?!
Kama wamewalipa magereza kuna tatizo gani? Tatizo nyie pesa za ruzuku mnanywea konyagi tu.
 
Hii kashfa ni kubwa kiasi inaweza kumtoa mtu madarakani kwa nchi zilizo serious kwenye kusimamia sheria na utawala bora. Huwezi kutumia jeshi kwenye shughuli zako za Kisiasa kwenye mfumo huu.
Haya ni matusi kwa watanzania wote.
 
Magereza kwa sasa wako kama JKT wanazalisha hata nyinyi Chadema mnaweza kuwapa tenda yoyote.
 
Toka maktaba :

18 Dec 2019
Dar es Salaam, Tanzania

BENDERA za CHADEMA zaondolewa USIKU wa giza

Kikosi kinachodhaniwa ni cha polisi kilionekana maeneo ya Mlimani city wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Jana usiku tarehe 17 disemba 2019, na bendera zote za chama cha CHADEMA ziliondolewa. Mlimani City kuna vikao vya chama cha CHADEMA kuandaa mkutano mkuu wa kuteua viongozi wa chama kama inavyotakiwa na sheria za nchi na taratibu za Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa.

More info :

19 December 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Mkutano Mkuu wa CHADEMA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe

amewashukia baadhia ya askari Polisi walioshusha bendera za chama hicho zilizowekwa barabarani kwenye mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam.
 
Nasikia kipara kipya na @wakudadavua hao wamepewa special offer ya kucheza ngoma kesho dodoma kwenye kikao cha mabosi wao.
Aiseee ccm wamejichokea , hadi kupandisha bendera wanashindwa..wkt Kuna majo bless akina mgonjwa mtambuka, bia yangu..mama ntilie wa kawe..USSR, Yehova, sumve, na kipara kipya wapo tu na hawana kz yyte..au nao wamegoma??
 
Hawa watu wameshajikatia tamaa na sasa wameamua semeni mtavyosema ila sisi hatujali.

Kama ni kupoteza,wameshapoteza sasa kwanini wahangaike huku hata muda umeshawatupa mkono?

Hata ile fomu yao kuandikwa ni ya kwenda kugombea uongozi wa vyombo vya dola sio tu ilikuwa lengo ni kutisha,bali ile ilikuwa ni dalili nyingine ya kukiri kukataa kwao tamaa na hivyo hawana tena cha kupoteza(hawawezi poteza mara mbili).

Hata kitendo hiki cha leo ni ishara nyingine ya wao kujikatia tamaa unless huduma hii ya kupandishiwa bendera wameilipa serikalini.

Wangekuwa wanaheshimu wapiga kura,wengeonyesha document kulipia huduma hii au kutoa ufafanuzi lakini kwakuwa hawajali na wamejikatia tamaa,wametuacha tuseme tunavyoweza ila wao hawajali.

Tunaomba document yenye control number kama uthibitisho wa kulipia hii huduma serikalini vinginevyo msilaumu watu kwa wanayoyasema mitandaoni kuanzia huko twitter,hapa JF na kwingineko.

View attachment 1500216
Picha inasema kwamba., Ndg, Mwenezi Polepole amepungukiwa maarifa kabisa, kitendo cha kutumia wafungwa kupandisha Bendera za Chama!!??

Sidhani kama Mwenezi wa Zamani ndg Nape angeruhusu upuuzi huu ufanyike..

Polepole wakulaumiwa kwa hili.
 
Yaani wanaiogopa cdm kuliko hata corona
Toka maktaba

18 Dec 2019
Dar es Salaam, Tanzania

BENDERA za CHADEMA zaondolewa USIKU wa giza

Kikosi kinachodhaniwa ni cha polisi kilionekana maeneo ya Mlimani city wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Jana usiku tarehe 17 disemba 2019, na bendera zote za chama cha CHADEMA ziliondolewa. Mlimani City kuna vikao vya chama cha CHADEMA kuandaa mkutano mkuu wa kuteua viongozi wa chama kama inavyotakiwa na sheria za nchi na taratibu za Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa.
 
Kumbe na wewe huna uhakika!!
Tatizo nyinyi mmekariri magereza ya zamani na si hii ya Magufuli. Magereza ya sasa ni kama JKT wanazalisha na wanatakiwa wajitosheleze kwa kila kitu na si kutegemea ruzuku toka serikalini. Hata nyinyi Chadema mkiwataka wawafanyie kazi haikatazwi ili mradi muwalipe. Magufuli amebadilisha mambo mengi sana tatizo nyinyi bado mna taswira ya magereza za zamani.
 
Back
Top Bottom